Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Mkuu Maxence Melo ebu tupia ile katuni aliyo ichoraga Said Michael, ikimuonyesha Max nyuma ya Desktop kavaa suit nyeusi na Bashe akiwa amesimama nyuma kidogo ya Max akimwambia maneno flani hivi...🔥🤣
 
Ndio maana Huwa nawaambia watu uwekezaji wowote ndani ya Tanzania lazima uwekeze kimachale sana yaan mguu nje mguu ndani hususani sisi watu wa vipato vya chini. Leo umejipinda shambani kulima kwa gharama, haya mama huyo katoa tamko inamaana kuuza mazao kwa hasara kunakuja mbeleni
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu. Lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani. Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanya biashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa rais wa JMT la kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.
Tunafurahia mazao kutokuuzwa nje ya nchi ili wakulima wetu wafilisike? Mbona vitu vingi tunauza nje na hakuna tatizo? Mbona Tanzania inanunua nguo kutoka nje badala ya kutumia pamba na hakuna tatizo? Mimi siungi mkono zuio la mauzo ya mazao nje ya nchi kwa sababu soko la ndani linawahujumu sana wakulima. Tunajua kuwa nguvu kazi kubwa ya nchi ipo katika shughuli za kilimo, lakini kwa sababu kilimo hakilipi watu wanakimbilia mjini ili kufanya uchuuzi. Pale ambapo kilimo kitapewa kipaumbele na kikawa kinalipa watu wetu wataongeza uzalishaji kwa ajili ya soko la ndani na nje. Bila soko la nje kilimo cha mazao kitakuwa hakina maana kwa Watanzania.

Inafika mkulima anauza gunia moja la mahindi kwa Tsh.25,000 halafu hakuna anayejiuliza alizalisha gunia moja la mahindi kwa gharama gani.

Ukiamua kufanya mahesabu ya kulizalisha gunia moja la mahindi linaliuzwa kwa Tsh.25,000 ni unyonyaji kwa sababu gharama ya uzalishaji ipo juu sana. Chukua mfano ufuatao kwa gharama ya kukuza mahindi kwa eka moja:
Mbolea 1-kupandia (bila ruzuku) = Tsh.150,000
Kulima kwa Trekta x 2 (eka moja) = Tsh.100,000
Kg.8 @8,000 = Tsh.64,000
Palizi la shamba = Tsh.30,000
Kuvuna = Tsh.50,000
Jumla ya gharama kwa mchanganuo hapo juu ni Tsh.394,000
Hapo mkulima hajahesabu gharama zingine kama kusafirisha/mbolea ya kukuzia/kupukuchua
Kwa eka 1 kwa uzalishaji wa uhakika unaozingatia kilimo cha kisasa utapata gunia 20, hivyo 20@Tsh.25,000 = Tsh.500,000.

Kwa hiyo hakuna faida ya maana inayopatikana kwa kuuza mazao katika soko la ndani.
 
Ndio maana Huwa nawaambia watu uwekezaji wowote ndani ya Tanzania lazima uwekeze kimachale sana yaan mguu nje mguu ndani hususani sisi watu wa vipato vya chini. Leo umejipinda shambani kulima kwa gharama, haya mama huyo katoa tamko inamaana kuuza mazao kwa hasara kunakuja mbeleni
Kwa ukweli Tanzania kila siku sera zake zinabalika utafikiri hali ya hewa.
 
Watu walikuwa wanaanza kujiajiri kwenye kilimo. Vijana hawa mtawapa kazi gani? Matatizo mengine ni ya kujitakia tu.
 
Kuna mengi sana yatatokea kutuondoa kwenye mada
 
Ungekuwa wewe ungejiuzulu?

20230228_101830.jpg
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu. Lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani. Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanya biashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa rais wa JMT la kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.
Uzalendo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Kama Rais anawapangia wakulima bei basi mei mosi akiwa anatangaza mishahara mipya na nyongeza atangaze na bei za mazao ya wakulima la sivyo hana mpango na kukua kwa sekta ya kilimo.
Ngoja tulime maparachichi , chai ma tumbaku tuone kama mtakula
 
Huyu msomali hawezi kujiuzulu kwa vile wapo pale kwa ajili ya njaa na siyo sifa stahiki
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi...
Muwe mnaunganisha dots.Juzi Rais alisema mazao mengi ya chakula yanauzwa nje na hatupati fedha za kigeni.

Leo Rais kasema Ghala la chakula litapewa pesa kukusanya Tani laki Tano.

Kumbuka toka Magufuli NFRA ilikuwa inanua tani 10000.

Nyie mnadhani hizo tani laki Tano zote ni hifadhi tu na mnajua kwanini kaitolea hiyo kauli Kanda ya ziwa?

Rais Wala hajatangaza kufunga mpaka.Jifunzeni kuunganisha dots.
 
Unafikiri kinachohitajika ni nini kati ya kuongeza uzalishaji wa ndani Ili kuweza kututoshereza ama KUFUNGA mipaka ya kibiashara?

Hoja ya kuwanifaisha middle men je, hii Ina ukweli kiasi Gani?
 
Back
Top Bottom