Kabla ya hii trip nimesolve taa zote za dashboard.
Check engine ilikuwa kwasababu ya post-cat heated oxygen sensor. Gari ilivyokuwa chini inaonekana ilipiga ardhi pale connector harness ya sensor pakapasuka na waya kukatwa. New sensor nikaclear code kwa kale ka mashine kangu ka $10 check engine haijarudi tena
Fuga zina ujinga mmoja kukiwa na weakness yoyote kwenye braking system ina disable traction control, wanaita VDC (Vehicle Dynamic Control) na kuwasha taa za VDC OFF na SLIP. Ikiwa kwenye hii situation ukikanyaga hovyo linadrift na kuteleza, though its fun [emoji23][emoji23]. Nilicheki pads ziko fresh, kumbe mafuta ya breki yalikuwa nusu - hata sio low. Kujazia mpaka kwenye max taa zikazima after some driving.
Gari ikiwa na clean dashboard inaleta imani kidogo, sio christmas lights kama za wajerumani Cc
Extrovert