Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Waziri Bashe anajisikiaje baada Rais kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi? Ni busara akaachia ngazi

Bashe nae ni wale wale. Wezi wa kutumia midomo yao. Kwenye biashara ya mazao Bashe ana personal interest.
 
Acha upotoshaji mkuu, unajua faida ya export kwenye uchumi wa nchi au unaleta tu ushabiki wa kipumbavu hapa,
Ukiharibu soko la wakulima mwakani uzalishaji unapangua then bei itapanda vilevile

Sina hakika ila anayezuia export ya mazao ndo anapaswa kujiuzulu sio Mhe Bashe
Export inapromote productive
 
Kwanini watu hawataki kujifunza kutokana na Maamuzi yetu, Kuna mwaka Tuliamua kuhusu Koroshi Nini kilitokea kwenye Hilo zao ule mwaka weyu Hadi Leo ni Siri ya wale wakulima wa Kusini, Mwaka Jana tumeamua tena kuruhusu Mafuta ya kula kutoka nje Kila mkulima wa Alizeti amepata majibu ya huo uamuzi ulivyosadia kushusha Bei ya Alizeti Toka 95000/ Kwa mwezi 9/2022Hadi Bei kufikia 55000/ mwezi wa 12/2022.

Waliolima Alizeti mwaka huu wanaogopa hata kuvuna Bei walizitarajia hazipo watu wote wanakimbilia Mafuta ya korie or Mafuta Safi, Jee mbona watu kuwapigai kilele Wala viongozi hawataki kywasemea Wakulima walizeti?

Tuwe na sera zinzoeleweka, ninahisi tunashida kwenye policy making or approach zetu kwenye policy zinashida sana, Kuna wakati huwa namuelewa Sana Mh Msukuma kuhusu Wasomi wetu wanashida sana vichwani mwao, ukitaka kujua Hilo la Elimu zinashida angalia sana pitia JF utajuwa wapi tumekwama kwenye elimu
 
Swali la msingi sana la kuujiuliza Kwanini wakenya wameweza kununua Chakula Kwa Misimu zaidi ya Minne(4) nje ya Nchii Yao? Wamekosa mavunu Kwa Misimu mingi ila wanaweza kula na kununua unga Kila siku. Najiuliza hivi ikitokea kwetu hapa japo Misimu miwili hamna Mavuno au yakawa haba Tutaweza kununua Chakula kutoka Kwa majirani zetu? Kama hicho Cha ndani tunashindwa tunapiga kilele Bei Bei zipo Juu? Ndio tuwezi kwenda kunua Gunia La Mahindi Uganda tulilpeleke Mtwara itawezikana? Wenzetu wengi wameweza hili kwakuwa watu wao wengi wapo kwenye Sector ya Ajira , wanadubiris mwisho wa mwezi wapata mishahara wanunue Chakula .Eli nasisi tufikie huko lazima tuwekeze sana kwenye kilimo, Eli tupate malighafi nyingi , tuwezi kuendesha viwanda mbalimbali tupate Ajira vipato viongezeke, Tunalima Mbaazi , Tunalima Dengu, Tunalima Alizeti,, Tunalima miwese ila Bado tuna import Ngano kutoka Canada, Mafuta ya kula kutoka Malaysia na Dubai, product za Mbaazi kutoka India, bidhaa za ngizi kutoka Kenya, furniture kutoka china. Halafu unalalamika Chakula Bei kubwa? SEMA hatuna Hela za kununulia Chakula vipato vyetu ni vidogo
 
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.

Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.

Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.

Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.

Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.





Hawezi Kuachia ngazi Never ever on Earth,
Anatakiwa mamlaka teuzi ibatilishe uteuzi wake kwa kutoshauri Ipasavyo!
Tuliongea sanaaa humu jamvini lakini hatukisikilizwa!
Mazao yameuzwa sanaaa Kenya!
Tumepiga sanaa Kelele wao wakachukulia Ni siasa tuuu!
Ila Haya bwanaa!
Watu kama hawa hawamsaidii Rais Mama Samia Suluhu Hassan!
wanatakiwa Wawekwe pembeni kwanza wawe ni Washauri tuu!
 
Wewe ni mkulima? Gunia linaponunuliwa laki na na ishirini kwa mkulima badala ya elfu sitini,mnufaika ni nani!?

Wafanyabiashara tunayanunua hayo mazao hata kabla mkulima hajajua bei itakuja kuwaje huko sokoni, guts za kupanga bei nikimuwinda shambani hana kwasababu hata mtaji wa kuendeshea hicho kilimo.

Nakubaliana nae nimkopesha 200000 kwa malipo ya 70000 kila gunia, kisha ikifika wakati wa mavuno huko sokoni gunia linasimamia 100000Tsh, nachukua gunia zangu idadi sawa na pesa niliyompa then anabaki na guni zake, mnufaika ni nani?

Wajinga wachache kama wewe waliozoea kutusi hamuwezi kuelewa mambo yanayoendelea field.
 
Hahahah kajamaa kamepigwa za uso na mkuu wake! Lakini Rais Samia amechelewa sana kwani madhara yameshakuwa makubwa sana kila bidhaa haishikiki kabisa ile fungulia mbwa ilikuwa ya kijinga sana tena sana!

Kwa hiyo maamuzi yake bado yanaonekana ya kjikosha na kumtupia zigo Bashe lakini ukweli ni kwambwa Rais anafanya kila maamuzi ili asionekanane anafanana kimaamuzi na mtangulizi wake hata kama jambo ni la msingi …mwisho wa siku ana kumbuka shuka kumekucha!

