Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Wazee wa Mathematics: Jibu lipi ni sahihi hapa?

Safi, wanachanganya na hii
IMG_20220904_104048.jpg
 
Kujibu mjinga ni ufedhuli, kama hujui kitu nyamaza uonekane mwerevu, jibu ni 1 ila kwavile wewe ni mjinga utaendelea na ubishani

Fafanua tuone uerevu wako sio kukalia maneno tu huku kichwani hamna kitu, hata Kanga nayo inayo maneno.

Kama 6÷2(2+1) =1, na 6÷[2(2+1)] itakuwa ngapi??.

🤣🤣🤣
 
Fafanua tuone uerevu wako sio kukalia maneno tu huku kichwani hamna kitu, hata Kanga nayo inayo maneno.

Kama 6÷2(2+1) =1, na 6÷[2(2+1)] itakuwa ngapi??.

🤣🤣🤣

6÷{2(3)}=1

6÷2(3)=1

6÷2*3=9

Usishupaze fuvu ntakupiga makofi sasa😀😀😀
 
BODMAS, B=Bracket, O=Order, D=division, M=multiplication, A=Addition , S=Subtraction.

You have to firstly deal with numbers in brackets, then deal with those numbers with "orders" (ie powers, square roots etc) then you follow the other operations as per order.
MAPEGAZIJUTO... I like it waeleze hao waswahili wabishi
 
Unaanza kufanyia kwenye mabano kwanza, maana hiyo ni conditional.
Baadaye ndo Magazijuto.

Jibu sahihi ni 9
Umekosea, kitaalamu hayo mabano huwezi kuyafungua bila kuzidisha hiyo mbili iliyo nje ya mabano. Usisahau kuwa 2 ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani ya mabano kwasababu hakuna tendo la kuzidisha hapo katikati. Kitaalamu hiyo mbili ya nje ya mabano ni common factor ya (2 +1). Inawezekana ulikimbia hesabu za factorization wewe. Scientific calculator iko sahihi
 
Hebu na sisi tujaribu:

6÷2(2+1)= 6÷2×3, kulingana na sheria ya BODMAS, yaani MAGAZIJUTO lazima uanze na 6÷2 na ndipo jibu lake uzidishe kwa 3; yaani (6÷2)×3=3×3=9.
Umekosea, kitaalamu hayo mabano huwezi kuyafungua bila kuzidisha hiyo mbili iliyo nje ya mabano. Usisahau kuwa 2 ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani ya mabano kwasababu hakuna tendo ka kuzidisha hapo katikati. Kitaalamu hiyo mbili ya nje ya mabano ni common factor ya (2 +1). Inawezekana ulikimbia hesabu za factorization wewe. Scientific calculator iko sahihi
 
Hapa hatupimani nani anajua zaidi bali ni suala la kuelimishana tu kwani hakuna anayejua kika kitu isipokuwa Mungu tu.

Haya hebu tuanze darasa:-

6÷2(2+1), hii ni sawa na kuandika, 6÷2×(2+1), kwa sheria ya MAGAZIJUTO (forget about BODMAS), lazima tuanze na expression iliyomo ndani ya mabano "MA" yaani (2+1) ambapo unapata 3, hivyo expression nzima inakuwa hivi; 6÷2×3; katika expression hiyo kuna matendo mawili; tendo la kugawanya na kuzidisha, kwa sherai ya MAGAZIJUTO ni LAZIMA uanze na kugawanya ndipo umalizie na kuzidisha kwani MA= Mabano, GA=Gawanya, ZI=Zidisha, JU=Jumlisha, TO=Toa, kwahiyo 6÷2×3 ni sawa na (6÷2)×3,

Yaani, 6÷2×3=(6÷2)×3= 3×3=9.

