Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Nitumie namba yako inbox. Nipo naunda group la Whatsapp la wazazi wa watoto wote ambao wamefutiwa matokeo. Tusimame pamoja na kuongea kwa sauti moja
Weka link hapa ya kujiunga WhatsApp mkuu ...
 
Wameonewa tu hao hadi shule za kayumba wameiba mitihani safari hii, ukitaka kujua hilo fuatilia matokeo ya nyuma na ya sasa
 
Hakuna mzazi anayeweza unga mkono uhuni huu, ikithibitika wafungiwe kabisa, I wazazi na watoto ni whanga katika jambo hili, yaani sio fair kwa mzazi ambaye hana Idea na hata watoto wengine hawana Idea ama ridhaa katika mazingira kama hayo ...
Huu ni unyanyasaji na ukatili mkubwa kwa wazazi na watoto Hawa. Watoto wamefanyiwa ubakaji kwa kushirikishwa uovu huu kwa vile tu ni watoto wasio na uwezo wa kubishana na waasisi wa uovu huu. Serikali Ione ukatili huu unaofanywa na wenye mashule dhidi ya watoto kwa manufaa Yao binafsi. Kuwahukumu na kuwanyima watoto haki za kielimu kwa uovu huu ni ubakaji kwa watoto. Serikali iangalie jambo hili kwa umakini . Ishughulikie waliosababisha haya na sio kuwaharibia watoto ubaadae wao. Please please please...... Kwani mtoto akishawishiwa kufanya ngono tunahesabu kafanya kwa ridhaa yake ????????! Serikali tafadhali iangalie mateso haya waliyosababishiwa watoto... Please !!!
 
Unaongelea miaka hiyo.Haya mabadiriko yameanza tangu 2019,au huyo ndugu yako kamaliza darasa la saba 2019? Ukitaka kujua mambo yamebadilika,mtoto wako afike darasa la sita kisha mrushe aende Form one kwakuwa tu ana uwezo uone kama utapata admission kama zamani

Mbona ulisema ajira bila kuonesha cheti cha darasa la saba hupati?
 
Nitajie ajira serikalini ambapo viambanisho ni pamoja na cheti cha std 7... Mimi kwenye faili langu la ajira hakuna hicho cheti.
Takukuru mkuu bila cheti cha drs la saba hupati kazi

Namba ya drs la saba inatumika kwa usajili wa mtihani wa taifa wa form two. Mambo yamebadilika atakayedharau drs la saba akifika mbele atakwama tu kufanya mitihani ya taifa labda kuwe na mabadiliko tena.
 
Haina athari ndugu. Anakosa tu admission shule za serikali.
Anaendelea sekondari kama kawaida na haitadhuru kufanya mitihani ya taifa ya kidato cha 2 na kuendelea.
Kwa sasa inaathari kubwa, kwa maana ya kwamba mtihani wa kidato cha pili namba itakayotumika kujisajili ni ile ya mtihani wake wa darasa la saba. Hii ni kama ambavyo namba ya kidato cha nne inavyotumika katika vyuo na bodi ya mikopo. Hivyo ni bora zaidi kuchelewa kwa mwaka huu mmoja kuliko kufika kidato cha pili ukajajutia baadae.
 
Poleni sana wazazi wenzetu mlioguswa.

Pole Kwa watoto wasio na hatia.

Karma iwakute walimu wanaocheza michezo michafu ili shule zao zionekane zinafaulisha sana wazidi kupata wateja.

Mpeleke tu private anapokelewa
Nakubaliana nawe kwa 100% isipokuwa maneno yako manne ya mwisho! Huko private watachukua ada zao za miaka miwili baada ya hapo hawatapata usajili wa kufanya mtihani wa kidato cha pili, kwa vile usajili utategemea namba ya kumalizia mtihani wa darasa la saba. Kama ambavyo namba ya kidato cha nne inavyotumika kusajiliwa chuo chochote. Wazazi mlioguswa na hili tatizo la wenye shule, fanyeni hima watoto wafanye huo mitihani, mtaja shukuru baadae. Labda kama kuna vigogo walioathirika na mwisho wa siku watabadili huu utaratibu. Mwisho wa siku hili sii LENU ni LAKO
 
Poleni sana wazazi wenzetu mlioguswa.

