Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Naomba kuuliza kma nakupata vizuri, Inamaana kwa mwaka 2023 anaweza kuanza kidato cha kwanza na ikifika muda wa kufanya mtihani wa darasa la saba anafanya ili aipate hiyo Prem namba? Je hiyo Prem namba ya mwaka huo wa 2023 itamruhusu kufanya mtihani wa kidato cha pili kwa 2024?
Noop afanye mtihani kwanza wa std 7,hatoanza form 1 bila prem no ya std 7 na tsm 9 yake inapelekwa Shule husika atakayoenda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri shule za private wanamchukua mtoto anapofaulu mtihani wao wa kujiunga na shule yao na si matokeo ya mtihani wa darasa la saba. Na pia haitaathiri mitihani mwingine ya sekondari au chuoni.
Hivyo nakuhimiza umtafutie shule atakayoweza kuendeleza na masomo ya sekondari. Usipoteze muda.
Huna akili, mambo yamebadilika
 
Pole sana rafiki inaumiza sanaa kufutiwa mtoto matokeo jamani daaahhh...!!!
I can feel youu!ila hizi private Jamani mi nadhani wangekua wanafungia shule ila siyo wanafunzi kufutiwa matokeo inaumiza sanaa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mwanafunzi ni mnufaika wa udanganyifu
 
Hapa watu wasikudanganye humu, mifumo ya elimu imebadilika namba aliyofanyia mtihani la 4 itamruhusu afanye mtihani wa la Saba

Na ya la Saba itamruhusu afanye mtihani wa form 2

Na ya form 2 itamruhusu afanye mtihani wa form4 kama akitaka kurndelea six kama atafaulu au chuo hizo namba za form 4 zitamruhusu aenedelee huko hamna mkato. Hapa dogo arudie tu apige Pepa ya std 7
Ushauri huu uzingatiwe. Kufutiwa mtihani kwa lugha nyepesi hatambuliki kama mtoto alimaliza std7. Wazee wa shortcut wasikuchanganye
 
Unaongelea miaka hiyo.Haya mabadiriko yameanza tangu 2019,au huyo ndugu yako kamaliza darasa la saba 2019? Ukitaka kujua mambo yamebadilika,mtoto wako afike darasa la sita kisha mrushe aende Form one kwakuwa tu ana uwezo uone kama utapata admission kama zamani
Hawajui Hawa lolote

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Inaukweli..kuwa nikienda baraza la mitihabi nitakuta matokeo ya mtoto wangu..wenye ufahamu tusaidie hili..maana kama wazazi tuna sintofahamu nyingi
Inategemea na sababu zilizopelekea kufutiwa hayo matokeo.Si kweli kuwa ukienda pale una uhakika wa kupewa hayo matokeo.Cha muhimu tu ni kwemda ili upate uhalisia lakini pia na hatma ya watoto wenu itakuwaje? Nachokiona hapa ni watoto kurudia mitihani tu swala linakuwa watarudia lini,mwaka huu au watasubiri tena Next year which is the worst case scenario kwa mtoto kupoteza mwaka mzima tena
 
Nafikiri shule za private wanamchukua mtoto anapofaulu mtihani wao wa kujiunga na shule yao na si matokeo ya mtihani wa darasa la saba. Na pia haitaathiri mitihani mwingine ya sekondari au chuoni.
Hivyo nakuhimiza umtafutie shule atakayoweza kuendeleza na masomo ya sekondari. Usipoteze muda.
Usimpotoshe tafadhari si sawa.Ingekuwa ni rahisi hivyo kwa mfumo wa sasa basi NECTA wasingekuwa na jeuri ya kufuta matokeo.Hizo shule za Private mwisho wa siku wanapeleka taarifa za wanafunzi wao NECTA.
 
Noop afanye mtihani kwanza wa std 7,hatoanza form 1 bila prem no ya std 7 na tsm 9 yake inapelekwa Shule husika atakayoenda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Nahisi umedanganya,, Mfano watoto waliosoma kenya primary ama uganda primary je hawaruhusiwi kusoma o level Tanzania?
 
Nahisi umedanganya,, Mfano watoto waliosoma kenya primary ama uganda primary je hawaruhusiwi kusoma o level Tanzania?
Hajadanganya,kuna utaratibu wao ambao wanapaswa kuufuata na watapewa na Baraza,hakuna anaekuja tu na kusoma bila kupitia pale NECTA kama mwisho wa siku utataka afanye mitihani ya Baraza.Inawezekana tu kama mtoto wako utataka asome mitaala ya Cambridge ambayo iko nnje ya NECTA
 
Prem haianzii std 7 inaanzia std toka std 1 namba ya usajili wa mwanafunzi ambao haukufutwa kilichofutwa ni matokeo.
 
Ushauri wangu! Nenda ofisi za halmashauri au mkoani, onana na DEO au REO akupe mwongozo kama kuna namna ya kuipata PREM number ya mwanafunzi na kujua kama itaathiri au kutoathiri kitu akienda sekondari. Mifumo ya elimu kwa sasa sio ya makaratasi ni online tu haina ujanja ujanja kama wa zamani ambao wengi wanausemea hapo juu

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Prem namba inapatikana shuleni aliposoma mtoto na kwenye matokeo ipo
 
Prem haianzii std 7 inaanzia std toka std 1 namba ya usajili wa mwanafunzi ambao haukufutwa kilichofutwa ni matokeo.
Mfano mimi mtoto wangu kafutiwa matokeo ila prem Number ipo, japo haina matokeo (W) je anaweza endelea std 7 au inapaswa arudie Darasa std7
 
Back
Top Bottom