Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu. Lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.
Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani. Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.
Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanya biashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.
Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa rais wa JMT la kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.
Tunafurahia mazao kutokuuzwa nje ya nchi ili wakulima wetu wafilisike? Mbona vitu vingi tunauza nje na hakuna tatizo? Mbona Tanzania inanunua nguo kutoka nje badala ya kutumia pamba na hakuna tatizo? Mimi siungi mkono zuio la mauzo ya mazao nje ya nchi kwa sababu soko la ndani linawahujumu sana wakulima. Tunajua kuwa nguvu kazi kubwa ya nchi ipo katika shughuli za kilimo, lakini kwa sababu kilimo hakilipi watu wanakimbilia mjini ili kufanya uchuuzi. Pale ambapo kilimo kitapewa kipaumbele na kikawa kinalipa watu wetu wataongeza uzalishaji kwa ajili ya soko la ndani na nje. Bila soko la nje kilimo cha mazao kitakuwa hakina maana kwa Watanzania.
Inafika mkulima anauza gunia moja la mahindi kwa Tsh.25,000 halafu hakuna anayejiuliza alizalisha gunia moja la mahindi kwa gharama gani.
Ukiamua kufanya mahesabu ya kulizalisha gunia moja la mahindi linaliuzwa kwa Tsh.25,000 ni unyonyaji kwa sababu gharama ya uzalishaji ipo juu sana. Chukua mfano ufuatao kwa gharama ya kukuza mahindi kwa eka moja:
Mbolea 1-kupandia (bila ruzuku) = Tsh.150,000
Kulima kwa Trekta x 2 (eka moja) = Tsh.100,000
Kg.8 @8,000 = Tsh.64,000
Palizi la shamba = Tsh.30,000
Kuvuna = Tsh.50,000
Jumla ya gharama kwa mchanganuo hapo juu ni Tsh.394,000
Hapo mkulima hajahesabu gharama zingine kama kusafirisha/mbolea ya kukuzia/kupukuchua
Kwa eka 1 kwa uzalishaji wa uhakika unaozingatia kilimo cha kisasa utapata gunia 20, hivyo
20@Tsh.25,000 = Tsh.500,000.
Kwa hiyo hakuna faida ya maana inayopatikana kwa kuuza mazao katika soko la ndani.