Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

Mambo mengine tuwe wahalisia BASHE alikuwa sahihi. Chukulia ww upo manyoni una gunia 50 za mahindi unataka kujaza kwa bei ya 35,000/-kwa kuwa mipaka imefungwa huna jinsi umelima kwa taabu jasho Na damu. Lakini MUNGU saidia mipaka imefunguliwa gunia limefika 75,000/- Na linaendelea kupanda
WW NDIO MKULIMA UNGECHAGUA WAPIII?
amewapigania wakulima lakini bahati mbaya.
USIMUBEZE TAFADHARI
 
Kwenye hii issue mama kachemka sanaaaaaa,
 
huo utakuwa upumbavu wa ajabu, bora kilo ifike elfu 10 ili watu wengi waende kulima
Matajiri wengi wanakimbilia kwenye siasa wachache sana wanaojikita kwenye kilimo.

wakulima wengi wanalima heka chache kwa jembe la mkono au plau.
kulima heka nyingi ni gharama alafu pia unapolima ni kama unabeti kwasababu kilimo chetu sehemu kubwa tunategemea mvua,mvua zikigoma mkulima anapata hasara.
 
Kuzuia chakula kisiuzwe nje na wakati serikali haina uwezo kununua ni kuwaonea wakulima,kama serikali inaweza kununua inunue tena kwa bei nzuri,wakati walikuwa wanawauzia watanzania ka tsh.750 hadi 850 kwa kilo lakini utashangaa watanunua kwa tsh.400 kwa kilo.Kwa ujumla Bashe alikuwa sawa kwani mkulima kalima kwa gharama zake ana uhuru wa kutafuta faida ama vipi serikali itoe ruzuku. Msifikiri ni wakulima wadogo kuna watanzania wamewekeza katika mashamba makubwa mtawatia hasara.
 
Achana na Bashe, mpongeze mhe. Rais kwa kuliona hilo. Binafsi naunga mkono hoja na Namshukuru sana Mungu kwa kumpa Rais wetu hekima hiyo.
kauli ya waziri ndio msimamo wa rais na serikali yake, hujui wanachoongeaga ndani ya baraza la mawaziri, hii kauli na baada ya kigundua kosa lao sasa ndio hicho ukisikiacho.
Yawezekana hujui au unajua ila siasa sihasa
 
Hao wakulima walionufaika kwa kuuza mazao nje wako wapi kwanza?

Nina uhakika jimbo lake lote kama kuna wakulima wana-export mazao yao wenyewe hawafiki watano labda Kigwangala pekee yake.

Haijalishi mipaka ipo wazi au la,Wafanyabiashara hununua mazao kwa bei ya soko la ndani.

Hapo Nzega ndogo,Nata hata Ilalwashimba ni mkulima gani anauza nje?

Hata BBT ni suala la muda tu,hiyo pesa bora ingejenga schemes za umwagiliaji.

Gunia la mpunga debe sita ni 100,000+ mpunga mzuri na 78,000-90,000 pishori na ndiyo kilele cha msimu wa mavuno mikoa ya Shinyanga na Tabora.

Wakulima wanaenda kuuza mazao yote kwa tamaa halafu by November hata mbegu hawana.
 
Watu tumekopa tumelima, kwenda kuuza marufuku, hii nchi hii! changamoto sana
 
Hao wakulima walionufaika kwa kuuza mazao nje wako wapi kwanza?

Nina uhakika jimbo lake lote kama kuna wakulima wana-export mazao yao wenyewe hawafiki watano labda Kigwangala pekee yake.

Hapo Nzega ndogo,Nata hata Ilalwashimba ni mkulima gani anauza nje?

Hata BBT ni suala la muda tu,hiyo pesa bora ingejenga schemes za umwagiliaji.

Gunia la mpunga debe sita ni 100,000+ mpunga mzuri na 78,000-90,000 pishori na ndiyo kilele cha msimu wa mavuno mikoa ya Shinyanga na Tabora.

