Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613
Nashindwa kuelewa watu sijui wanakwama wapi, chama ambacho ndio chenye rais wa nchi, ndiyo nguvu ya nchi iliyo, serekali Huwekwa na chama kwa ngazi zote, chama huituma serekali na kuipa majukumu sera na kila kitu, Makonda ndiye mdomo wa chama hakuna namna waandamizi wavumilie tu, chama hakiko tayari kuona sera zake hazitekelezwi, kama kiko makini kitaikaripia serekali na pengine kuiwajibisha, POWER OF POLITICAL PARTY, CCM.
 
Nashangaa Mwenezi wa Chama anamkoromea Mkurugenzi kuwa anaweza kumtumbua. Na Mkurugenzi alivyo kilaza anaanza kuimba Rashi. Ngoja Makonda awadharilishe, maana watu wenyewe hawajitambui.
Nyie ndo hamjui mnataka nini. Watendaji wakiachwa mnalalamika, wakishughulikiwa mnalalamika! Wakila Rushwa mnalalamika, wakidhibitiwa mnalalamika!!!

Hii nchi watu wake Kuna nati zimelegea vichwani
 
Tusubiri mpenda league ajibuu tulias hapo hapo.......utasikiaaa jibu kwa sauti kubwaaa
 
Nashindwa kuelewa watu sijui wanakwama wapi, chama ambacho ndio chenye rais wa nchi, ndiyo nguvu ya nchi iliyo, serekali Huwekwa na chama kwa ngazi zote, chama huituma serekali na kuipa majukumu sera na kila kitu, Makonda ndiye mdomo wa chama hakuna namna waandamizi wavumilie tu, chama hakiko tayari kuona sera zake hazitekelezwi, kama kiko makini kitaikaripia serekali na pengine kuiwajibisha, POWER OF POLITICAL PARTY, CCM.
Hakika
 
Wewe unazungumzia mfumo wa chama kimoja wa Kikomunisti kama wa China.
Nashindwa kuelewa watu sijui wanakwama wapi, chama ambacho ndio chenye rais wa nchi, ndiyo nguvu ya nchi iliyo, serekali Huwekwa na chama kwa ngazi zote, chama huituma serekali na kuipa majukumu sera na kila kitu, Makonda ndiye mdomo wa chama hakuna namna waandamizi wavumilie tu, chama hakiko tayari kuona sera zake hazitekelezwi, kama kiko makini kitaikaripia serekali na pengine kuiwajibisha, POWER OF POLITICAL PARTY, CCM.
 
Kwani yeye ni mtendaji wa chama?

Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.

Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.

Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.
watu wazembe sana, wanashindwa kujituma Wacha awabane tu
 
Na kwenye chama bosi wake nani?
Kwenye chama bosi wake mwenyekiti wa mtaa. Kwa ubunge bosi wake chamani ni
Mwenyekiti mkoa .na kwa uwaziri bosi wake mwenyekiti na makamu taifa.mwenezi hawamwiti bosi wanamwita komredi .kazi ya makonda ni kueneza sera za chama ambako hazijafika .kuelimisha zaidi.kulinda taswira ya chama kimikakati.yy anatakiwa akienda mahali kushirikiana na viongozi wa chama eneo husika kimya kimya kuongeza umaarufu wa chama .hata mkuu wa wilaya kuacha ofisi kumpokea mwenezi wa chama sio sawa ile nafasi ya utendaji sio kisiasa.makonda anataliwa apokelewe na chama yy sio kiongozi wa serikali
 
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613

..hata Naibu Waziri Mkuu sio bosi wake.

..hakuna cheo cha Naibu Waziri Mkuu ktk Katiba yetu.

..hili suala lilishafafanuliwa na Mwanasheria Mkuu Andrew Chenge wakati Rais Mwinyi alipomteua Mrema kuwa Naibu Waziri Mkuu.
 
Kuna mambo kwa maneno ni rahisi sana ila kwa vitendo ni ngumu. Kwa katiba iliyopo chama kina nguvu kubwa mno. Huyo Bashe kama waziri ambaye pia ni mbunge akizinguana na chama akafutwa uanachama anapoteza vyeo vyake vya ubunge na uwaziri. Kwa katiba yetu huwezi kuwa waziri bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Hata Rais hawezi kuwa rais bila chama. Kiuhalisia waziri akitunishiana misuli na MWENEZI ataishia kuumia na kulaumu watu. Bashe itakuwa kajiropokea.
 
..unaweza kuwa Waziri bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

..Rais ana nafasi 10 za kuteua wabunge na sio lazima wawe wanachama wa chama chochote cha siasa.

..kwa hiyo anaweza kuteua Waziri asiye na chama kwa kutangulia kumteua kuwa mbunge.
 
Arusha alipigiwa simu kuhusu bei ya sukari na akajibu "nimepokea maagizo" na akaelezea mkakati wa Serikali kutatua uhaba wa sukari Nchini.
Au unamuongelea Bashe mwingine?
 
Bashite anawatisha tisha wajinga wenzie ambao hawajui wanachikifanya maofisini kwao yaani kama mimi tu. Bashe anajitambua - damu nyingine hiyo.
 
..unaweza kuwa Waziri bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

..Rais ana nafasi 10 za kuteua wabunge na sio lazima wawe wanachama wa chama chochote cha siasa.

..kwa hiyo anaweza kuteua Waziri asiye na chama kwa kutangulia kumteua kuwa mbunge.
Tupe mfano wa waziri aliyeteuliwa bila kuwa na Chama hapa Nchini.
 
Back
Top Bottom