Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Mambo mengine tuwe wahalisia BASHE alikuwa sahihi. Chukulia ww upo manyoni una gunia 50 za mahindi unataka kujaza kwa bei ya 35,000/-kwa kuwa mipaka imefungwa huna jinsi umelima kwa taabu jasho Na damu. Lakini MUNGU saidia mipaka imefunguliwa gunia limefika 75,000/- Na linaendelea kupanda
WW NDIO MKULIMA UNGECHAGUA WAPIII?
amewapigania wakulima lakini bahati mbaya.
USIMUBEZE TAFADHARI
 
Kwenye hii issue mama kachemka sanaaaaaa,
 
huo utakuwa upumbavu wa ajabu, bora kilo ifike elfu 10 ili watu wengi waende kulima
Matajiri wengi wanakimbilia kwenye siasa wachache sana wanaojikita kwenye kilimo.

wakulima wengi wanalima heka chache kwa jembe la mkono au plau.
kulima heka nyingi ni gharama alafu pia unapolima ni kama unabeti kwasababu kilimo chetu sehemu kubwa tunategemea mvua,mvua zikigoma mkulima anapata hasara.
 
Kuzuia chakula kisiuzwe nje na wakati serikali haina uwezo kununua ni kuwaonea wakulima,kama serikali inaweza kununua inunue tena kwa bei nzuri,wakati walikuwa wanawauzia watanzania ka tsh.750 hadi 850 kwa kilo lakini utashangaa watanunua kwa tsh.400 kwa kilo.Kwa ujumla Bashe alikuwa sawa kwani mkulima kalima kwa gharama zake ana uhuru wa kutafuta faida ama vipi serikali itoe ruzuku. Msifikiri ni wakulima wadogo kuna watanzania wamewekeza katika mashamba makubwa mtawatia hasara.
 
Achana na Bashe, mpongeze mhe. Rais kwa kuliona hilo. Binafsi naunga mkono hoja na Namshukuru sana Mungu kwa kumpa Rais wetu hekima hiyo.
kauli ya waziri ndio msimamo wa rais na serikali yake, hujui wanachoongeaga ndani ya baraza la mawaziri, hii kauli na baada ya kigundua kosa lao sasa ndio hicho ukisikiacho.
Yawezekana hujui au unajua ila siasa sihasa
 
Hao wakulima walionufaika kwa kuuza mazao nje wako wapi kwanza?

Nina uhakika jimbo lake lote kama kuna wakulima wana-export mazao yao wenyewe hawafiki watano labda Kigwangala pekee yake.

Haijalishi mipaka ipo wazi au la,Wafanyabiashara hununua mazao kwa bei ya soko la ndani.

Hapo Nzega ndogo,Nata hata Ilalwashimba ni mkulima gani anauza nje?

Hata BBT ni suala la muda tu,hiyo pesa bora ingejenga schemes za umwagiliaji.

Gunia la mpunga debe sita ni 100,000+ mpunga mzuri na 78,000-90,000 pishori na ndiyo kilele cha msimu wa mavuno mikoa ya Shinyanga na Tabora.

Wakulima wanaenda kuuza mazao yote kwa tamaa halafu by November hata mbegu hawana.
 
Watu tumekopa tumelima, kwenda kuuza marufuku, hii nchi hii! changamoto sana
 
Hapo unaona hata huyo anayenunua Kwa wakulima na kusafirisha Bado anapata Faida ndogo ya Tshs 1000/ Hadi 1500/= Hapo inatokea unakopesha Mahindi hapo Manzese wanakulipa after one week?
Hii sector lazima tuiangalie upya ni sehemu Gani tumekwamaaana sio mkulima Wala mfanyabiashara wa ndani anayefaidika na kilimo
 
Watu wamekopa
Watu tumekopa tumelima ,kwenda kuuza marufuku ,hii nchi hii !changamoto sana
Matrekta Mapya kutegemea kulipa madeni Yao mwezi wa July , wakulima wanadaiwa madeni makubwa kwenye mbegu, kwenye Disiel walizikopeshwa wakalimie, wengine walikopa
 
Nadhani hapa ni Muhimu sasa kuondoa misinformation kwa Mh. Rais, huenda watu wasiokuwa na nia njema wanaweza kupeleka taarifa zisizo za kweli zitakazo pelekea tamko la usitishaji linalochochea kuwakatisha tamaa wakulima.

