Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mashimo ni mengi, juzi niliondoka dar 12 jioni nimeingia Arusha 03.00, barabara mbovu sana.
Kuna matuta hayana alama ya zebra, kuna sehemu za barabara lami imechubuka...yaani ni hatari hasa ukiwa na gari ya chini.
Mara kadhaa nilijibamiza kwenye matuta yasiyo na alama au mashimo...kilichonisaidia gari imeinuka.
Ni hatari kutembea usiku kuja kaskazini
Hiyo njia nimepiga shimo mpaka roho ikaniuma.
 
Mambo view eco lodge.
Not super fancy but very traditional. Angalia Google map, call for reservations and ask for a discount. Kuna rooms with the view of the valley.

Wahudumu wanaweza kukutafutia kuku wa kienyeji wakakutengenezea.
Okay thanks...last time nilikaa Mullers mountain lodge...it was an amazing experience!
 
Oh mashimo yameongezeka? Na usiku kuona mbali ni issue. Mara ya mwisho nilisafiri jioni nikapata msala saa 12 ndio ilikuwa pona yangu vinginevyo ningelala barabarani hadi asubuhi. Sisafiri tena usiku.
Napenda sana safari za usiku. 90% ya safari zangu huwa ni usiku. Na ninakiwasha haswaaa...
 
Safari ya usiku inachosha na kuboa sana.

October tulienda Moshi.

Kuna wakati mpaka nikatamani nipaki nilale sema tulikuwa gari mbili tunaongozana.

Tulitoka Dar saa 9 mchana. Tunafika Bagamoyo saa 11. Foleni yake si mchezo. Moshi tuliingia saa 5 usiku. Ila niliionea huruma gari.

Barabara ni mbovu sana hasa kipande cha Segera Msata.
Safari ya usiku haijawahi kuniboa

Yaani na enjoy haswaa
 
Back
Top Bottom