Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

kuna muda nikasikia Rais kaidhinisha kuingiza tani kadhaa za mchele kufidia upungufu wa chakula, sasa nikashangaa Rais na waziri wake awawasiliani ama ni vipi!
 
Bashe hamna kitu mule kiingereza kingi kujifanya mjuaji ili Hali hakuna chenye manufaa anachokifanya
 
Acha upotoshaji mkuu, unajua faida ya export kwenye uchumi wa nchi au unaleta tu ushabiki wa
Tuondoleeni upuuzi wenu.....unatetea export ya mazao ya chakula?

Nani kasema export ya cash crops imzuiwa? Yaani mnashindwa ku think big katika hili?
 
Unauza Bandari nje kwa hasara halafu unazuia kunde kuuza nje na watu humu ndani mnashangilia. Sisi ni sample bunge letu na viongozi wetu tuna Major the minor.
Ngoja wakulima walime kukidhi chakula na kugeukia mazao ya biashara tuone kama mtakula korosho na ufuta.
Maana hapo zao linalozuiwa ni mahindi na mchele si kingine
 
Ukitaka kuwa fukara nchi hii kuwa mkulima. Unalima wewe masoko/bei wanapanga wengine.

Ni kawaida sana bei za mazao mbalmbali (haa ya biashara) kuwa regulated, sio Tz tu.

Sio kweli kuwa sector ya kilimo hailipi kwa Tz, ni kwamba wanaonufaika ni gurus wa biashara ya nafaka (wanasiasa) pamoja na madalali masokoni.

Yani chakula kiuzwe nje au ndani, anaenufaika ni mfanyabiashara ndiomaana mimi huwa sioni point yoyote kusema "Mkulima anaenda kunufaika"

KILIMO UKIFANYE NA MTAJI MKUBWA, kiasi kwamba kila hatua usihitaji msaada wa wafanyabiashara, kitu ambacho wengi hawawezi.
 
Gharama za kilimo Cha mahindi:-
1. Kukodi ekari Moja ni Tshs 50,000/= eneo pori namba moja
2. Mbegu kg 6 ni Tshs 30,000/=
3. Wapandaji watano. 15,000/=
4. Kulima na Trecta. 40,000/=
5. Palilizi ya kwanza. 30,000/=
6. Palilizi ya pili. 25,0000=
7. Gharama za kuvuna 20,000/=
8. Gharama za kupukucha 25,000/=
9. Kubeba kutoka Shambani. 10,000/=
10. mfuko tupu moja. Bbb 700/=
Jumla ya gharama zote ni zaidi ya 245000/= Kwa ekari Moja, na Ekari Moja unaweza pata kati ya Gunia mbili Hadi tatu. Mwaka huu wengi Mahindi yameshia kwenye lenta Kwa sababu ya jua, na waliovuna wamepata wastani Wagunia Moja Kwa ekari Moja, Sasa unapozuia kuuza Mahindi Kwa Bei yenye madlahi au yenye kurudisha gharama za uzalishaji jioni unamkandamiza huyu mkulima wa Mahindi?

Watu wakae chini waone wanapunguzaji gharama za uzalishaji, Sector ya Kilimo inathiriwa sana na kupanda Kwa Disiel kunapandisha gharama za uzalishaji na uchukuzi.

Unapuuza Disiel Kwa mkulima kipindi Cha Kulima Disiel elikuwa 3000plus, hakuna aliona hiyo athari ya Mafuta kuwa Juu itapandisha Bei za kulimia Kwa matrekta, usafirishaji wa mbegu, kubeba Mazao Shambani,

Hahahah kajamaa kamepigwa za uso na mkuu wake! Lakini Rais Samia amechelewa sana kwani madhara yameshakuwa makubwa sana kila bidhaa haishikiki kabisa ile fungulia mbwa ilikuwa ya kijinga sana tena sana!..
 
Hahahah kajamaa kamepigwa za uso na mkuu wake! Lakini Rais Samia amechelewa sana kwani madhara yameshakuwa makubwa sana kila bidhaa haishikiki kabisa ile fungulia mbwa ilikuwa ya kijinga sana tena sana!
Leo Hii ukipata bahati ya kufika Kiteto eneo la pori namba moja, utawaonea huruma hao wakulima kutokana na gharama wanazoingia na kipato wanachopata .

Mtu anatumia gharama kubwa kipato kidogo, hata Bei elio Sokoni Leo Hii ya 90,000/= haewizi rudisha gharama zake.

Mfano Kuna Bwana Moja maarufu Kwa jina la Mnyalukolo hapo pori namba moja amelima Mahindi Ekari 40, Amevuna Mahindi Gunia 40 na Alizeti Gunia 6, Gharama alizotumia ni zaidi ya 9,000,000/ hayo mavunu hayarudishe hata nusu ya gharama zake,
 
Ukitaka kuwa fukara nchi hii kuwa mkulima. Unalima wewe masoko/bei wanapanga wengine.
Hii ndiyo hoja kuntu.
Mkulima amesaidiwa nini ili kumdhibiti asiuze nje.

Hii ni sawa na baadhi ya viongozi nyakati fulani walipiga marufuku kuuza mahindi ya kuchomwa.

Kuna.baadhi ya wilaya zilipiga marufuku kuuza ndizi nje ya wilaya lakini zenyewe zinaingiza mchele.

Namaanisha mkulima.akombolewe badala ya kudhibitiwa.

Udhibiti unaondoa hoja ya :
JEMBE NI MALI.
 
Acha upotoshaji mkuu, unajua faida ya export kwenye uchumi wa nchi au unaleta tu ushabiki wa kipumbavu hapa,
Ukiharibu soko la wakulima mwakani uzalishaji unapangua then bei itapanda vilevile

Sina hakika ila anayezuia export ya mazao ndo anapaswa kujiuzulu sio Mhe Bashe
We kilaza.
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

HAJAZUIA KASHAURI TUSIUZE NJE, LAKINI AKIZUIA ATAUA SECTA YA KKILIMO BORA CHAKULA KIPANDE BEI TUPANUE MASHAMBA WATU WAACHE KUWANYONYA WAKULIMA
 
Mungu anawaumbua taratibu!

Yale mataahira ya bashe hapa ndani sijui yana hali gani?
Bashe yupo sahihi sana kilimo ni biashara kama biashara zingine inatakiwa wakulima waone faida ya kilimo ili wengi wakalime , kama hakina faida nani atawekeza hela zake na muda knye kitu kisicholipa?
 
yeye.pamoja.na..mama.yake..wanakula.matapishi.yao kwa.sababu.walijifanya.wanajua.sana.kufungua.nchi.waendelee mbona macho.yanawatoka.sasa
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

We choko! Si ukalime na wewe??!! Wenzako wahenyeke mashambani wewe ukae kusubiri chakula cha bei rahisi wakati kuna watu wako tayari kulipa pesa zaidi kwa chukula hicho hicho..? Ukitaka chakula cha bei rahisi lima na wewe...!!!
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.

Kijamaa huwa kinakaza fuvu na kutoa macho kama sangara mbichi kww hoja zisizo na mashiko kabisa
 
Atabadilisha kauli atasema mama kwa upendo mkubwa kabisa amesikia kilio cha wana nchi wake
Bunge pia litasimama kwa dakika 2 kumpongeza rasi kwa uchapakazi na kumpongeza raisi kws kazi nzuri
 
Back
Top Bottom