Kama unayohoja hapo karibu tujadiliane kwani kujadilana ni moja ya njia ya kujifunza, ni kitu ambacho wenzetu Wazungu hufanya na hivyo kujiongezea elimu, tofauti kwa sisi Waafrika ni mashindano ya nani anajua zaidi hatimaye siku zote tupo nyuma ya Wazungu.
Umekosea, kitaalamu hayo mabano huwezi kuyafungua bila kuzidisha hiyo mbili iliyo nje ya mabano. Usisahau kuwa 2 ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani ya mabano kwasababu hakuna tendo ka kuzidisha hapo katikati. Kitaalamu hiyo mbili ya nje ya mabano ni common factor ya (2 +1). Inawezekana ulikimbia hesabu za factorization wewe. Scientific calculator iko sahihi.

Ngoja nikufundishe kidogo huenda ukaelewa zaidi
6÷2(2+1) mathematically si sawa sawa na 6÷2x(2+1). Moja jibu lake ni tisa na nyingine jibu lake ni moja. Hata kama ingetokea majibu yakafanana lkn solution ya kusolve ni tifauti kabisa..

Mfano
2(2+2) si sawa sawa na 2x(2+2) hata kama majibu ni sawa au yanafanana. Tazama uchanganuzi hapa chini.

Kwenye 2(2+2), mbili ya nje ya mabano ni common factor hivyo kufungua mabano huwa inazidishwa na kila namba ya ndani 2x2+2x2=8. Kwa maana nyingine hapo BODMAS hai apply kwasababu hakuna tendo la kuzidisha hapo.
Wakati kwenye 2x(2+2) kuna matendo zaidi ya moja so, lazima ua apply BODMAS na unaanzia ndani ya mabano inakuwa ni 2x4=8. Ingawa majibu yanafanana lakini hizo ni solutions mbili tofauti, na tofauti yake utaiona pale unapopata equation yenye matendo mengi.
 
Pale unapofungua mabano inatakiwa uzidishe na Ile mbili nje Mana Ni Kama imerahisishwa tu ikatolewa nje mkuu. Sijui Kama unaelewa. Yaani Ile kutolewa nje inabidi uirudishe ndani Mana imebeba namba zote zilizo ndani sema amerahisisha kihesabu
Exactly
 
Nafunga Mjadala kama hamjaelewa hapa tena basi:
Baada ya kufungua mabano inafuata zidisha, namaanisha 2(3) = 2x3 hapo tuko wote? Siku zote ukifungua mabano kinachofuata ni ZIDISHA.
Sasa umekariri MAGAZIJUTO kuwa formula yake siku zote ukitoka mabano unafata gawanya kitu ambacho calculator ya simu imefanya. Ila sasa kwa hesabu au hisabati sio lazima uende gawanya formula inaweza kuwa MAZIGAJUTO narudia MAZIGAJUTO na sio MAGAZIJUTO kwa sababu MULTIPLICATION and DIVIDE are interchangeable. .
Kwa formula ya MAZIGAJUTO jibu ni 1, na ni sahihi kabisa kwa standard mathematics na ndio jibu mama.
Pia kwa formula ya MAGAZIJUTO jibu ni 9, na ni sahihi kabisa haujakosea, uko sahihi. .

Go back to my explanation above post 27 nimefafanua. .
Wewe naye umewavuruga tu watu hapa. Wambie warejee hesabu za factorization za form two, wataelewa kuwa mbili ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani, imekuwa factorized au tunaweza ita ni common factor
 
Umekosea, kitaalamu hayo mabano huwezi kuyafungua bila kuzidisha hiyo mbili iliyo nje ya mabano. Usisahau kuwa 2 ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani ya mabano kwasababu hakuna tendo ka kuzidisha hapo katikati. Kitaalamu hiyo mbili ya nje ya mabano ni common factor ya (2 +1). Inawezekana ulikimbia hesabu za factorization wewe. Scientific calculator iko sahihi

Nimekimbia hesabu za factorization??!!--- ungekuwa unanijua vyema ungeona aibu kwa hiyo kauli yako.

Ili uzidishe hiyo factor 2 na iwe ni sehemu ya namba zilizomo ndani ya hayo mabano katika lugha ya kimahesabu hiyo expression ilipaswa iwe hivi:-

6÷[2(2+1)], hapo sasa hii part [2(2+1)] inakuwa sawa na 6.

