Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Ila Mimi kama mwalimu sijaona mantiki ya serikali kuwawajibisha watoto kwa makosa ya wasimamizi wa mitihani pamoja na wamiliki wa shule serikali iangalie namna ya kuwasaidia watoto hawa ikiwezekana warudie kufanya mtihani kwa gharama za waliopelekea kufutiwa matokeo yao.

Poleni sana Wahanga
Kwani waliogundua hii janjajanja sio wasimamizi? Je wasimamizi wangehusika wasingefukia mashimo???
 
Kama B ndo jibu sahihi wafanyaje?
Kama B ni sahihi hakuna tatizo, hayo ndio matarajio ya Baraza. Tatizo ni pale wanapoandika jibu moja lisilo sahihi mfano watahiniwa wote waandike A , wakati A ni kosa....!!!
 
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
Majibu yaliandaliwaje? Walichomoa Pepa na kupeleka nje ya chumba Cha mtihani au???
 
Hivi mkitafuta wanasheria hamuezi kuishitaki shule na ikawalipa mamilioni ya hela kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1. Wewe kama mzazi uliingia mkataba na shule kwa makubaliano ya kumpatia mwanao elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Kama mzazi ulitimiza wajibu wako wa kuhakikisha mtoto anaenda shule ikiwa ni pamoja na kulipa ada, kununua uniforms, madaftari nk.
2. Shule ilikuwa na wajibu wa kumfundisha mtoto na kumwandaa kufanya mtihani wa taifa, badala yake shule kama shule haikutimiza wajibu wake na ikachukuwa njia ya mkato ya kuvujisha mitihani ili kuficha uzembe wake.
3. Mzazi na mtoto kwa pamoja hamkuomba mtoto aonyeshwe mitihani ilikuwa ni utashi wa shule husika. Mimi nadhani watanzania tunauzembe wa kupuuza mambo ya msingi na kuita kupoteza muda. Kichwa ngumu kama mimi tungeishia kwanza mahakamani kwa kudai fidia ya mamilioni
Waasisi wa hii mambo ni wakubwa katika ngazi mbalimbali ambao Kila Leo hutoa matamko kutishi walimu wakuu kuwapokonya nafasi shule zikiwa za mwisho.... Hii ilipelekea wengi kujiingiza kwenye uhalifu na matokeo yake kukuta wasio jua kusoma na kuandika wakiingia sekondari.!!!
I'll
 
Haya Waambieni wajiandae kufanya mitihani Tarehe 21-22

Huo mtihani ni wa kukomolewa
 
Naona wametoa second chance
FB_IMG_1670690850071.jpg
 
POLENI SANA PRIVATE MPELEKE

ATHARI HAMNA MFANO MIMI NILISOMA UGANDA NIKAISHIA LA NNE NA NIKARUDI HAPA TZ NIKASOMA HADI CHUO NA BAADHI YA KAZI ZA SERIKALI NIMEFANYA NA CHUO MKOPO NILIPEWA

NB make sure mwanao anapata cheti Cha lasaba
Unamshauri atafute cheti feki badala ya kumwambia arudie la 7?
 
Kwa Sasa usajili wa mtoto kidato Cha nne unaanzia std 7 ndugu hvyo mtoto wako kama hajamaliza std asahau kuhusu mtihani
Ile prim no yake ya std 7 itahitajika form two na form four pia
Ndo sera ya elimu ya Sasa hvyo std 7 ni lazima
Mimi ni mwalimu naongea uhalisia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Je mtoto anaweza kufanya mtihani wa darasa la 7 kama mtahiniwa binafsi? Je kuna uwezekano kwa mtoto wa mwenzetu hapa, kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza, halafu akajisajili kama mtahiniwa binafsi ili mwakani afanye tena mtihani wa la 7 akiwa kidato cha kwanza?
 
Back
Top Bottom