Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kuna siku nasafiri usiku, nikaona chombo mbele yangu kina taa moja, nikadhani ni pikipiki.

Hamadi mita kama 50 naona ni gari ina mzigo.

Niliyumba siku ile sitasahau, sio kwa kumkwepa vile.

Siku nyingine maeneo ya mwanga, chombo hakina taa nyuma.

Nagundua ni trekta limebeba mazao nimeshafika mita kama 50 hivi. Nikamkwepa nikavaa tuta.

Nimetokea kuchukia sana kusafiri usiku. Hasa hizi barabara zetu huchelewi kukuta kundi la ng'ombe au mbuzi barabarani na upo zako 170kph.

Ndo utajua hujui.
Wanao washaga taa moja hawana akili nzuri
 
Hii ya trekta isiyo na taa wala reflector nyuma nilikutana nayo mida ya saa moja usiku karibu na Nangurukuru, halafu upande wa pili naona taa za chuma inakuja. Siku ile nilikanyaga break nikaja kusimama kama mita 5 hivi kutoka kwenye trekta. Bahati nzuri nilikiwa just 100-120kph. Sipendi kabisa safari za usiku. Nasafiri usiku ikibidi tu na hapo speed mwisho 120.
Sasa wengine kutembea chini ya 140kph hatuwezi ndio maana nakwepa safari za usiku.
 
Yule ni mwamba,mbali na hiyo Aristo yenye 2gzte ana ile Chaser tourer nayo ni hatari,cha kushangaza kwa muonekano ni gari ya kawaida ila sokoni bei inagonga usd 20,000 bila cif
Jamaa yuko njema sana kwny hio mambo aisee,kuna tourer kule be forward inagonga mpk $37,000 mzee baba.

Kuna kipindi huyo jamaa alikua na Supra,Noma sana.
 
Huwezi kuwasha taa moja mkuu....ni kwamba moja imeungua and they just don't care!
Ni uzembe wa hali ya juu.. na hasa magari ya mikaa na mizigo na yanayo enda midani huko maporini ndio mala nyingi huwa nabahatika kukutana nayo.. na mengine huwa yanazima taaa
 
Nilishawahi drive Carina Ti 1500cc to 140km/hr gari ikawa inaanza kukosa stability,Swali nililojiuliza ni Je,itakuwaje kwa mtu anayeendesha Carina Ti 2200cc ambayo i think ni Turbo charged akaenda 180km/hr sijawah pata majibu.

Itakua uoga wako tu mkuu...m naendeshaga bits rs 180kph inakua kawaida tu mkuu
 
Kweli aisee,nna mpango na aristo siku za mbeleni huko nitaipiga modes za kizushi hata ikitoa HP 350 sio mbaya,haiwezekani gari ina kifua halafu inatoa HP 276 tu.
Tuzisake pesa tu,vitu vizuri vipo mkuu.. ukiwa na long term planning, unapata vitu vizuri sana.. mie miaka mitatu mbeleni najiona kwenye machine ya ulaya ya uhakika sio ya kichovu.. ila kwa sasa hivi acha nipambambane na mjepu tu
 
Back
Top Bottom