Pole Kwa watoto wasio na hatia.

Karma iwakute walimu wanaocheza michezo michafu ili shule zao zionekane zinafaulisha sana wazidi kupata wateja.

Mpeleke tu private anapokelewa
Kwan hiyo St Anne Marie si ni private pia? Au mie ndo sielewi?
 
Nitumie namba yako inbox. Nipo naunda group la Whatsapp la wazazi wa watoto wote ambao wamefutiwa matokeo. Tusimame pamoja na kuongea kwa sauti moja
Weka hapa bumber hiyo ili tutume msg kujiunga
 
Hivi mkitafuta wanasheria hamuezi kuishitaki shule na ikawalipa mamilioni ya hela kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1. Wewe kama mzazi uliingia mkataba na shule kwa makubaliano ya kumpatia mwanao elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Kama mzazi ulitimiza wajibu wako wa kuhakikisha mtoto anaenda shule ikiwa ni pamoja na kulipa ada, kununua uniforms, madaftari nk.
2. Shule ilikuwa na wajibu wa kumfundisha mtoto na kumwandaa kufanya mtihani wa taifa, badala yake shule kama shule haikutimiza wajibu wake na ikachukuwa njia ya mkato ya kuvujisha mitihani ili kuficha uzembe wake.
3. Mzazi na mtoto kwa pamoja hamkuomba mtoto aonyeshwe mitihani ilikuwa ni utashi wa shule husika. Mimi nadhani watanzania tunauzembe wa kupuuza mambo ya msingi na kuita kupoteza muda. Kichwa ngumu kama mimi tungeishia kwanza mahakamani kwa kudai fidia ya mamilioni
Sasa utamdai fidia nani??? Wew una uhakika gani mwanao bila kuibiwa pepa angefaulu.?? So wanafutiwa matokeo ili warudie mtihani bhasii hayo ya ada ndo risk zenyewe maana angefaulu bila kugundulikaa ungefurahi na kuimba pambio za shangwee[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
sijasema aangalie mtandaoni lama atakuta *W kwa sababu kituo kimefungiwa

mzazi nenda baraza matokeo ya mwanao yapo tena kwa ukamilifu wake kulingana na alichopata......

humu utapigiwa kelele tu... FATILIA MATOKEO YA MWANAO BARAZA...
Inaukweli..kuwa nikienda baraza la mitihabi nitakuta matokeo ya mtoto wangu..wenye ufahamu tusaidie hili..maana kama wazazi tuna sintofahamu nyingi
 
Kama bashite aka daudi baraza hawakumrebishia gamba enzi za simba wa yuda sembuse nyie st anne? Nimeona jina la kigogo wa polisi shilogile wengine mnapesa lakin hamna mamlaka.

Pepa ni 2023
 
Kwa kweli kwa hili selikali ingepitia upya sheria ya kuwafutia watoto matokeo kwa makosa yaliyofanywa na uongozi wa shule(sababu watoto si watu wazima na ingelikuwa ni watu wazima wote wasingeliingia kwenye mkumbo huo)...Mapendekezo yangu.
1. Serikali iingie gharama kuwapa watoto wote wa aina hiyo mtihani mwingine
2. Serikali ichukie hatua kali ikiwa ni pamoja na kuzitoza faini kubwa au kuzifungia shule zitakazobainika kufanya udanganyifu(zikifungiwa mbili ,tatu kwa miaka kuanzia 6-12 nyingine hazitajaribu kufanya upuuzi huo sababu mbali na kutoa huduma ya elimu wamiliki wa shule hizo wanaziendesha kibiashara) au au vyote kwa pamoja.
 
Kwa sasa inaathari kubwa, kwa maana ya kwamba mtihani wa kidato cha pili namba itakayotumika kujisajili ni ile ya mtihani wake wa darasa la saba. Hii ni kama ambavyo namba ya kidato cha nne inavyotumika katika vyuo na bodi ya mikopo. Hivyo ni bora zaidi kuchelewa kwa mwaka huu mmoja kuliko kufika kidato cha pili ukajajutia baadae.
Sasa namba ya darasa la saba si wanayo? Ambacho hawana ni matokeo ?
 
Back
Top Bottom