East Wind
JF-Expert Member
- Jun 17, 2020
- 2,783
- 6,058
Wanao washaga taa moja hawana akili nzuriKuna siku nasafiri usiku, nikaona chombo mbele yangu kina taa moja, nikadhani ni pikipiki.
Hamadi mita kama 50 naona ni gari ina mzigo.
Niliyumba siku ile sitasahau, sio kwa kumkwepa vile.
Siku nyingine maeneo ya mwanga, chombo hakina taa nyuma.
Nagundua ni trekta limebeba mazao nimeshafika mita kama 50 hivi. Nikamkwepa nikavaa tuta.
Nimetokea kuchukia sana kusafiri usiku. Hasa hizi barabara zetu huchelewi kukuta kundi la ng'ombe au mbuzi barabarani na upo zako 170kph.
Ndo utajua hujui.