Wazee wa Mkataba Mwitongo ndio walishauri Nchimbi arudishwe kwenye Uongozi

Wazee wa Mkataba Mwitongo ndio walishauri Nchimbi arudishwe kwenye Uongozi

OOps!!! unaongelea jeshi gani???sijakuelewa ndugu.
Nafikiri anaongelea jeshi Nicaragua 🇳🇮 maana hili la kwetu majenerali wote ni makada waandamizi wa CCM na wanapakuliwa minyama kama watawala sasa kuwaambia habari hizo watakuona unataka kuwanyang'anya tonge mdomoni. .Majeshi yote hadi TISS wamejaa makada wa CCM.
 
Sema wewe kaka mkubwa uliyeshikilia katikati.

Mimi nilipoona jina la Mwitongo nikastuka kidogo.

Nikauliza, huu mkataba ni watu wamekutana kweli? Au mtoa mada anatumia poetic license tu kunogesha habari, akimaanisha kuwa kuna upendeleo katika kupata viongozi?

Maana haya ni mambo mawili tofauti.

Kuwepo kwa kikao kilichopanga upendeleo maalum kwa watoto wa viongozi ni tofauti sana na spirit ya kuwapendelea watoto wa viongozi inayoibuka organically tu.
Kwa uelewa wangu Mimi hili jambo lipo!

Linaonekana kabisa!! Hata uwe unapiga kazi vipi kama huna was kukushika mkono huchomoki labda ujiunge chama Cham wajenzi huru kama kina meko na mkapa ndio uchomoke!!
 
Inawezekana kuna upendeleo.

Lakini je, kuna kikao kilikaa na kupanga upendeleo huu uwepo rasmi?

Au ni upendeleo ule wa kawaida tu wa kujuana unaojengeka bila kikao maalum?

Mtoa maada kasema kuna kikao maalum kilipanga, kuna maswali anakimbia kuyajibu.
 
Yani watu walikaa chini wakakubaliana hivyo kabisa? Wewe umejuaje hilo?

Sikatai kwamba inaonekana kuna upendeleo, watoto wa watu fulani wanaonekana kupata nafasi za uongozi kirahisi, tunapata picha kwamba majina yanawasaidia. Hilo kulibishia ni vigumu.

Lakini, unatuambia kuna kikao kilikaa na kupanga hili kabisa?

Umejuaje? Unaweza vipi kuthibitisha haya maneno ni ya kweli na si chumvi za conspiracy theories tu?

Mbona watoto wengine kama kina Kippi Warioba kila wakigombea wanakatwa tu, kaka Kippi kagombea u Meya Dar kashindwa, kagombea ubunge Kawe kashindwa.
Alikuwa mkuu wa wilaya huko Moshi akaacha ili agombee ubunge. Wajumbe wakamfanya kitu kibaya.
 
Alikuwa mkuu wa wilaya huko Moshi akaacha ili agombee ubunge. Wajumbe wakamfanya kitu kibaya.
Kaka Kippi alivyokatwa Kawe kuna kinamama walilalamika sana, nikajua kweli Kippi anapendwa na watu lakini CCM kama alivyosema Kaka Makongoro ina mambo ya ziada mengi sana.

Kaka Makongoro mwenyewe alikatwa akaenda kugombea NCCR Mageuzi kupata ubunge Arusha Mjini.
 
Yani watu walikaa chini wakakubaliana hivyo kabisa? Wewe umejuaje hilo?

Sikatai kwamba inaonekana kuna upendeleo, watoto wa watu fulani wanaonekana kupata nafasi za uongozi kirahisi, tunapata picha kwamba majina yanawasaidia. Hilo kulibishia ni vigumu.

Lakini, unatuambia kuna kikao kilikaa na kupanga hili kabisa?

Umejuaje? Unaweza vipi kuthibitisha haya maneno ni ya kweli na si chumvi za conspiracy theories tu?