Matatizo haya yote yamesababishwa na Rais mwenyewe kwani alikuwepo wakati Bashe anatoa kejeli na kutojali kwa hiyo asijitoe kwenye hili
Sidhani kama Mh Rais alimaanisha Wakulima wasiuze Mazao yao wanakotaka!

Mh Rais amesema Serikali itanunua Mazao tani laki Tano kupitia NFRA.

Na akataka Wakulima waiuzie Serikali Mazao kabla ya kuwaza kwenda Nje!

Maana yake ni kwamba Serikali nayo itanunua Nafaka kwa Bei Nzuri kwa Mkulima.

Lakini Mazao Yataendelea kuuzwa kokote wakati Serikali ikifanya Mpango wa kutekeleza Kilimo cha Umwagiliaji ili Wakulima wavune mara 2 kwa Mwaka badala ya mara moja.

Kilimo ni Biashara.
 
Wafanyabiashara tunayanunua hayo mazao hata kabla mkulima hajajua bei itakuja kuwaje huko sokoni, guts za kupanga bei nikimuwinda shambani hana kwasababu hata mtaji wa kuendeshea hicho kilimo.

Nakubaliana nae nimkopesha 200000 kwa malipo ya 70000 kila gunia, kisha ikifika wakati wa mavuno huko sokoni gunia linasimamia 100000Tsh, nachukua gunia zangu idadi sawa na pesa niliyompa then anabaki na guni zake, mnufaika ni nani?

Wajinga wachache kama wewe waliozoea kutusi hamuwezi kuelewa mambo yanayoendelea field.
Acha ujinga wewe,mbona hapa tabora hatufanyiwi hivyo!?..unafikiri wakulima wa Leo ni WA 70-90!?..tuna elimu zetu na tunalima
 
Sidhani kama Mh Rais alimaanisha Wakulima wasiuze Mazao yao wanakotaka!

Mh Rais amesema Serikali itanunua Mazao tani laki Tano kupitia NFRA.

Na akataka Wakulima waiuzie Serikali Mazao kabla ya kuwaza kwenda Nje!

Maana yake ni kwamba Serikali nayo itanunua Nafaka kwa Bei Nzuri kwa Mkulima.

Lakini Mazao Yataendelea kuuzwa kokote wakati Serikali ikifanya Mpango wa kutekeleza Kilimo cha Umwagiliaji ili Wakulima wavune mara 2 kwa Mwaka badala ya mara moja.

Kilimo ni Biashara.
Uko dunia ipi kwenye border huko mahind hayarusuwi kwenda nje ya nchi
 
Wakati Bashe anahubiri Ile Siasa ya Soko holela la Mazao , hususani Mahindi Rais alikuwa nani!?!? Tatizo sio Bashe 😠😠😠
Tatizo ni Uongozi Mbovu.!
Tatizo ni Utawala' Tatizo ni watawala!
Tatizo ni Watawaliwa!
Hakuna Visheni yoyote ya Kilimo na Mazao yake...Tunasubiri kudra ya Mungu!
Tukivuna Mazao mengi Kwa nasibu na Kwa majirani Kuna njaa ..tunajisifu...na kushangilia!
Kukiwa na Upungufu ...tunafunya mipaka!
Yote haya yanatokea Kwa kudura a a Mungu tu !
 
Achana na Bashe, mpongeze mhe. Rais kwa kuliona hilo. Binafsi naunga mkono hoja na Namshukuru sana Mungu kwa kumpa Rais wetu hekima hiyo.
Kila mwenye akili timamu lazima aunge mkono. Ni Mazuzu wachache tu wanaojifanya wakulima Kwa kiwanyonya wakulima.
 
Hivi Rais amepiga marufuku ama anawapa wafanya biashara fursa kuwa serikali yao itanunua hayo mahindi.

Hivyo wasubirie, lkn wale wenye haraka watauza tu.
 
Kwa mara ya kwanza Leo ndio athari imeanza kujitokeza ya kuzuia kuuza Mahindi nje, Sokoni Manzese Bei imeshuka kutoka Tshs 980/ Kwa Kg Hadi 810/= ila Bei ya Sembe imebaki pale pale haejashuka wenye Mashine za Sembe wanauza Bei Ile Ile, Na Kwa wakulima Wa mashambani Mah Wafaindi yameshia kutoka 85000/= Kwa Gunia Hadi 60,000/= Hapo ndio tunajuwa aliyekuwa anafaidi ni mkulima ama mnunuzi, wafanyabiashara na Madalali hawezi kuasirika hata kidogo wao wanashusha Bei Kadri watakavyo, Leo Hii mkulima amepata hasara ya Tshs 25000/ Kwa Gunia. Tusubiri Hadi jumatatu wakulima watazidi kulia Bei itakuwa 50,000/ lakini sembe itabaki pale pale , na wajanja wa Kasikazini watazidi kutoboa Kibishi kwenye hayo masoko yaliyokatazwa, Muda ni rafiki mzuri tusubiri tuone.
 
Wakulima wanachezewa kwa sababu hawajitetei, wapowapo tu, Bei nzuri zimewabeba sana msimu uliopita, ingeendelea hivi miaka miwili, kila mtu angelima, Ila hatimae fitina ya wavivu imeshinda, wanaofanya hii dhihaka ya kufunga mipaka wanasema wanamsaidia mkulima!!! Wakulima kimyaaa kufika mwezi wa tisa debe la mahindi litakuwa 6000, huku mfuko wa mbolea ya ruzuku 70,000 inaumiza Ila bei ndogo ndio usalama wa chakula na nchi, umasikini wa wakulima ndio amani ya Taifa!!!!
 
Back
Top Bottom