Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Wazee wa Tanga kusoma albadir kwa waliomuua Mzee Ali Mohamed Kibao

Hilo ni wazo zuri ila ninachojua watahongwa isisomwe ,pia wazee wanaweza kushitaki kwa mizimu yao itajibu tu.
Watahonga wangapi, hapa Kwa msisi Handeni wazee wanafanya ya kimila zinahitaji ndoo sita za mate hadi Jumamosi , hili nyugu siyo la kitoto, na Pangani nako wamejipanga kivyao lazima kieleweke tu, huko Mbaramo Lushoto nako wazee wameshamaliza tangu jana wanasikilizia matokeo tu.
 
Hio dua lazma kwanza msomaji awe msafi kwelikweli, na iliwezekana sana enzi hizo kwa sasa labda waroge ila kukuta mtu msafi wa kukusomea albadili ikafanya kazi kwa sasa ngumu
Yaani mtu msafi kwelikweli amuombee mtu ili mabaya yamkute?
Usafi sasa wa mtu huyo u wapi sasa?

Who can bring a clean thing out of an unclean?
 
Albadiri sio Dua , bali ni uchawi wa kiarabu. Ndio maana siku zote inasomwa kuleta madhara tu na sio manufaa. Huwezi sikia mgonjwa akasomewa albadiri ili spine au mwanafunzi akasomewa albadiri ili afaulu mitihani. Albadiri ni uchawi.
Mbona kama unajitetea sana subiri mpindishwe midomo baadhi yenu mgeuke vichaa na wengine WAFE kama alivyo kufa huyo kada wa chama
 
Hakuna cha albadiri wala albajoto mimi ni muislamu na nimechukizwa sana na hichi kitendo ila kusema ukweli izo dua za albadiri sijui albajoto hamna lolote zaidi ya watu kufanya ushirikina tu

Muislamu wa kweli anoijua vizuri dini yake hafanyi huo upuuzi
Waislam Wachache sn wanaweza kuusem huu ukweli
Big up
 
Hakuna cha albadiri wala albajoto mimi ni muislamu na nimechukizwa sana na hichi kitendo ila kusema ukweli izo dua za albadiri sijui albajoto hamna lolote zaidi ya watu kufanya ushirikina tu

Muislamu wa kweli anoijua vizuri dini yake hafanyi huo upuuzi
Athari zimeanza kujiri mapema kabla hawajapiga kisomo.

Mkuu jishikilie hapo ulipo isije ikaondoka na wewe
 
Hakuna cha albadiri wala albajoto mimi ni muislamu na nimechukizwa sana na hichi kitendo ila kusema ukweli izo dua za albadiri sijui albajoto hamna lolote zaidi ya watu kufanya ushirikina tu

Muislamu wa kweli anoijua vizuri dini yake hafanyi huo upuuzi
Mkuu,
Mimi sio mwislamu lakini Kuna nyakati unaruhusu Kila silaha iliyopo mbele Yako kutumika kama itasaidia.

Watu wamepiga kelele kuhusu watekaji wao wamekaa kimya maana tunaotekea ni sisi.

Hivyo kama albadir ni ibada, ushirikina, shirki, uchawi vyovyote utakavyiita na utaenda kuwapata wahusika na iwe hivyo.

Tunapopatwa na jangwa Huwa tunawaambia watu wasali kwa Iman zao. Sasa kama wameona walifanya albadir kisasi kitalipwa na iwe hivyo.

Kule Meru wanavunja chungu kama sehemu ya kulipa kisasi na iwe hivyo.

Ikitokea wachawi wa Gamboshi wakasema watafanya ibada yao waliohusika wadhurike na iwe hivyo.

Yaani mpaka wahusika Waite maji mmmma.

Hii ndio inaitwa okoa maisha Yako kwa gharama yeyote ile. Hivyo tuepuke kutekwa kwa gharama yeyote ile
 
Kutoka Tanga inaripotiwa kuwa wazee wa Tanga wamepanga kusoma dua ya kushitakia almaarufu kama albadil kwa walioshiriki kumuua mzee mwenzao Alli Mohamed Kibao.

Watakaosomewa duwa hiyo ni wale waliopanga njama za maauaji,walioshiriki kumteka,waliomuua,waliofahamu mpango mzima wa mauaji hayo,nk

Kwenye suala la duwa ukiondoa wazee wa Pemba basi wanafuata wazee wa Tanga
waanze na peter msigwa
 
Kama kuna mchango nami nita toa.
Lakini hawa majambazi uta sikia ni marufuku kusanyiko la aina yoyote.
Kumbuka wakati wa Lissu watu wali panga kwenda kanisani kumuombea, wahuni waka piga marufuku hata kuvaa fulana yenye picha ya Lissu.
 
Hiki kisomo kinafanya kazi asilimia 100 wakuu nimeshuhudia live na mimi nilikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kwenye dua hiyo.

Aise tulishuhudia watu wanapukutika vibaya sana tena kabla ya vifo vyao walikuwa wanakiri kufanya uhalifu huo na kufanya vituko vya ajabu.

Wale wale waliokuwa wanahisiwa ndiyo waliopukutika mmoja baada ya mwingine.

Ikishasomwa hii dua huwa haina ku reverse ni mwendo wa kutafuna tu kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom