Waziri Abdallah Ulega: Madai ya Samaki kuhifadhiwa kwa maji ya maiti ni hisia tu

Waziri Abdallah Ulega: Madai ya Samaki kuhifadhiwa kwa maji ya maiti ni hisia tu

Afanye utafiti huru asiseme ati hakuna kitu kama jicho wakati sisi ndio wauzaji wa hizo dawa na sisi ndio wavuvi na wahifadhi samaki

Atusikilize tumwambie ukweli tupone
Hah Mama D kumbe wewe Ndo muuzaji!!!!
 
Anaogopa soko la Samaki la Tanzania kuporomoka kwenye soko la Dunia.
 
Kwamba mtu mwenye ELIMU kiwango Cha Doctorate, tena kiongozi mkubwa wa pili baada ya Rais anaweza simama jukwaani na kuongea Kwa "HISIA"

Siamini ktk Hilo.

Naamini " Uchumi wa Kanda ya ziwa kwa S.Gang unahujumiwa".

Yana mwisho hayo lakini.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Haya ndio maswali tunayopaswa kujiuliza kwa sasa , kwamba Je kuna ukweli wa haya nambo au ndio tusubiri kanusho la Kuku au tusubiri kuambiwa Ng'ombe nao wanamekula majani yenye sumu ?

Je Kuna njama za kuwafanya Watanzania wote Vegetarians ?
 
Maisha ya mijini ni tofauti na maisha ya vijijini.

It is easy to tell why urban people have short life expectancy than rural people regarding eating healthy food.
 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Hamis Ulega amesema suala la maji ya kuoshea maiti kudaiwa kutumika kuhifadhia Samaki halina uhakika na kwamba ni hisia tu.

Akijibu swali Bungeni kuhusu taarifa hizo ambapo inadaiwa matumizi ya maji hayo yanasababisha Saratani kwa walaji, amesema “Siyo kweli na ndio maana Makamu wa Rais (Phillip Mpango) ameagiza Wizara ya Afya ifanyie utafiti ili kama kuna kitu cha aina hiyo kizuiwe mara moja.

“Niwatoe hofu Watanzania, wapo salama na hakuna shaka yoyote juu ya taarifa hizo.”

Huyu Waziri naye ana upungufu mkubwa. Atawezaje kusema kuwa watanzania wapo salama wakati tunaambiwa kuwa 60% ya wagonjwa wote wa saratani wanatoka kanda ya Ziwa?

Yawezekana maji ya kuoshea maiti siyo chanzo cha hali hiyo, lakini kusema wakazi wa kanda ya ziwa wapo salama, ni uwongo. Linatakiwa lipatikane jibu, kwa nini wagonjwa wa saratani ni wengi sana kanda ya Ziwa kuliko maeneo mengine yote ya Tanzania?

Kwa sasa kila mwanachi achukue tahadhari kwa kuzingatia all hypotheses:

1) uhifadhi wa samaki kwa kutumia chemicals hatari (ulaji samaki wa ziwa Victoria ni hatari)

2) mercury poisoning (maji na vyakula vinavyopatikana maeneo ya machimbo ya wachimbaji madini wadogo ni hatari)

3) heavy metal contamination (maji na vyakula kutoka maeneo yaliyopo mazingira ya uchimbaji madini ni hatari)

4) madawa yanayotumika kwenye kilimo.cha pamba (ardhi inayotumika kwenye kilimo cha pamba ni hatari inapotumika katika kilimo cha mazao ya chakula).

5) utiririshaji wa maji ya sumu ndani ya ziwa kutoka viwandani (maji ya Ziwa Victoria ni hatari)

Chukua tahadhari mpaka sababu ya uhakika itakapopatikana. Utafiti wa jambo hili unaweza kuchukua miaka kadhaa mpaka kupata jibu la uhakika.
 
Back
Top Bottom