Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Ndugu zangu, usiku wa leo sijalala vizuri, nimefadhaishwa sana na kitendo cha mwanangu wa darasa la saba aliyekuwa anasoma shule ya St Anne Marie academy ya jijini Dar es Salaam kufutiwa matokeo. Yaani nina hasira kali sana kiasi sijajua nichukue hatua gani dhidi ya uongozi wa shule.

Naombeni tushauriane, kama wewe siyo mhanga wa jambo hili unaweza pita kimya kimya tu maana kwa sasa sihitaji kejeli, nahitaji faraja na ushauri.

Hivi mtoto ataenda private? Je, haiwezi kuwa na athari kwenye mitihani ya form four?

Naomba kuwasilisha.
Msipende mikumbo mnapotafutia watoto shule za kwenda kusoma kuna vingi vya kuchunguza kabla hujaamua kumpeleka hapo mtoto
 
Naungana na serekali kufungia matokeo baadhi ya shule serekali ipo sahihi kabisa uhuni wa shule za binafsi haukubaliki kabisa, maana haiwezekani ndani ya darasa moja, swali la kwanza wanafunzi wote wajaze B, swali la pili wanafunzi wote wajaze C swali la tatu darasa ZIMA wakose, swali la nne wanafunzi wote wapate, alkadhalika hivyo hivyo kwa maswali yote 25. This is evils.
Hicho sio kigezo cha kufutiwa watakuwa waliwekewa mtego, ila kwa sasa wapo wanabadiri majina ya shule na kusajiri upya, badara ya st.john utakuta shule inaitwa New st.john na usajiri ni miezi sita utakuwa umekamilika na hiyo new st.john mmiliki ni mtu mwingine sijui hapo sheria zinasemaje.
 
Kwa kweli kwa hili selikali ingepitia upya sheria ya kuwafutia watoto matokeo kwa makosa yaliyofanywa na uongozi wa shule(sababu watoto si watu wazima na ingelikuwa ni watu wazima wote wasingeliingia kwenye mkumbo huo)...Mapendekezo yangu.
1. Serikali iingie gharama kuwapa watoto wote wa aina hiyo mtihani mwingine
2. Serikali ichukie hatua kali ikiwa ni pamoja na kuzitoza faini kubwa au kuzifungia shule zitakazobainika kufanya udanganyifu(zikifungiwa mbili ,tatu kwa miaka kuanzia 6-12 nyingine hazitajaribu kufanya upuuzi huo sababu mbali na kutoa huduma ya elimu wamiliki wa shule hizo wanaziendesha kibiashara) au au vyote kwa pamoja.
Zaidi shule husika zigaramie gharama za watoto hao kurudia mitihani endapo serikali itaridhia. Jamani watoto wasiharibiwe ubaadae kwa makosa ya walimu wao na wamiliki wa shule.
 
Ndugu zangu, usiku wa leo sijalala vizuri, nimefadhaishwa sana na kitendo cha mwanangu wa darasa la saba aliyekuwa anasoma shule ya St Anne Marie academy ya jijini Dar es Salaam kufutiwa matokeo. Yaani nina hasira kali sana kiasi sijajua nichukue hatua gani dhidi ya uongozi wa shule.

Naombeni tushauriane, kama wewe siyo mhanga wa jambo hili unaweza pita kimya kimya tu maana kwa sasa sihitaji kejeli, nahitaji faraja na ushauri.

Hivi mtoto ataenda private? Je, haiwezi kuwa na athari kwenye mitihani ya form four?

Naomba kuwasilisha.
Nafikiri shule za private wanamchukua mtoto anapofaulu mtihani wao wa kujiunga na shule yao na si matokeo ya mtihani wa darasa la saba. Na pia haitaathiri mitihani mwingine ya sekondari au chuoni.
Hivyo nakuhimiza umtafutie shule atakayoweza kuendeleza na masomo ya sekondari. Usipoteze muda.
 
selikali ilibebe kama lilivyo ila shule itakuja kulipia kwenye Faini.
Zaidi shule husika zigaramie gharama za watoto hao kurudia mitihani endapo serikali itaridhia. Jamani watoto wasiharibiwe ubaadae kwa makosa ya walimu wao na wamiliki wa shule.
 
