Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wanao washaga taa moja hawana akili nzuri
 
Sasa wengine kutembea chini ya 140kph hatuwezi ndio maana nakwepa safari za usiku.
 
Yule ni mwamba,mbali na hiyo Aristo yenye 2gzte ana ile Chaser tourer nayo ni hatari,cha kushangaza kwa muonekano ni gari ya kawaida ila sokoni bei inagonga usd 20,000 bila cif
Jamaa yuko njema sana kwny hio mambo aisee,kuna tourer kule be forward inagonga mpk $37,000 mzee baba.

Kuna kipindi huyo jamaa alikua na Supra,Noma sana.
 
Huwezi kuwasha taa moja mkuu....ni kwamba moja imeungua and they just don't care!
Ni uzembe wa hali ya juu.. na hasa magari ya mikaa na mizigo na yanayo enda midani huko maporini ndio mala nyingi huwa nabahatika kukutana nayo.. na mengine huwa yanazima taaa
 
Nilishawahi drive Carina Ti 1500cc to 140km/hr gari ikawa inaanza kukosa stability,Swali nililojiuliza ni Je,itakuwaje kwa mtu anayeendesha Carina Ti 2200cc ambayo i think ni Turbo charged akaenda 180km/hr sijawah pata majibu.

Itakua uoga wako tu mkuu...m naendeshaga bits rs 180kph inakua kawaida tu mkuu
 
Kweli aisee,nna mpango na aristo siku za mbeleni huko nitaipiga modes za kizushi hata ikitoa HP 350 sio mbaya,haiwezekani gari ina kifua halafu inatoa HP 276 tu.
Tuzisake pesa tu,vitu vizuri vipo mkuu.. ukiwa na long term planning, unapata vitu vizuri sana.. mie miaka mitatu mbeleni najiona kwenye machine ya ulaya ya uhakika sio ya kichovu.. ila kwa sasa hivi acha nipambambane na mjepu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…