Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani yeye ni mtendaji wa chama?

Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.

Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.

Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.

huo utaratibu unatusaidia nn wananchi???

Makonda piga kazi nchi mbovu sana hii
 
Waziri Bashe yuko sahihi kwa asilimia mia kwenye kauli yake hii. Serikali ndio mtawala na waziri anawajibika kwa Rais aliyemteua. Hii habari ya chama kujifanya ndio wenye ilani na kuingilia mambo ya taaluma na utawala si mahali pake. Nafarijika kuona baadhi ya watu akiwemo Bashe wanaanza kuuona ukweli na kuonyesha msimamo hadharani ....Big Up Bashe!!.🫶
 
Ni sawa na kusema huyo ‘Bi Tozo’ hana jeuri ya kutumbua mtu.

Mawaziri ambao ni wasaidizi wake wameharibu popularity ya raisi kila kitu kinaenda mrama.

Badala ya kuwatumbua, mama watu kaamua atengeneze sinema yake ya ‘hadaa’ kwa wananchi aonekane anajali. Halafu anatokea mtu anataka kutia kitumbua mchanga na hiyo move yenyewe.

Kwani huyo Makonda ukienda kanda ya ziwa baada ya ziara yake unadhani utakuta kuna hata moja limetekelezwa aliloagiza. Si wote wanajua sio boss wao ila wanacheza sinema ya ‘bi-tozo’ tu.

Kumvaa Makonda hadharani ni sawa na kuujaribu uvumilivu wa raisi hasa kwa mawaziri walioharibu kama Bashe.

Watch this space
 
Kiserikali Bashe yuko sahihi... lakini ukiangalia aina ya mfumo wetu, viongozi wa chama bado ni wakubwa kwa Bashe.
Kumbuka Rais aliyemteua ni Mwenyekiti wa chama chake, anawasiliana na Bashe kama Rais na Mwenyekiti kwa hiyo anachofanya Mwenezi ni kuuza sura na kutafuta milage ya kisiasa kwake yeye binafsi kupitia chama chake.
 
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613
Asuburi wakati akirudisha fomu ya kuomba CCM kupitishwa kwa jina lake kugombea ubunge au teuzi mbalimbali ndo atajua bosi wake ni nani!!
 
Back
Top Bottom