Wazee wa β€˜Road Trip’ mpo?

Wazee wa β€˜Road Trip’ mpo?

Kuna siku mida ya saa 9 nlilipaki nyuma ya tanker la mafuta pale Kibaigwa nikajilaza nipunguze usingizi.

Ndoto ikaja niko kibati halafu kuna kuna kicheche cha tanker la mafuta naenda kukivagaa. Kukurupuka usingizini na kufungua macho naona lori lilelile nililoliota liko mbele yangu sasa live. Panic yake mzee, mpaka kuja kugundua nilikuwa naota nimeshateseka sana.

Nikalaza vizuri kiti nikaendelea kulala. [emoji23]
Ka vitu ambavyo nimeshindwa, ni kupaki gari sehemu nilale.. hili hata niwe tight vipi huwa natobo lengo kuu huwa nipate sehemu nzuri sana ya kulala.. ili nikiuchapa usingizi nauchapa kwelii πŸ˜€
 
Mwanza napo si mchezo. Kwa afya inabidi safari igawanywe mara mbili
Mwanza 😳😳😳... Natoka dar alfajiri saa 2 usiku nipo mwanza ... tena huwa napitilizia kula bata kama sio the cask basi uswazi diamond (napenda yale masato yao na palivyo changamka, nakaa napiga na maji hata lita tatu maana wengine alcohol hatuijui) au bonasera ... narudi hotelin asubuhi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.. japo sio mala zote huwa nafanya hivi.. hutokea siku nikiwa nimechangamka
 
Mzee Kikwete zamani sana (early to mid 90's) alikuwa na mashine kama hii, sijui kama angali anayo...

Miraj, Sele Kikwete wazee mlitutesa sana kitaa cha Migombani...



Sent using Jamii Forums mobile app

This weekend (Jumamosi), ipige sop sop ile Nissan niliyocrush nayo toka Maktaba signals to Mbuyuni.... Ntakusubiria Mediteranian....

Nna jambo nalo Nissan, my crush car πŸ₯°.

Halafu uache kutoa siri za familia ntakusemea kwa shemeji ...🀣🀣🀣🀣

Mambo sukari, nimwkumithiii....😜😜
 
Nimepitia uzi mzima,hakuna aliyepiga trip ya Mbeya,,
Halafu sijaona aliyeanzia trip Yake Mbeya,,ina maana Mbeya wote hatuna magari mwee[emoji38].

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa tunakuja mama...

Na raha ya MB ukiwa warudi jiji la Makamba lazima uzame Kiwira pale kwenda kuchukua mikungu kadhaa ya 'matoke', mtindi kwa wale wamama Kiwira town, then wasogea Kabwe kubeba mchele, Uyole kuchukua parachichi...

Raha ya MB ni misosi, kuna raia wanaweka nyama za mafungu pale Nanenae, kama ni mroho wa nyama utakula hadi ukinai, au kuna chocho fulani Soweto/Mama John pale, kuna raia wana kaanga mdudu hatari...

Uyole.jpg
 
This weekend (Jumamosi), ipige sop sop ile Nissan niliyocrush nayo toka Maktaba signals to Mbuyuni.... Ntakusubiria Mediteranian....

Nna jambo nalo Nissan, my crush car [emoji3059].

Halafu uache kutoa siri za familia ntakusemea kwa shemeji ...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mambo sukari, nimwkumithiii....[emoji12][emoji12]

Hahah...

Kasinde sasa hivi nipo kama wewe tu mama, naburuta makalio chini (gari za chini)...

Hivi kuna siku nishaacha kumiss Kasinde kweli...yo always missed 'mlamba sukari Kasinde' [emoji3059]
 
Yeah Mbeya parefu. Ila nahisi umbali wake hauoni ndani kwa umbali wa kwenda Mwanza.
Kwa mujibu wa Tanroad
Dar - Mby 822km
Dar - Mwz 1152km

Hivyo utofauti ni kama 330km (approx umbali wa Dar - Muheza)

Ukitaka ufaidi safari ya Dar-Mby tembea usiku, ukiwa na gari nzuri ni safari ya masaa 7 hivi hadi 8, ila kama si mzoefu tembea mchana utumie masaa 13 au zaidi
 
Wazee wa Trip nimetamani safari ndefu ya Bus hata nje ya nchi
Naombeni ideas za safari ndefu. Zaidi kwa Njia ya bus Kutokea Dar- popote[emoji28]
You can plan for Dar - Mombasa (via Tanga), utaweza iona Tanga yote utamiss tu kupita wilaya ya Lushoto, Korogwe...

Au pia unaweza safiri kwenda Kampala, Uganda na vile wewe ni mtu wa mishemishe unaweza pata chimbo la kibiashara huko (huwa naona raia wanaenda UG kuexplore machimbo, dunno what's good out there)...

Au kama wataka safiri ndani ya Tanzania, Dar-Kigoma or Dar-Musoma or Dar-Bukoba zaweza kuwa safari nyingine ndefu...
 
Back
Top Bottom