Mbona watoto wengine kama kina Kippi Warioba kila wakigombea wanakatwa tu, kaka Kippi kagombea u Meya Dar kashindwa, kagombea ubunge Kawe kashindwa.
Baba yake anakosoa saana serekali
 
Mkataba Mwitongo ni mkataba ulio asisiwa enzi za Mkapa na ukiwa na lengo la kuhakikisha watoto wote wa watawala wanapewa kipaumbele au upendeleo katika kila nyanja, ikiwemo Siasa,uongozi au hata Uchumi.

Kamati ya huu Mkataba kwa sasa inaongozwa na Mzee Mizengo Pinda, na pia inawatu kama Yusugu Makamba, Msuya,Piusi Msekwa, Anna Makinda, na washauri kama Mstafu Kikwete, na Mstafu Mwinyi, na pia wastafu wa Zanzibar.

Hii kamati ndio huwa inapokea majina ya watoto wa viongozi wanao hitaji nafasi mbali mbali za juu, na wanacho fanya ni kupitia hayo majina na kumpatia Raisi ili sasa awaangalie kwenye teuzi.Pia endapo kuna mtoto anataka examption za Kodi, Upendeleo kwenye maswala tenda na maswala mengine.

Emanueli Nchimbi wakati mkataba unaasisiwa alikuwa UVCCM, na inaaminika alitoa mchango mkubwa sana wa mawazo na ya jinsi huu mkataba utatekelezwa na ndio maana wazee wakaona ni lazima Mama amrudishe Emanul kwenye nafasi za juu either ndani ya Chama au Serikalin yaani awe active katika siasa na sio kuwa Balozi.

Kumbuka pia huu mkataba ulifutwa na Magufuri wakati wa utawala wake na hakutaka kusikia huo ujinga kamwe.

Hii kamati pia ina kazi ya kupokea malalamilo kutoka kwa watoto wa wastafu wote, endapo wanakumbana na Changamoto zozote, kunyanyaswa labda na TRA, na mamlka zingine au kupewa nafasi ambazo hazina hadhi, Watoto wengi hawataki ukuu wa wilaya wala Mkoa,wanataka sana Ukurugenzi au nafasi zingine za hadhi yao.

Kilicho fanya Magufuri afute huu mkataba ni kitendo cha watoto wengi kuwa wanapitisha mizigo free Bandarini, hilo Magufuri alilipinga sana na Ridhiwani ndio mtoto wa kwanza kukumbana na kizingiti hichi wakati wa Magufuri mara baada kuwa alikuwa mtoto wa wa Mstafu anaye pitisha mizigo mingi sana Bandarini free.

Kama ni mfuatiliaji wa mikutano ya Halimashauri kuu za CCM wakati wa Magufuri,kuna siku Yusufu makamba aliwahi tamka ndani ya mkutano kwamba Raisi wetu sio mtu wa vimemo hivyo msimsumbue na vimemo vya teuzi, ndio kipindi hicho Magu alikuwa ametoka kupiga pini huo mkataba Mwitongo.

Kumbuka awamu ya mama huu mkataba Mwitongo uko implemented kwa 100%
Watoto wa Nyerere, Warioba, Msuya, Dr Salim, Lowassa, Sumaye, Sokoine, Malecela na watoto wa Magufuli mwenyewe huu mkataba unawahusu au ni kakikundi furani pekee?
 
Mkataba wa mwitongo haupo.

Ukiniambia mkataba wa CCM wanamtandao, utaeleweka kirahisi.

Ni mkataba wa kuruhusu viongozi kufanya Biashara ndani ya uongozi na upendekeo wa Wala RUSHWA.

Ni mkataba wa waliovunja azimio la Arusha. Mkataba huo hauhusishi wazalendo wa Nchi kama Nyerere, Warioba, Mkapa, Magufuli nk nk.

Magu alijaribu kuuvunja na hakumaliza KAZI, Ajaye atamaliza KAZI Kwa ufasaha.

