Waziri anayemiliki jumba la kifahari ufukweni Dubai atajwa

Nani au taasisi ipi labda unapendekeza imchunguze huyo waziri?

Fikiria ripoti za CAG zinazowekwa wazi, madudu yake huwa hayachunguzwi kivile, sasa nani atamchunguza mtu aliyefanya usiri kumiliki mjengo UAE...
Nafikiri ni kati ya walio wizara ya manoti
 
Mkuu unaonekana na wewe ni mmoja wapo wa majizi haya yaliyopo serikalini.

Waziri unapataje 300billion kwa miaka hata 30 kwa kutegemea mshahara wako halali?

Wacha kudanganya watu ndugu yetu maana watanzania wa leo siyo wale wa zana za mawe.
 
SIO AJABU! Tattizo hana biashara wala chanzo chochote cha uwezo wa kumiliki mali hizo. MAANA YAKE NI MWIZI
Huu ni ukweli mchungu.

Bahati mbaya watanzania wengi hawajui hilo na viongozi wezi wanatumia huo mwanya kuiba bila hofu yoyote.
Wananchi wasiojua wanawaita hao wezi majina ya kuwatukuza/pongeza kama WAJANJA, WATOTO WA MJINI na mengine ya kuwasifu kwa huo wizi wanaofanya.
 
Kati ya hao watano kuna mawaziri wangapi?
Sioni Waziri kwa kweli. Mimi Nasubiri waliotayari kutupa mikakati Yao ya kupata fedha za kununua majumba zaidi ya hayo huko ughaibuni kama fashion mpya baada ya fasheni ya uchawa kukosa nguvu.

Vinginevyo, siwezi kujiletea sonona kwa upuuzi huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…