Wazazi wenye Watoto wa Secondary wa Shule za Dar Kagueni Mashavu ya Watoto wenu kwani kuna Mmoja nimemuadabisha Kimara Stendi Juu Darajani leo

Wazazi wenye Watoto wa Secondary wa Shule za Dar Kagueni Mashavu ya Watoto wenu kwani kuna Mmoja nimemuadabisha Kimara Stendi Juu Darajani leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hakuna Kitu ambacho GENTAMYCINE nachukia kama Watoto wa Shule (Watoto zetu) kuwa na tabia za Matusi Matusi tena Hadharani ambako Watu wazima tupo au tunapita.

Leo mida ya Saa Mbili Usiku GENTAMYCINE nilikuwa nakatiza zangu Kimara Juu Darajani na nikakuta Wanafunzi wa Upili (Secondary) wakiwa wamejikusanya njiani na Mmoja Wao anatukana Matusi makubwa ya Nguoni huku Wenzake wakifurahia na Wapita Njia wakiwaangalia tu.

GENTAMYCINE nikiwa kama mrekebishaji wa tabia (kote kote) hapa JamiiForums na Uraiani sikupenda Kitendo kile kwani Kiungo kilichokuwa Kinatukanwa ni cha Waliotuweka Matumboni mwao Miezi Kenda / Tisa, Kutuzaa, Kutulea na leo kuwa Wakubwa (Wababa) hivi huku Wengine hata tukitwaa Tuzo za Mwanachama Bora wa Majukwaa husika (Ukinuna Jinyonge Ufe) nikaona nisilinyamazie.

Hivyo nikajivisha Ushujaa wa muda pale Juu Darajani Kimara na kwenda walikokuwa na Kumuuliza yule aliyekuwa Akitukana hovyo kuwa Kulikoni anakosa Adabu vile?

Kwa Kujiamini kabisa na bila ya Uwoga akanijibu Kunya (Hovyo) huku akinidindia ambako nami GENTAMYCINE nikaona si vibaya sana kama nikiyatumia Mafunzo Tukuka aliyoniachia The Late Bruce Lee kama Urithi ambako wakati ananiletea Kibesi na Kutunushia Kifua chake nikampiga Kofi (Kelebi) moja takatifu la Kimedani (Kung Fu) ya Kujifunzia katika Video Chumbani nikaona Kanywea na Wenzake kula Manyoya (Kukimbia) kushuka chini.

Hivyo nikabaki nae huku akiwa anaugulia Kofi langu la Kimedani na kuanza kuwa Mpole Kwangu na Kuniomba Radhi huku Akikiri kuwa kweli alikosea.

Kwakuwa GENTAMYCINE upande wa Pili wa Moyo wangu Umeumbwa na Huruma nami Roho Mtakatifu akaniingia ghafla na Kumhurumia na Kumsamehe huku nikimtaka asirudie tena na kumtaka akifika Nyumbani upesi sana atafute Barafu kisha aigandishe Shavuni Kwake ili Maumivu ya Kelebu / Kofi langu yapungue na ikitokea Mru (siyo Mzazi) akimuuliza kwanini Shavu limevimba adanganye Jino limevimba ila kama Mzazi wake ( hasa Baba yake ) akimuuliza Kulikoni Shavu lake limevimba asifiche na asiongope bali aseme Kapigwa (Kaadhibiwa ) kutokana na Upumbavu na Ujeuri wake wa Kuiga Masela wakati akina GENTAMYCINE ndiyo Masela wa Kitambo hicho na mpaka leo ni Msela vile vile.

Wazazi fanyieni Kazi sana Nidhamu za Watoto wenu hasa hasa hawa wa Secondary Schools (Shule za Upili) kwani ni Jeuri, hawana Maadili na Adabu kabisa katika Jamii.

Na leo (hapa hapa) natangaza rasmi kuwa Kesho nitakuwa ama Segerea au Mbezi Louis (Maeneo ya Vituoni) na nitaendelea kimya kimya na hili Jukumu nililojipa Mwenyewe la Kurekebisha tabia za Vijana ( hasa Wanafunzi wa Kiume) na kwa Watakaokaidi Urithi wangu wa Kujifunzia Kung Fu za Legend Late Bruce Lee kupitia Video za zamani za mfumo wa VHS utawahusu.
 
Mambo ya balehe hayo, kipindi cha majaribu sana hicho kwa vijana, makofi mawili matatu sio mbaya.
Nilimpa Keleb / Kofi Moja tu takatifu na kuweweseka huku akichafua na hali ya Hewa ( Akijamba bila Kukusudia ) na sijui kama hakutoa pia kiaina na Punje ya Nnya ( Puu ) yake.

Hakuna Kitu GENTAMYCINE nachukia kama Matusi ( hasa kwa Watoto au Wanafunzi ) na sitoacha Kuwanyoosha.
 
Madogo wapo kwenye ile stage iliobatizwa majina mengi kama ujuha/puberty/Adolescence/Balehe/Foolish age ambapo wakimaliza 4m4 ndo hao wakijiunga humu JF ni full matusi
 
Siku watakuchoma spoku/spoke za mapaja ndio utajuta.

Ukija Arusha fata mambo yako maana watoto hao wanatembea na pisto (pistol), bisibisi (screw driver) na spoke (spoku) hawakawii kukutoa upepo (kukutoboa tumbo).
 
Back
Top Bottom