Tusubiri.
 
Siyo lazima viongozi wawe wanazaa viongozi.

Lakini, tukija kutafuta watu wenye usomi, hususannhuu wa kupima darasani, wenye kujuana na watu, wenye kuandaliwa vizuri kushika uongozi, hatutazunguka humo humo kwenye watoto wa viongozi na ndugu zao?
Kwenye usomi na watu walioandaliwa sio lazima kuzunguka humo humo kwa watoto wa viongozi na ndugu zao, Tanzania ina watu wengi wasomi wenye akili sana na wenye kukidhi vigezo vyote vya kuwa viongozi bora ambao sio watoto wa viongozi lakini wengi wao hawapati fursa hiyo ya uongozi au wanavurugwa njiani wanapoteana kabisa.
 
Kwa maana nyingins inayo eleweka kirahisi ni kwamba Ccm ni chama cha kifamilia zaidi.

Kama mzazi wako haja wahi kuwa kiongozi kwenye hii nchi, basi sahau teuzi. Hiyo ndiyo CCM. Na bado kuna watu wana iligia makofi

Mzazi wa Paul Makonda (DB) ni nani na amewahi hudumu katika nafasi ipi ya uongozi wa hii nchi na ndani ya CCM mpk useme kupata madaraka lazima mzazi wako awe ameshika hatamu ya uongozi wa juu? Orodha ni ndefu, ungana nao ule matawi ya juu!
 
Mkataba wa mwitongo haupo.

Ukiniambia mkataba wa CCM wanamtandao, utaeleweka kirahisi.

Ni mkataba wa kuruhusu viongozi kufanya Biashara ndani ya uongozi na upendekeo wa Wala RUSHWA.

Ni mkataba wa waliovunja azimio la Arusha. Mkataba huo hauhusishi wazalendo wa Nchi kama Nyerere, Warioba, Mkapa, Magufuli nk nk.

Magu alijaribu kuuvunja na hakumaliza KAZI, Ajaye atamaliza KAZI Kwa ufasaha.

Tusubiri.
Mkapa alikuwa na uzalendo gani? fuatilia uuzaji wa NBC hadi Baba wa Taifa akadinidha machozi, Mkapa muondoe hapo.
 
Kwenye usomi na watu walioandaliwa sio lazima kuzunguka humo humo kwa watoto wa viongozi na ndugu zao, Tanzania ina watu wengi wasomi wenye akili sana na wenye kukidhi vigezo vyote vya kuwa viongozi bora ambao sio watoto wa viongozi lakini wengi wao hawapati fursa hiyo ya uongozi au wanavurugwa njiani wanapoteana kabisa.
Sawa,

Naelewa.

Lakini uongozi si usomi tu pia. Kuna vetting.

Tatizo ni kwamba, tuna realities mbili.

Tuna reality ya kikatiba na kisheria, inayotaka haki sawa kwa wote.

Halafu tuna reality ya kiutamaduni. Hii haijali haki sawa kwa wote. Kwenye utamaduni unampendelea mtu wa familia yako, ndugu yako, jirani yako, mtu unayemjua siku nyingi kwanza.

Kisukuma hata kusalimiana tu mtu mkubwa anakuuliza "ng'wa nani?". Anataka kujua umetokea nyumba gani? Babu yako nani, bibi yako nani?

Utamaduni wetu umekaa kichifuchifu bado, kindugundugu, maisha ya kujuanajuana.

Lakini sheria zetu na katiba zinataka watu wote wawe na fursa sawa, bila kujali kujuana.

Na katika mgongano wa utamaduni na sheria, mara nyingi utamaduni unashinda na sheria inapindishwa.
 
Tunatakiwa tuachane na huu utamaduni wa kijima kwani unatuchelewesha sana katika uwajibikaji na maendeleo. Tamaduni nyingine zimepitwa na wakati na zina hasara nyingi kuliko faida.
 
Back
Top Bottom