Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Traffic nchi nzima wanasimamia sana overtaking mahali ambapo mstari hauruhusu, hata kama ni salama.

Wapiga picha wanakaa haswa kwenye milima, wanajua malori yatakuwa slow nawe utataka kuyapita kwenye mstari ulionyooka. Ukifanya hivyo utakuta picha na cheti chako mbele.
Duh washaninasa sehemu kama hii....jamaa wanajua wapi uvumilivu unatushinda.
 
Mashimo ni mengi, juzi niliondoka dar 12 jioni nimeingia Arusha 03.00, barabara mbovu sana.
Kuna matuta hayana alama ya zebra, kuna sehemu za barabara lami imechubuka...yaani ni hatari hasa ukiwa na gari ya chini.
Mara kadhaa nilijibamiza kwenye matuta yasiyo na alama au mashimo...kilichonisaidia gari imeinuka.
Ni hatari kutembea usiku kuja kaskazini
Aisee asante kwa taarifa hii, niliona kipande cha same-himo kina changamoto hizi. Kwingine wapi?
 
Ohooo
Haya bwana mkubwa ..tukapigapo na ka honi kumbe sio ww😂😂😂

Ila kama ingekua ni ww ningekua nshakufahamu fika maana jamaa alikua na pisi kali anaongea nayo mwendo wa taratiibu ....anachelewesha watu wa nyuma kila mtu alikua akiovateki anamuangalia kwanza na alikua ameshusha kioo
Ha ha ha ha DVA watapata tabu sana....honi kama zote! Vanguard nyeusi?!!
 
Msitunyime kapicha hata ka Tecno msafara wenu hiyo tarehe
Kuna Msukuma Kadogosa kasema atatuma Treni kila siku tarehe hizo ibebe zaidi ya abiria 2000 na baada ya mwaka mpya vivyo hivyo
najua bado tutawaona barabarani Chalinze Segera Himo
Kuanzia kesho misafara inaanza
 
I love long drives!
Ukiwa njiani kurudi, pandisha Lushoto. 60 Kms kutoka Lushoto town kuna kijiji kinaitwa Mambo. Hali ya hewa ni njema Sana, highest point na unaona pare and sambaa land around you. Network ya simu ni ya shida na hakuna TV. Ukikaa siku 2 tu utarudisha nyuma umri wako kwa miaka 10.

Enjoy your trip mazee
 
Malori yamekuwa kitega uchumi cha traffic katika hili kwakweli. Wanapiga picha where you least expect it. Na as a matter of fact katika sheria ngumu kucomply nazo ni hii ya mistari ya kukatiza.

Overtake lorries with care mkuu au andaa budget ya vyeti kadhaa. Problem is wakikusimamisha wanakuchelewesha so you are better off just being patient kuongozana na lorry for 2 - 5 minutes mpaka mistari iruhusu ulipite.
Fine_2_01-Copy.jpg


RRONDO
 
I love long drives!
Ukiwa njiani kurudi, pandisha Lushoto. 60 Kms kutoka Lushoto town kuna kijiji kinaitwa Mambo. Hali ya hewa ni njema Sana, highest point na unaona pare and sambaa land around you. Network ya simu ni ya shida na hakuna TV. Ukikaa siku 2 tu utarudisha nyuma umri wako kwa miaka 10.

Enjoy your trip mazee
Lodge gani nzuri....iko kwenye ratiba
 
Hasa barabara ya kaskazini imeharibika sana, wazee wa kupenda kutembea usiku inauniza sana.
Safari ya usiku inachosha na kuboa sana.

October tulienda Moshi.

Kuna wakati mpaka nikatamani nipaki nilale sema tulikuwa gari mbili tunaongozana.

Tulitoka Dar saa 9 mchana. Tunafika Bagamoyo saa 11. Foleni yake si mchezo. Moshi tuliingia saa 5 usiku. Ila niliionea huruma gari.

Barabara ni mbovu sana hasa kipande cha Segera Msata.
 
Back
Top Bottom