Waziri Bashe amjibu Tundu Lissu kuhusu Wabunge kufanya biashara ya pamba, amwambia 'Mbona Mwenyekiti wake alikuwa Mfanyabiashara na Mbunge'

Waziri Bashe amjibu Tundu Lissu kuhusu Wabunge kufanya biashara ya pamba, amwambia 'Mbona Mwenyekiti wake alikuwa Mfanyabiashara na Mbunge'

Upumbavu wa hii inchi upo kwenye mambo yafuatayo.
1. Kutokuwa/kutofuata maadili.
2. Kutokuwa na hofu ya Mungu.
3. Kutokutii sheria,kanuni,miongozo na taratibu.
4. Katiba kutokufuatwa.

Kuanzia juu (Rais) ambaye ndiye mtendaji mkuu wa inchi anayepaswa kufuata katiba kama "msahafu" wa Taifa, anakengeuka, huku chini ni nani atakayekuwa tayari kufuata sheria, kanuni na taratibu tulizojiwekea!!??

Tumesikia na kuona kwa masikio na macho yetu ya nyama kuwa Mh. Rais anasema kwamba anaona aibu kumchukulia hatua mtu aliyemzidi umri, hapo kweli tunategemeaje hawa wa chini waweze kuchukua hatua kwa wanaofanya makosa!!!??

Tumesikia na kuona Mh. Rais akitamka kuwa ni ruksa watu wale kwa urefu wa kamba zao, sasa hapo unategemea yule Afisa Mtendaji wa Kijiji asichukue rushwa kwa mwanakijiji anayehitaji kugongewa muhuri tuu!!??

Tuna tume ya maadili ambayo mpaka kesho hakuna anayejua inalisaidiaje taifa katika kuhakikisha tunakuwa na viongozi wasio na makando kando ya "kimaslahi"!!

Utatuzi ni tuanze upya kwa kuandila katiba mpya ambayo kila mwananchi awe kiongozi au raia wa kawaida itamtia hofu ya kufanya tofauti na katiba inavyosema.
 
Wabunge na Mawaziri wa CCM waache exploitation sisi sote ni Watanzania.
 
Conflict of interest apo inatokea mimi daktari leo Nikiwa na Pharmacy nje ya hospital ni sawa?
 
watanzania bhana kila siku Nchi nchi nchi nchi hivi nyie hamwezi kuishi maisha yenu na kuacha maisha ya nchi yaendeleee , hiv kama ww una akili timamu kwann usikomae na maisha yako badala ya kuzungumzia kitu usichoweza kukibadilisha, PUMBAVU KABISA HAMENI NCHI MWENDE NCHI NZURI
 
Ni utetezi wa kijinga na kipumbavu toka Kwa waziri!!

Anawezaje kuhalalisha makosa yake Kwa utetezi wa mbona fulani naye alifanya hivyo?

Kwa ukiri huu, ni wazi sasa kuwa, kumbe Tundu Lissu yuko damn right na kamwe hajawasingizia wote aliowataja akiwemo yeye Hussein Bashe kumiliki kampuni ya ununuzi wa tumbaku na akiwakopa wakulima huko Tabora...

==============================================

Pia kumbe ni kweli, Mwenyekiti wa bodi ya pamba ni ndugu Christopher Gachuma mjumbe wa halmashairi kuu ya CCM taifa ambaye pia ni;

1. Nidiye mnunuzi mkuu wa pamba Tanzania..

2. Ni mmoja wa wamiliki wa vinu vya kuchambulia pamba (ginneries)

3. Ni Mwenyekiti wa bodi ya pamba, bodi inayopanga bei ya pamba ya wakulima na wakati huohuo huyu Gachuma na bodi yake ndiyo isimamie maslahi ya wakulima wa pamba..

=====hapa pana mgongano wa maslahi na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma=====
================================================
Kumbe naye huyu Hussein Bashe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni za ununuzi wa tumbaku huko Tabora na anawakopa wakulima badala ya nipe nikupe..

Halafu wakati huo huo Hussein Bashe ndiye waziri mwenye dhamana ya kilimo na kusimamia maslahi ya wakulima wakiwemo hao wa tumbaku huko Tabora..

====Katika mazingira haya, tusemeje? Je, sio kwamba huu ni mgongano wa maslahi ya umma na ukiukwaji wa sheria na kanuni za maadili ya viongozi wa umma====?

Je, ni halali na inaingia akilini kwa waziri kujitetea kwa kusema mbona fulani naye alifanya kosa kama hilo?
Dalili ya wivu huanza kwa malalamiko
 

Bashe amesema sio dhambi kwa viongozi wa bodi ya pamba kufanya biashara ya pamba, na wala hakuna tatizo kwa wabunge kufanya biashara hiyo ya pamba.

Jana tar 2/9/2023 Lissu aliongelea jambo hili akiwataja viongozi wa CCM ambao akiwepo Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba kutawala biashara hivyo na hivyo kuwaminya wakulima linapokuja suala la kupanga bei.

Bashe ameyasema haya katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Waandishi wa habari leo 3/9/2023

Bashe kajibu kisiasa na kutoongelea mgongano wa maslahi kwa viongozji hao wa CCM kujiingiza kwenye biashara hiyo huku wakiwa kwenye uongozi wa bodi hizo.
Hili jambo angeacha lisemwe na wasio na mgongano wa maslahi. Atulie atadhalilika
 

Bashe amesema sio dhambi kwa viongozi wa bodi ya pamba kufanya biashara ya pamba, na wala hakuna tatizo kwa wabunge kufanya biashara hiyo ya pamba.

Jana tar 2/9/2023 Lissu aliongelea jambo hili akiwataja viongozi wa CCM ambao akiwepo Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba kutawala biashara hivyo na hivyo kuwaminya wakulima linapokuja suala la kupanga bei.

Bashe ameyasema haya katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Waandishi wa habari leo 3/9/2023

Bashe kajibu kisiasa na kutoongelea mgongano wa maslahi kwa viongozji hao wa CCM kujiingiza kwenye biashara hiyo huku wakiwa kwenye uongozi wa bodi hizo.

Mbowe sio mwenyekiti wa bodi ambayo inapanga bei ya mazao ambayo yeye mwenyewe ndiye mnunuzi mkubwa!

Gachuma ni mwenyekiti wa bodi ya Pamba. Bodi ya Pamba ndiyo wapanga bei ya Pamba. Gachuma ndiye munuzi mkubwa wa Pamba🤔 Hii ina uhusiano gani na mbowe. Kama Gwachuma anafanya biashara basi atoke kwenye bodi huu ni wizi wa wazi
 
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepatwa na nini? Mbona Bashe wa kabla ya kuteuliwa kuwa waziri alikuwa machachari sana kuliko huyu wa sasa?

Mazao yote makubwa chini yake yameanguka bei ,pamba, korosha hali ni mbaya. Kwenye tumbaku wakulima hawajalipwa hadi leo!!!kila siku ni ahadi na ngonjera zisizo isha kabisa.

Kitu ambacho hakijui Samia au anakijua lakini ameamua kukaa kimya ni mawaziri wake kugeuka wafanyabiashara wakubwa sana. Ukiona mafuta yameadimika sababu kubwa ni kwamba viongozi wa hiyo wizara ndiyo wamiliki wa vituo vya mafuta kwa hiyo hata yakifichwa ili yapande bei hawaoni shida, pia ukiona mazao ya kilimo hayapandi bei ujue wanunuzi wakubwa wa hayo mazao ni haohao mawaziri wa rais Samia!.
Kumbe sometimes kichwani unakuwaga siyo MTUPU
 
Back
Top Bottom