Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ili kumpunguzia safari ya kupanda milima kuja hapo Singapore itapendeza wewe mwenyeji ushuke fasta uumpeleke pale bambalaga na viwanja vingine mgeni afurahie
Hili nalo ni neno , natoka singida saa moja saa tatu na nusu nipo bambalaga tunaanza na supu nzito kabisaa.. jumamosi naona panawaka sana pale , shida hawawezi zile za kibabe asubuhi pale wanabaki sana wachezaji wa akiba, wachezaji wote wa maana wanakata pumzi mapema

Offshore Seamen
 
Kwahio unanishauri nisibebe mbuzi, nibebe chumvi pilipili na kisu tu?!
 
Holy Man ISO M.CodD wiki ya kwanza mwezi ujao nina trip ya Dodoma. Sijawahi kupita njia ya Kati zaidi ya Morogoro. Nipeni dondoo njia ikoje hasa kwa gari zetu zinazotembelea tumbo!
Ukiwa unaimaliza gairo kuuanza mkoa wa dodoma, kuna kimuiniko kimoja kireeefu..

Sasa juzi alhamisi wameweka vituta vyembamba lakini vikali sana. Gari za chini lazima zikwangue labda wawe wamerekebisha.

Kwa kifupi huo mpando wameuharibu kabisa! Ikitokea malori yamekutangulia hapo ni balaa
 
Huwa nabaki na maswali mengi sana kuhusu mainjinia wetu.
 
Sio Ranchi ya Kongwa kweli hapo?
 
Haha nchi ngumu hii bwashee bila mamlaka Utapata taabu sana
 
Singapore hapo ni hatari sana, unaweza ukatafuta breakdown ili ubaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…