Mmh uwezo wa kufanya mambo gani
Mimi kwangu utajiri ni kuwa na pesa za kukimu yale mahitaji yote muhimu ya binadamu na bado zikabaki nyingine za kutosha kufanya maendeleo na kuweka akiba (na hii ndiyo tafsiri ya kawaida ya kiuchumi tukiachana na hizi ngonjera za utajiri wa moyo sijui nafsi)
In short kwangu mimi tajiri ni yule mtu ambaye pesa zake siyo za mawazo
Sasa wewe mwenzetu unachotaka kutuaminisha hapa ni kwamba hata mtu akipata nauli tu ya kuweza kumfikisha Mbeya au Moshi na kurudi akasema na yeye asafiri aoshe macho kidogo basi tayari ni tajiri
Wakati unaweza kukuta amesacrifice vitu kibao hapo ambavyo ni vya muhimu ili tu kujichanga hadi kufikisha hiyo hela kusudi tu na yeye asafiri sababu kusafiri ni hobby yake
Mimi kwangu huyo siyo tajiri maana hela zake ni za mawazo na hata mimi kama nina hela za mawazo kama hizo siwezi kujihesabia kuwa ni tajiri na hata mtu akisema mimi ni tajiri nitakuwa naona kama ananitukana tu
Kwahiyo siyo kila anayesafiri ni tajiri