Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Next week nina trip kutokea Dar es Salaam, hadi Tabora ( kituo - siku moja). Tabora hadi Mwanza ( kituo siku hazijulikani), baada ya hapo tunarudi Dar es Salaam.. Aina ya gari Toyota Alphard
Travel safely mkuu, never allow Driver wakati unaendesha uwe passenger, lazima uwe in control, good and safe distance following ni muhimu mno, always endesha nyuma ya heavy trunks ili yakusafishie njia na kukupa slope kidogo na hii inasaidia kuokoa wese
 
Sijaelewa, aendeshe nyuma ya heavy trunks? Au heavy trucks? Si atafika keshokutwa?
 
Kufata mtu nyuma hatari sana, na moja ya kitu ambacho siwezi kuendesha huku nipo nyuma nyuma ya mtu
 
Sijaelewa, aendeshe nyuma ya heavy trunks? Au heavy trucks? Si atafika keshokutwa?
Sorry trucks, faida ni to clear the way, usifanye tailgating hii ni hatari, ni nzuri kwa safari za usiku,binafsi always T1,kutoka Mbeya to Dar ninakua nyuma ya tanker, na pia beam light zako ziwe kawaida, safari inakufanya uwe macho na makini
 
My number one rule sikai karibu na lorry. Nikilifikia nalipia nafasi inapotokea na kuliacha. Ukikaa nyuma ya truck hata mbele huoni na kawaida ukiendesha unatakiwa uone zaidi ya gari lililo mbele yako.
 
Unasema kweli kabisa mkuu, ni
Kuna ajali ilitokea huku kisarawe Costa ya abiria kisarawe-machinga complex kale kasiti kadogo alikaaa mama mmoja kushoto jamaa kulia kama kawaida dereva.

Gari ikafeli breki mlimani wakati wanashuka waliogundua alikuwa huyo mama na dereva na jamaa wa kushoto mbelee..
Yule mama akapaniki akaanza kupiga kelele na kutaka ashike steering sababu ilikuwa mlimani alafu kuna Kona kalii.....
Kelele zake zikafanya abiria wa nyuma wajue gari imeshafeli mabreki abiria wengine wakapaniki nao bahati mbaya Ile gari.
Dereva alishindwa kui-controll sababu yule mama aliiing'ang'ania na huwezi amini gari Zima alikufa huyo mama TU mara nyingi wanaume Huwaga kimya ata utembee vipi ila wanagugumia ndani Kwa ndani nna shuhuda za ajali nyingi chanzo ni kelele na kupanic kwenu.
Nilishawahi endesha rav4 kili time tokea moshi mbaka dar breki ilikua ya kupump unaipatia chini kabisa ndio inakubali. Nilikua na wamama wawili ndani, alafu njiani kuanzia mombo mbaka karibia na bagamoyo ilikua inatandika mvua ya maana. Kuna mida ilibidi tuwe tunasimama maana hata mbele kuona ilikua shida. Mwenyezi mungu ni mwema tulifika salama ile safari. Tulitoka moshi town kama sa1 asbh na town tukaingia sa12 jioni. Najua ningewaambia breki hazikopoa, ile safari isingewezekana. Mimi kimoyo moyo nilikua nahofia wami lakini tulipita bila shida yoyote.
 
Wadada tumekukosea nini jamani.
Wanaume ndio wanaoongoza kwa kutoa maelekezo kwa dereva.
Ila hii inategemea, last month natokea moro narudi mjini nilirudi na mdada mmoja tena nilikaa nae mbele kabisa. Akaanza ohoo tuwahi sijui harusi sijui ana dina date maneno kibao. Namimi ndo vile sipendi kukwaza mtu nikawa namsikiliza. Hapa chalinze kuja vigwaza(katikati nimesahau) lakini miaka ya 2016-2018 gari za dar moro zilikua zinasimama kuchimba dawa kwenye kahoteli flani hivi, nikaovertake mara trafik huyu hapa na kweli niliingia mstari ulikua hauruhusu sema niliona mbali gari hakuna ndomana nikafanya hayo maamuzi. Chapu jamaa kaniweka pembeni namimi sipendagi kelele mingi nikatoka nishaandaa changu chini ya leseni. Jamaa akanambia unajipangia adhabu eeeh😂😂😂nikasema samahani poti.....then nduki mbaka mjini. Lakini bila yule dada na kelele zake mara v8 zinatupita sijui nini yani maneno kibao, ila naamini bila yeye hata jamaa asingekula pesa yangu siku ile.
 
Unasema kweli kabisa mkuu, ni

Nilishawahi endesha rav4 kili time tokea moshi mbaka dar breki ilikua ya kupump unaipatia chini kabisa ndio inakubali. Nilikua na wamama wawili ndani, alafu njiani kuanzia mombo mbaka karibia na bagamoyo ilikua inatandika mvua ya maana. Kuna mida ilibidi tuwe tunasimama maana hata mbele kuona ilikua shida. Mwenyezi mungu ni mwema tulifika salama ile safari. Tulitoka moshi town kama sa1 asbh na town tukaingia sa12 jioni. Najua ningewaambia breki hazikopoa, ile safari isingewezekana. Mimi kimoyo moyo nilikua nahofia wami lakini tulipita bila shida yoyote.
😅😅😅 Aisee.. Nilishatembea na gari haina brake kutokea Dodoma hadi Mwanza.. baada ya kumaliza safari nikajitafakari sana, ila nilimshukuru Mungu.
 
Unasema kweli kabisa mkuu, ni

Nilishawahi endesha rav4 kili time tokea moshi mbaka dar breki ilikua ya kupump unaipatia chini kabisa ndio inakubali. Nilikua na wamama wawili ndani, alafu njiani kuanzia mombo mbaka karibia na bagamoyo ilikua inatandika mvua ya maana. Kuna mida ilibidi tuwe tunasimama maana hata mbele kuona ilikua shida. Mwenyezi mungu ni mwema tulifika salama ile safari. Tulitoka moshi town kama sa1 asbh na town tukaingia sa12 jioni. Najua ningewaambia breki hazikopoa, ile safari isingewezekana. Mimi kimoyo moyo nilikua nahofia wami lakini tulipita bila shida yoyote.
Sasa sijui hii tuiteje ili usikwazike, unaingia highway 500km bila brake za uhakika?!!!
 
Back
Top Bottom