Badala yake, kiundwe chombo maalumu huru kiwe na uwakilishi mpaka ngazi ya Kiwilaya kitakachokaa na kupitia mahitaji na ndani vs yale ya nje ya mazao ya kilimo, na kutoa mapendekezo. Sio watu wanaamua hakuna kuuza nje, halafu watu wananunua ndani wanaconsolidate, Kisha kesho wanauza nje, lengo la kuzuia ukosekanaji wa Vyakula, linakuwa halijawa.solved ..ila wametengeneza mazingira mazuri kwa economic pedophiles kunufaika.
 
Humu kuna chawa wake wa kutosha, ngoja waibuke kutoka mafichoni.
 
Watakao shangilia hili ni wale ambao hawajawahi kulima ila kwa mkulima hili ni pigo kubwa. Kuna mwaka nililima nikawa nasubiri mda wa bei nzuri niuze kilicho nikuta sitaki tena kurudi shambani tena maisha yangu yote. Wakati wa mavuno gunia la mpunga liliuzwa sh55 nilisubiri miezi 7 badae kusubiri bei nzuri baada ya serikali kufunga mipaka nikaja uza sh35 kwa gunia sababu kuu ikiwa ni serikali kufunga mipaka kuuza chakula nje naona tena mwaka huu watu wakiacha kabisa kujishguhulisha na kilimo.
 
Ni kwamba nchi kwa sasa inaupungufu mkubwa sana chakula, "believe in please!"
 
Ukiwa mkulima utamwelewa Bashe alichokuwa anakitamania kwa wakulima,ni dhahiri kuwa wakulima wa nchi hii wanakosa tija ya kilimo chao kwa ukosefu wa soko la tija kwa mazao yao. Kilimo kina gharama kubwa kifedha, muda na nguvu kufungua mipaka ni moja ya jitihada ya kumkwamua mkulima, suala la uhakika wa chakula kwa nchi ni jukumu la serikali kununua first kupitia vihenge vyake vya chakula wakimeet target wafungue masoko(mipaka) dunia ya leo ni ya soko huria(soko la ushindani)
 
Mipaka ifungwe au ifunguliwe bei ya mazao kipindi cha mavuno hutegemea ukame au msimu ulikuwa na mvua za kutosha!

Na wafanyabiashara wananunua kwa bei ya soko la huko shamba siyo bei ya Kenya au Sudan.

Mkulima ananufaikaje sasa?
 
Hahaaaaaa!!!Rais ndio kaamua hivyooo.....sisi wakulima hatupingi, na tunaendelea kulima maaana hata soko la ndani linalipa for now.🤣
 
Sahihi Tena hao wakulima wadogo ndo wameishi maisha magumu sana mwaka Jana na mwaka huu baada ya msimu kuisha maaana vyakula vyote wameuza wanaenda nnua Mchele kwa 3500 unga 2000,maisha Yao yalikua magumu sana

Huko Buchosa, mwaka jana wakati msimu wa kulima mpunga umefika bro wangu mmoja alikuwa anakopesha wakulima pesa kwaajili ya kuendeshea kilimo (40000 kwa gunia moja wakivuna), alikuwa anafatwa yeye tena kwa kubebembelezwa ili awakopeshe, kwa mkataba kupitia ofisi za serikali ya kijiji.

Muda wa mavuno umewadia bei ya gunia sokoni ikaanzia 70000 na mpaka sasa imepanda maradufu yeye kazi yake ikawa ni kukusanya magunia tu. Yani katengeneza faida 30000 Tsh hata kabla hajaenda sokoni, halafu kuna raia zinaleta story za mkulima kufanikiwa?

WAKULIMA WENGI HUUZIA MAZAO SHAMBANI, kwahiyo mfanyabiashara ndio mnufaika siku zote.
 
Hivi mkulima akiuza Gunia lake la Mahindi Tshs 85000/ Hadi Tshs 90,009/ Sio Faida hiyo Kwa mkulima? Umesikia kuwa serikali itanunuwa Mahindi kupitia NFRA na CPB jee unajuwa hao Bei zao huwa ni kiasi Gani Kwa Gunia? Hao NFRA na CPB wakununua Bei kubwa sana itakuwa ni 50,000/ Kwa Gunia hapo Bado usumbufu wa kuamvuwa moisture ni 15, Mahindi machafu, , Wanaopewa tends ni matajiri wao wananuwa then ndio wanapeleka NFRA ila mkulima hawezi uza direct Kwa serikali mfano angalia pale Njia panda ya kapele mkoa wa Songwe wilaya ya momba ama Engusero Kwa wilaya KITETO ndio utajuwa kuwa mkulima anapata mateso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…