Wakulima wanaenda kuuza mazao yote kwa tamaa halafu by November hata mbegu hawana
Matahira ni wengi , hivi unafikiria Kwa Kutumia akili au Makalio yako? Mkulima anauza Mazao yake Direct Kwa wanunuzi wanaokwenda vijijini kwao , Kwa Hali ya kawaida tunategemea serikali ingeweka utaratibu mzuri wa masoko vijijini, Wewe usio na akili inategemea mkulima afanye Export!! Mkulima kazi yake yeye ni kuuza sehemu au mtu anayetoa Bei ya Juu. Leo Hii wafanyabiashara wa Mahindi wanaokwenda Kibaigwa ama Kiteto , Kondoa, mpwampwa wananunuwa Mahindi Kwa Tshs 90,000/= wakifika Sokoni Manzese wanauza Kwa Gunia Moja Tshs 105000/ hapo usafiri Kwa Gunia Moja no Tshs 8000/= ushuru 1500-2000 Kwa Gunia , mpakiaji Tshs 1000/ mshushaji Gunia 1000/= dalali Sokoni Manzese ni Tshs 1000/ Kwa Gunia
Hapo unaona hata huyo anayenunua Kwa wakulima na kusafirisha Bado anapata Faida ndogo ya Tshs 1000/ Hadi 1500/= Hapo inatokea unakopesha Mahindi hapo Manzese wanakulipa after one week?
Hii sector lazima tuiangalie upya ni sehemu Gani tumekwamaaana sio mkulima Wala mfanyabiashara wa ndani anayefaidika na kilimo
 
Watu wamekopa
Watu tumekopa tumelima ,kwenda kuuza marufuku ,hii nchi hii !changamoto sana
Matrekta Mapya kutegemea kulipa madeni Yao mwezi wa July , wakulima wanadaiwa madeni makubwa kwenye mbegu, kwenye Disiel walizikopeshwa wakalimie, wengine walikopa
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

Nadhani hapa ni Muhimu sasa kuondoa misinformation kwa Mh. Rais, huenda watu wasiokuwa na nia njema wanaweza kupeleka taarifa zisizo za kweli zitakazo pelekea tamko la usitishaji linalochochea kuwakatisha tamaa wakulima.

Badala yake, kiundwe chombo maalumu huru kiwe na uwakilishi mpaka ngazi ya Kiwilaya kitakachokaa na kupitia mahitaji na ndani vs yale ya nje ya mazao ya kilimo, na kutoa mapendekezo. Sio watu wanaamua hakuna kuuza nje, halafu watu wananunua ndani wanaconsolidate, Kisha kesho wanauza nje, lengo la kuzuia ukosekanaji wa Vyakula, linakuwa halijawa.solved ..ila wametengeneza mazingira mazuri kwa economic pedophiles kunufaika.
 
Humu kuna chawa wake wa kutosha, ngoja waibuke kutoka mafichoni.
 
Watakao shangilia hili ni wale ambao hawajawahi kulima ila kwa mkulima hili ni pigo kubwa. Kuna mwaka nililima nikawa nasubiri mda wa bei nzuri niuze kilicho nikuta sitaki tena kurudi shambani tena maisha yangu yote. Wakati wa mavuno gunia la mpunga liliuzwa sh55 nilisubiri miezi 7 badae kusubiri bei nzuri baada ya serikali kufunga mipaka nikaja uza sh35 kwa gunia sababu kuu ikiwa ni serikali kufunga mipaka kuuza chakula nje naona tena mwaka huu watu wakiacha kabisa kujishguhulisha na kilimo.
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

Ni kwamba nchi kwa sasa inaupungufu mkubwa sana chakula, "believe in please!"
 
Ukiwa mkulima utamwelewa Bashe alichokuwa anakitamania kwa wakulima,ni dhahiri kuwa wakulima wa nchi hii wanakosa tija ya kilimo chao kwa ukosefu wa soko la tija kwa mazao yao. Kilimo kina gharama kubwa kifedha, muda na nguvu kufungua mipaka ni moja ya jitihada ya kumkwamua mkulima, suala la uhakika wa chakula kwa nchi ni jukumu la serikali kununua first kupitia vihenge vyake vya chakula wakimeet target wafungue masoko(mipaka) dunia ya leo ni ya soko huria(soko la ushindani)
 