Kifupi Unachosema ni hiki; 6÷[2(2+1)]=1 na sio 6÷2(2+1). Kuna tofauti kati ya hizo expressions mbili.
 
mkuu ndio jibu ni moja ? acha kupotosha umma mkuu, tafuta mkali wenu wa hesabu muulize au iandike kwenye karatasi uifanye uone mkuu hesabu haifanywi kwa macho [emoji1787]
Jibu ni moja mkuu. Rejea factorization za form two
 
madam hapana jibu ni 9 hesabu haina majibu mawili na ndio maana ni rahis kupata mia na ndio maana ma TO wengi wanatokaga PCM sababu haya msomo hayana janja janja majibu yake ni universal na vitu kama hivyo
Jibu ni moja. Rejea theories zako za hesabu vizuri
 
Umekosea, kitaalamu hayo mabano huwezi kuyafungua bila kuzidisha hiyo mbili iliyo nje ya mabano. Usisahau kuwa 2 ya nje ya mabano ni sehemu ya namba za ndani ya mabano kwasababu hakuna tendo ka kuzidisha hapo katikati. Kitaalamu hiyo mbili ya nje ya mabano ni common factor ya (2 +1). Inawezekana ulikimbia hesabu za factorization wewe. Scientific calculator iko sahihi.

Ngoja nikufundishe kidogo huenda ukaelewa zaidi
6÷2(2+1) mathematically si sawa sawa na 6÷2x(2+1). Moja jibu lake ni tisa na nyingine jibu lake ni moja. Hata kama ingetokea majibu yakafanana lkn solution ya kusolve ni tifauti kabisa..

Mfano
2(2+2) si sawa sawa na 2x(2+2) hata kama majibu ni sawa au yanafanana. Tazama uchanganuzi hapa chini.

Kwenye 2(2+2), mbili ya nje ya mabano ni common factor hivyo kufungua mabano huwa inazidishwa na kila namba ya ndani 2x2+2x2=8. Kwa maana nyingine hapo BODMAS hai apply kwasababu hakuna tendo la kuzidisha hapo.
Wakati kwenye 2x(2+2) kuna matendo zaidi ya moja so, lazima ua apply BODMAS na unaanzia ndani ya mabano inakuwa ni 2x4=8. Ingawa majibu yanafanana lakini hizo ni solutions mbili tofauti, na tofauti yake utaiona pale unapopata equation yenye matendo mengi.

Hicho unachosema ni special case inayo involve operations za zidisha na gawanya lakini hiyo case hai apply kwenye expressions zenye mchanyiko wa operations (mfano operatiins za kujumlisha na kutoa).

Unachosema ni hiki, mfano;

2(2+1)=(2×2)+(2×1) ambapo hiyo ni sawa na 2×3=6, kwa maana hakuna tofauti kati ya 2×2+2×1 na 2×3, wewe umefungua brackets kwa kuzidishia hiyo 2 na mimi nimekokotoa ndani ya brackets kwanza halafu nikazidisha kwa 2, unapata jibu lile lile moja tu.

Tofauti ni pale operations za jumlisha na toa zinapokuwa involved hapo ni lazima u deal na kile kilichomo ndani ya mabano kwanza na sio kuzidishia hiyo factor.
 
Sioni tofauti ya MAGAZIJUTO na BODMAS
MA = BO
GA = D
ZI = M
JU = A
TO = S
NO.......BODMAS ni MAPEGAZIJUTO
..
MA=Mabano
PE=kipeou au vipeuo
GA=Gawia
ZI=Zidisha
JU=Jumlisha
TO=Toa
Ndicho alichoelezea ila MAJIBU YOTE NI CORRECT....
 
6÷{2(3)}=1

6÷2(3)=1

6÷2*3=9

Usishupaze fuvu ntakupiga makofi sasa😀😀😀
Heeeeeh hivi namba inaweza kuwekwa ndani ya mabano bila matendo ya kihisabati eti 2(3) 😅😅😅...ok ni hivi
2(3) ni sawa sawa na kusema 2×3....
Hivyo basi 6÷2×3= na ngapi leta jibu basi...
 
Back
Top Bottom