Waziri Bashe tafakari uwezo wako kabla hujaharibu kabisa sekta ya Kilimo

Kwa aina hii ya matumizi ya pesa za umma, tozo zitaendelea kuwaumiza wananchi maskini.
Mabilioni ya tozo hawa Freemasons wameshayateketeza ndani ya dakika chache hawa Freemasons tusipowadhibiti 2025 then tupo ka
 
Unadhani wakisema soko la nje ni nchi za ulaya basi. Ukitoa pamba na korosho ambazo zinaenda China na India sijui ni kitu gani tena tunauza nje ya mipaka ya Africa.

Mazao mengine mnunuzi mkubwa ni Kenya na yeye hiko hiko anachochukua Tanzania auze South Sudan, soko la ndani kwake, Ethiopia na Somalia. Wateja wengine directly kwetu hapo Burundi, Rwanda na Congo.

Sasa Congo, Somalia na South Sudan; kwenye chakula tatizo ni instability ya serikali zao zinazo sababisha kusua kwenye sector ya kilimo. Bila ya migogoro wala hawana shida na chakula hasa nafaka za Tanzania.

Kwa mfano kipindi hiki cha mapigano Sudan ndio kabisa demand ni muda itakuwa kubwa. Kwa ivyo ni wakutengeneza hela kwa wakulima uchwara ambao ni wananunua mashambani na kupeleka kwenye hayo masoko.

Lakini hizo nchi zikiwa stable hiyo demand wala isingekuwepo. Wateja wa asili kwa chakula cha Tanzania ni Kenya, Rwanda na Burundi. Hiyo export yenyewe ya mazao yote aifiki ata dollar billion mbili, we are not main players in food export kwenye bara letu.

Tunatatizo la yield per hector kwa wakulima wa africa; kulinganisha na nchi zilizoendelea. Badala ya ku focus kwenye kuongeza yield kwa ardhi ambayo inatumika tayari. Wao wanawaza miradi ya upigaji tu. Nchi kama South Africa na Egypt ambao sidhani ata asilimia 10 ya wananchi wakulima lakini atufikii ata asilimia 10 ya thamani ya food exports zao.
 
Natabiri Bashe kutumbuliwa hivi karibuni

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hapana alipendekeza kuwa ni bora kuwatumia vijana ambao tayari wanajishughulisha na kilimo wawezeshwe!!na walime mazao yanayotumia muda mfupi kukomaa (miezi 3-6) kwani itawafanya wapate pesa mapema.
white whizard nakubaliana kabisa na hii point , hata mimi nilishwahi kushauri wafanye juu chini kuwapata watu ambao tayari wapo knye industry kwa muda mrefu ila wanakwama mitaji, ardhi na mifumo mizuri . NADHANI WIZARA INAPITA HUMU ICHUKUE USHAURI
 
NDUGU naomba uwe na data kidogo usiwadnganye watanzania, tunauza nje kahawa, chai, tumbaku, mkonge, ufuta, dengu bado tuna matunda na maua sasa , Tuna potential kubwa sana ya kuwa food basket of Africa kwa sababu populations inakua kwa nchi zote zinazotuzunguka na matatio hayataisha na matumizi mbadala ya mazao bado yapo
 
Point hii nimeielewa sana
 
Kuna mbunge mmoja jana amemwambia "unachukua vijana wenye viduku mjini unawapa mashamba hawataweza,halafu unampa zao hadi kuvuna ni miaka 4,watayakimbia tu?kilimo sio kazi rahisi hivyo.
Hili nimeshaangaa pia, kwa muda huo wa miaka minne atawezaje kujitegemea? Au ataendelea kuhudumiwa na serikali?
 
Kwa hivyo unadhani nilipotaja atufikii ata 10% ya food export ya South Africa na Egypt ni mambo niliyoyatoa kichwani tu sio kwamba hizo takwimu zipo.

Na kukusaidia tu kwenye exports za kila kitu (total export) ndio kabisa atafukii ata 10% ya nchi inayo shika nafasi ya kumi kwa Africa ndio maana ata sikutaka kulinganisha huko.

Tanzania inaweza kuwa in export kila kitu ulichotaja hapo, ila individual sums zake zipo on 10’s of millions au 100s of million. The latter ni hizo bidhaa chache nilizotaja nje ya africa korosho, kahawa na cotton. Sasa angalia global export value ya kila hapo utakuta ni over $10 mpaka $30 billion. Wewe mwenye mauzo ambayo yapo in 10’s of million unadhani kwenye global demand za dunia ata usipo export unaweza influence prices kweli.


Google ‘value of food exports from Africa’ halafu uone kama tumo kwenye top ten, ata Somalia na Kenya atuwazidi kwenye food export alone. Ukitafuta data za total export za kila kitu za Africa ndio kabisa Tanzania sio big player. .
 
