Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

[emoji38][emoji38][emoji38]

Siku hizi wana gari nyingi sana,,route ziko specific na Kila eneo na route yake .
Kipindi cha mvua walikuwaga wanabadilisha labda siku hizi. Yaani gari nyingi walikuwa wanawapa abiria wa Kimara na Mbezi maana hao foleni zao ndiyo zilikuwa zinajaza vituo.

Wale wa Kivukoni na Morocco watasubirishwa hapo maana wanakuwa wachache hivyo wanadhani hawana haraka, gari zao zinabadilishiwa route wanapewa hao abiria kama utitiri.
 
Mna tabia mbaya [emoji1787][emoji1787]
Aahh tulikuwa tushajichokea zetu vichwa vinawaka moto balaa, tumehangaika kupigana tumekula vipepsi vya tumbo bahati mbaya ndiyo siti tulizoambulia halafu umpishe mtu kizembe tu daah inauma hata kama ni haki yake.

Tatizo bongo tumekariri kwamba ni hayo makundi tu ndiyo hayatakiwi kusimama kwenye usafiri, lakini wanasahau kwamba mtu anaweza kuwa kijana ana afya lakini siku hiyo tu akawa anaumwa kiasi hawezi kusimama muda mrefu.
 
Kipindi cha mvua walikuwaga wanabadilisha labda siku hizi. Yaani gari nyingi walikuwa wanawapa abiria wa Kimara na Mbezi maana hao foleni zao ndiyo zilikuwa zinajaza vituo.

Wale wa Kivukoni na Morocco watasubirishwa hapo maana wanakuwa wachache hivyo wanadhani hawana haraka, gari zao zinabadilishiwa route wanapewa hao abiria kama utitiri.
Hao ni halali yao kusubiri.

Watu unakuta wapo wanne tu mwendokasi lote,halafu Mbezi kuna mafuriko ya abiria na gari ishajaa.
 
Mimi mwenyewe nishawahi fanya hivyo siku hiyo kwenye kugombea siti si nikavamia za wamama wajawazito, tulikuwa wawili halafu wote mabinti wenye afya zetu tu.

Wenye siti zao wakaingia wakaanza kutuangalia kutaka tuwapishe si tukajifanya kama hatuelewi, yule mwenzangu ndiyo kabisa akainamia begi lake akalala wakaanza kutusema.
Mimi mwenyewe siku nikiamua kukaa,hata aje nani sisimami.

Siku Nikiwa na mood ya kupisha nitapisha hata kama siyo zile siti zao .

Juzi kati nilikuwa najisikia hovyo,zile siti tulikaa vijana wote,tena mwingine wa kiume kabisa,
Wakapanda wamama Fulani watu wazima yaani nilikauka hata sikusimama.
Hafu Wana kamtindo,wakipanda wanawaangalia usoni[emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi na miwani Yangu na barakoa aisee namimi namuangalia tu.
Ila nilikuwa naumwa.
Nikigeuka pambeni naona yule kaka ameinamia simu [emoji38],naangalia pembeni naona mdada anajidai kusinzia[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Yaani asubuhi ninaweza simama nikampisha Mtu..
Ila jioni wallah sisimami,yaani usimame hadi Mbezi!
Hapana Kwa kweli.
Mtu mwingine palepale gerezani /Mbezi anaona gari imejaa anapanda akitegemea vijana watampisha.

Mimi nikishikwa na huruma sana nitampisha Mtu aliyepanda njiani vituo ambapo gari halianzii na Haiwezekani kupata siti..nje na hapo adabu inipite tu pembeni.
 
Back
Top Bottom