Kuna jamaa niliandika hapa akanibishia sana lakin ukweli utabaki kwamba hz gari ni very risk sana kwa vijana.Kwenye nchi za wenzetu insurance Co. huwa zinachaji premium kubwa kwa kuzingatia umri wa dereva,ukubwa wa engine ya gari nk. Kwa mazingira yetu ya Tanzania ni kwamba Crown,Mark X na Brevis zinapendwa sana na vijana na ndizo zinazoongoza kwa mizinga mibaya sana.Nilishaenda kufanya service Spring City garage ilikuwa jumatatu fulani,hz gari zilikuwa zipo za kutosha tu sababu ya mizinga na hopeful lazima ni vijana kwenye mambo ya weekend, na nyingi zilikuwa mpya kabisa.