Madai yake eti ana-dream big..
The dude is dreaming backward.
Utadhan ni mwalimu na vijiji Vyake vya ujamaa.., ambavyo mpaka Karne hii unawasikia wabunge wakiviombea umeme,maji,shule,vituo vya afya , barabara, mawasiliano.... literally ni kama walirundikwa tuu kama wanyama...

Sasa huyu Waziri wenu anajifanya Waziri wa Ardhi,anawagawia vijana plots na kuwawekea Mabomba ya maji yasiyo na uhakika, analazimisha fani kwa vijana wa chips mayai..He will fail miserably.

Hiyo pesa anayoenda kuichezea angeiwekeza kwenye Bank ya kilimo na yeye Kazi yake ingekuwa kuwahamasisha Watanzania wenye Nia ya kujishughulisha na kilimo wachukue mikopo yenye masharti nafuu.

Waswahili wanasema unaweza kumpereka mbuzi mtoni ,but huwezi kumlazimisha anywe maji, Bashe anawapereka Mbuzi Mtoni.
 
Kwanini serikali/wizara isiwaongezee uwezo hao wanaoitwa wakulima wadogo wadogo ili wawe na tija na kuinfluence jamii kujiunga na kilimo, Waziri anafikiri watu hawataki kulima kwa sababu ya Ardhi tuu!?...Hao vijana anaowakusanya ukichunguza ,wengi wao wameacha mashamba makubwa vijijini kwao na kukimbilia mijini.

Vijana hao wangekua wanarudi vijijini kusalimia ndugu zao wakulima, wakakuta kuna godowns na fuso zinapakia mazao, yard kuna Tractors na land cruiser pick ups, maji bombani, na umeme solar or Tanesco, sebuleni watoto wanaangalia DStv, Fridge inaunguruma, wallah Waziri asingeona vijana wanatoka SUA wanaenda Dar au DOM wakati wa vikao vya Bunge Kudanga...wote wangerudi vijijini/mashambani kwenda kulima na kufuga, mjini wangekua wanakuja kwenda Embassy kuchukua visa na kufanya shopping ya VSOPs na kurudi zao Farms.
 
Post zako #71 & 72 ingelikuwa huko bungeni anaulizwa hayo maswali ayatolee ufafanuzi na justification ya hatua zake, tusingefika tulipo.

Ni kuchezea hela za walipa kodi.
 
I second you. Community farming ni uzezeta.
 
Ndio maana nawaambiga kwamba Tanzania tuna wanasiasa wanafiki wanaishi kutegemeana na anayewaongoza wameshamuona mama yeye si wa field ndio maana wanamdanganya Kwa hesabu ambazo ata kichaa hawezi kukubali.
 
Hebu Acha kuongea ujinga wako. Hii nchi years and years imekuwa ikilishwa na wakulima WA kawaida na changamoto zao zinajulikana.

Hebu piga simu Kwa ndugu zako wakulima tanzania waulize bei ya mbolea sasa hivi ni how much ? Mnaongea ujinga WA kilimo cha PDF na iPad
 
Post zako #71 & 72 ingelikuwa huko bungeni anaulizwa hayo maswali ayatolee ufafanuzi na justification ya hatua zake, tusingefika tulipo.

Ni kuchezea hela za walipa kodi.
Yeye Kazi yake ni kuwajibu wabunge kwa kejeli... yaani sometimes I wonder how do these people get there!?....kama kweli waganga wapo basi nadhan kama nchi tuwageukie Hawa waganga waache kuwasaidia hawa mediocre. Kwasababu mimi sitaki kuamini huyu jamaa ndio the Best we can have kwenye hiyo Docket...Na I just pray to God hayo mawazo asije akawa kayatoa kwa wataalam wa wizara, am really hoping ni mawazo yake binafsi, na kama ni mawazo ya Think Tank ya Wizara basi ninaelewa ni kwanini Tanzania tunaitwa maskini.
Post zako #71 & 72 ingelikuwa huko bungeni anaulizwa hayo maswali ayatolee ufafanuzi na justification ya hatua zake, tusingefika tulipo.

Ni kuchezea hela za walipa kodi.
 
kwa hiyo mkulima azalishe kwa ghrama za juu akuuzie kwa bei ya chini kisa nini? mbona hamwapangii wazalishaji wa cement au soda? Ujinga wa kiwango cha juu sana ndo maana watu walikikimbia kilimo, kama unaona vitu ghali zalisha vyako au badilisha mlo tu kula mtama na muhogo
 
Bashe ni akili kubwa nyie ngumbaru hamuwezi kumuelewa bakieni kujadili mambo madogo na matukio ya siasa..

Kwa taarifa Yako Bashe atakuwepo hapo Hadi ajenda 10/30 .

Mwisho mh.Rais tafuta Waziri mwenye akili kama Bashe kule Mifugo na Uvuvi Kuna hela ila hakuna watu wenye akili Wala maono walau awekwe hata Gwajima au Pro.Muhongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…