Wazee wa Mkataba Mwitongo ndio walishauri Nchimbi arudishwe kwenye Uongozi

OOps!!! unaongelea jeshi gani???sijakuelewa ndugu.
Nafikiri anaongelea jeshi Nicaragua 🇳🇮 maana hili la kwetu majenerali wote ni makada waandamizi wa CCM na wanapakuliwa minyama kama watawala sasa kuwaambia habari hizo watakuona unataka kuwanyang'anya tonge mdomoni. .Majeshi yote hadi TISS wamejaa makada wa CCM.
 
Kwa uelewa wangu Mimi hili jambo lipo!

Linaonekana kabisa!! Hata uwe unapiga kazi vipi kama huna was kukushika mkono huchomoki labda ujiunge chama Cham wajenzi huru kama kina meko na mkapa ndio uchomoke!!
 
Kwa uelewa wangu Mimi hili jambo lipo!

Linaonekana kabisa!! Hata uwe unapiga kazi vipi kama huna was kukushika mkono huchomoki labda ujiunge chama Cham wajenzi huru kama kina meko na mkapa ndio uchomoke!!
Inawezekana kuna upendeleo.

Lakini je, kuna kikao kilikaa na kupanga upendeleo huu uwepo rasmi?

Au ni upendeleo ule wa kawaida tu wa kujuana unaojengeka bila kikao maalum?

Mtoa maada kasema kuna kikao maalum kilipanga, kuna maswali anakimbia kuyajibu.
 
Alikuwa mkuu wa wilaya huko Moshi akaacha ili agombee ubunge. Wajumbe wakamfanya kitu kibaya.
 
Alikuwa mkuu wa wilaya huko Moshi akaacha ili agombee ubunge. Wajumbe wakamfanya kitu kibaya.
Kaka Kippi alivyokatwa Kawe kuna kinamama walilalamika sana, nikajua kweli Kippi anapendwa na watu lakini CCM kama alivyosema Kaka Makongoro ina mambo ya ziada mengi sana.

Kaka Makongoro mwenyewe alikatwa akaenda kugombea NCCR Mageuzi kupata ubunge Arusha Mjini.
 
Baba yake anakosoa saana serekali
 
Watoto wa Nyerere, Warioba, Msuya, Dr Salim, Lowassa, Sumaye, Sokoine, Malecela na watoto wa Magufuli mwenyewe huu mkataba unawahusu au ni kakikundi furani pekee?
 
Mkataba wa mwitongo haupo.

Ukiniambia mkataba wa CCM wanamtandao, utaeleweka kirahisi.

Ni mkataba wa kuruhusu viongozi kufanya Biashara ndani ya uongozi na upendekeo wa Wala RUSHWA.

Ni mkataba wa waliovunja azimio la Arusha. Mkataba huo hauhusishi wazalendo wa Nchi kama Nyerere, Warioba, Mkapa, Magufuli nk nk.

Magu alijaribu kuuvunja na hakumaliza KAZI, Ajaye atamaliza KAZI Kwa ufasaha.

Tusubiri.
 
Siyo lazima viongozi wawe wanazaa viongozi.

Lakini, tukija kutafuta watu wenye usomi, hususannhuu wa kupima darasani, wenye kujuana na watu, wenye kuandaliwa vizuri kushika uongozi, hatutazunguka humo humo kwenye watoto wa viongozi na ndugu zao?
Kwenye usomi na watu walioandaliwa sio lazima kuzunguka humo humo kwa watoto wa viongozi na ndugu zao, Tanzania ina watu wengi wasomi wenye akili sana na wenye kukidhi vigezo vyote vya kuwa viongozi bora ambao sio watoto wa viongozi lakini wengi wao hawapati fursa hiyo ya uongozi au wanavurugwa njiani wanapoteana kabisa.
 
Kwa maana nyingins inayo eleweka kirahisi ni kwamba Ccm ni chama cha kifamilia zaidi.

Kama mzazi wako haja wahi kuwa kiongozi kwenye hii nchi, basi sahau teuzi. Hiyo ndiyo CCM. Na bado kuna watu wana iligia makofi

Mzazi wa Paul Makonda (DB) ni nani na amewahi hudumu katika nafasi ipi ya uongozi wa hii nchi na ndani ya CCM mpk useme kupata madaraka lazima mzazi wako awe ameshika hatamu ya uongozi wa juu? Orodha ni ndefu, ungana nao ule matawi ya juu!
 
Mkapa alikuwa na uzalendo gani? fuatilia uuzaji wa NBC hadi Baba wa Taifa akadinidha machozi, Mkapa muondoe hapo.
 
Sawa,

Naelewa.

Lakini uongozi si usomi tu pia. Kuna vetting.

Tatizo ni kwamba, tuna realities mbili.

Tuna reality ya kikatiba na kisheria, inayotaka haki sawa kwa wote.

Halafu tuna reality ya kiutamaduni. Hii haijali haki sawa kwa wote. Kwenye utamaduni unampendelea mtu wa familia yako, ndugu yako, jirani yako, mtu unayemjua siku nyingi kwanza.

Kisukuma hata kusalimiana tu mtu mkubwa anakuuliza "ng'wa nani?". Anataka kujua umetokea nyumba gani? Babu yako nani, bibi yako nani?

Utamaduni wetu umekaa kichifuchifu bado, kindugundugu, maisha ya kujuanajuana.

Lakini sheria zetu na katiba zinataka watu wote wawe na fursa sawa, bila kujali kujuana.

Na katika mgongano wa utamaduni na sheria, mara nyingi utamaduni unashinda na sheria inapindishwa.
 
Tunatakiwa tuachane na huu utamaduni wa kijima kwani unatuchelewesha sana katika uwajibikaji na maendeleo. Tamaduni nyingine zimepitwa na wakati na zina hasara nyingi kuliko faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…