Mambo mengine tuwe wahalisia BASHE alikuwa sahihi. Chukulia ww upo manyoni una gunia 50 za mahindi unataka kujaza kwa bei ya 35,000/-kwa kuwa mipaka imefungwa huna jinsi umelima kwa taabu jasho Na damu. Lakini MUNGU saidia mipaka imefunguliwa gunia limefika 75,000/- Na linaendelea kupanda
WW NDIO MKULIMA UNGECHAGUA WAPIII?
amewapigania wakulima lakini bahati mbaya.
USIMUBEZE TAFADHARI
Mipaka ifungwe au ifunguliwe bei ya mazao kipindi cha mavuno hutegemea ukame au msimu ulikuwa na mvua za kutosha!

Na wafanyabiashara wananunua kwa bei ya soko la huko shamba siyo bei ya Kenya au Sudan.

Mkulima ananufaikaje sasa?
 
Hoja ya kipuuz kabisa , mkulima anapata hizo ruzuku ? Au mnaongea kama wapumbavu hapa ?
Ni nani anayeingia hizo gharama ili wewe na wenzako mpate huo mtelezo wa bei mnaotaka ? , Ni kazi ya mkulima hiyo ?
Ni kazi ya mkulima kukaa na kusikiliza njaa zako ?
Na hiyo kazi ya serikali kununua mazao inamhusu nini mkulima ,? Wewe njanjaa zako unataka umtwike mzigo mkulima

Hao wapuuz wenzako wanaoitwa serikali kupitia NFRA walikuwa wapi muda wote huo kushindwa kununua hayo mazao kutoka kwa mkulima ?

Na ninyi ni takataka gani mpaka kumpangia mkulima la kuuza , ninyi mmeshindwa kulima ? ,Hamna mikono ? ,Ninyi mishahara yenu na mapato yenu kuna anayewapangia matumizi ?
Hahaaaaaa!!!Rais ndio kaamua hivyooo.....sisi wakulima hatupingi, na tunaendelea kulima maaana hata soko la ndani linalipa for now.🤣
 
Sahihi Tena hao wakulima wadogo ndo wameishi maisha magumu sana mwaka Jana na mwaka huu baada ya msimu kuisha maaana vyakula vyote wameuza wanaenda nnua Mchele kwa 3500 unga 2000,maisha Yao yalikua magumu sana

Huko Buchosa, mwaka jana wakati msimu wa kulima mpunga umefika bro wangu mmoja alikuwa anakopesha wakulima pesa kwaajili ya kuendeshea kilimo (40000 kwa gunia moja wakivuna), alikuwa anafatwa yeye tena kwa kubebembelezwa ili awakopeshe, kwa mkataba kupitia ofisi za serikali ya kijiji.

Muda wa mavuno umewadia bei ya gunia sokoni ikaanzia 70000 na mpaka sasa imepanda maradufu yeye kazi yake ikawa ni kukusanya magunia tu. Yani katengeneza faida 30000 Tsh hata kabla hajaenda sokoni, halafu kuna raia zinaleta story za mkulima kufanikiwa?

WAKULIMA WENGI HUUZIA MAZAO SHAMBANI, kwahiyo mfanyabiashara ndio mnufaika siku zote.
 
Hivi mkulima akiuza Gunia lake la Mahindi Tshs 85000/ Hadi Tshs 90,009/ Sio Faida hiyo Kwa mkulima? Umesikia kuwa serikali itanunuwa Mahindi kupitia NFRA na CPB jee unajuwa hao Bei zao huwa ni kiasi Gani Kwa Gunia? Hao NFRA na CPB wakununua Bei kubwa sana itakuwa ni 50,000/ Kwa Gunia hapo Bado usumbufu wa kuamvuwa moisture ni 15, Mahindi machafu, , Wanaopewa tends ni matajiri wao wananuwa then ndio wanapeleka NFRA ila mkulima hawezi uza direct Kwa serikali mfano angalia pale Njia panda ya kapele mkoa wa Songwe wilaya ya momba ama Engusero Kwa wilaya KITETO ndio utajuwa kuwa mkulima anapata mateso
 
Back
Top Bottom