Pole sana rafiki inaumiza sanaa kufutiwa mtoto matokeo jamani daaahhh...!!!
I can feel youu!ila hizi private Jamani mi nadhani wangekua wanafungia shule ila siyo wanafunzi kufutiwa matokeo inaumiza sanaa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cheti ya darasa la saba ni kama cheti ya kipaimara tu.. hakina maana yoyote... Peleka mtoto private... Au nenda wizaran wanaweza kukusaidia kumpeleka shule mtoto

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
Kwa Sasa usajili wa mtoto kidato Cha nne unaanzia std 7 ndugu hvyo mtoto wako kama hajamaliza std asahau kuhusu mtihani
Ile prim no yake ya std 7 itahitajika form two na form four pia
Ndo sera ya elimu ya Sasa hvyo std 7 ni lazima
Mimi ni mwalimu naongea uhalisia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna uchawi hapo, anaenda sekondari kama kawaida, ishu ingrkuwa sisi ambao tunategemea mtoto afaulu tuuze kuku kumpatia pesa asome sekondari ya serikali
Kaka hyo ilikua zamani Sasa hivii itahitajika prim no ya std 7 kwanza hata huko private,na tsm 9 yake inaenda kule private
Sasa hivii Sheria zimebadilika mnooo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Sasa usajili wa mtoto kidato Cha nne unaanzia std 7 ndugu hvyo mtoto wako kama hajamaliza std asahau kuhusu mtihani
Ile prim no yake ya std 7 itahitajika form two na form four pia
Ndo sera ya elimu ya Sasa hvyo std 7 ni lazima
Mimi ni mwalimu naongea uhalisia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sawa nashukuru kwa kunifungua... Nilikuwa cjui haya mambo... Kumbe mambo yamebadilika... Asante sana

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
 
Waalimu wa sekondari waje watuambue nini umuhimu wa PREM NUMBER ambayo mtoto anatokanayo shule ya msingi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ndio kitambulisho chake Ile Prim no Sasa hivii mfumo umechange kabisaaaa bila std 7 matokeo hatakubaliwa sekondari maana form two pale Kuna prim zinajazwa za std 7 kama hana anarudi tena primary Drs la afanye mtihani wa la 7
Hvyo yapaswa umakini sana ktk maamuzi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Watu wengi humu wanajifanya wajuaji Sana wakati wanayoyaongea ni uongo.Siku hizi kuanzia shule ya msingi wako kwenye mfumo mmoja wa serikali.Kumhamisha mtoto shule ya private ni lazima kupita ngazi zote kwa mujibu wa serikali,unaanzia shuleni,unaenda kati hadi halimashauri.Nyie mdanganyeni wakati anaomba ushauri.Mifano mnayotoa ni ya Zamani.
Umemaliza kabisaaa Ndo ukweli ulivyo Sasa hv

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua NECTA wamefungia kituo cha mitihani (sio shule) fatilia matokeo yake yapo na utayapata.

usipotoshwe humu kwa sasa sajili za wanafunzi zinafanyika kuanzia primary na inahama kila mwaka na hata unapomuhamisha shule ni mfumo sio enzi zetu.

narudia Matokeo ya mwanao yapo na ukifatilia unayapata ni kituo cha mitihani ndicho kimefungiwa (sio shule)
Wanafutiwa matokeo ndugu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ila Mimi kama mwalimu sijaona mantiki ya serikali kuwawajibisha watoto kwa makosa ya wasimamizi wa mitihani pamoja na wamiliki wa shule serikali iangalie namna ya kuwasaidia watoto hawa ikiwezekana warudie kufanya mtihani kwa gharama za waliopelekea kufutiwa matokeo yao.

Poleni sana Wahanga
Watoto walipaswa waseme kama alivyofanya Iptisam vile

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hicho sio kigezo cha kufutiwa watakuwa waliwekewa mtego, ila kwa sasa wapo wanabadiri majina ya shule na kusajiri upya, badara ya st.john utakuta shule inaitwa New st.john na usajiri ni miezi sita utakuwa umekamilika na hiyo new st.john mmiliki ni mtu mwingine sijui hapo sheria zinasemaje.
NECTA si wajinga
 
Back
Top Bottom