butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Kwa Tanzania ni ngumu kutenganisha serikali na Chama,Rais ndiyo Mwenyekiti wa CCM na ata ikitazama Wajumbe wa Kamati kuu ya chama Spika wa Bunge ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM pamoja na Waziri Mkuu.Kwani yeye ni mtendaji wa chama?
Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.
Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.
Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.
Hoja yako ingekuwa na mashiko kwa mfumo wa nchi kama Afrika Kusini Mwenyekiti wa ANC siyo Rais wa nchi.
Makonda anawahoji Watendaji kwa niaba ya Wananchi waliotoa kero zao!
Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app