Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
ni sahihi kabisa kiutendaji,ila kichama makonda yuko sahihi pia.

anapopiga simu makonda,lengo sio kumuwajibisha waziri,ama afisa husika,lengo ni kuwapa majibu wananchi wanaosikiliza,ambao kimsingi ndio maboss wa awali wa kila mtumishi.

watu wanaleta hisia humu sababu wanamchukia makonda,lakini ile ndio kazi ya mwenezi,ambazo mlichukia sana zikifanywa na viongozi wa mbio za mwenge mkidai hawana staha.
 
..Al Noor Kassum alikuwa hana chama akateuliwa Waziri wa madini na nishati.

..tena hata kuongea Kiswahili alikuwa hawezi.
Ali Noor Kassim aliyezaliwa mwaka 1924 na kufa 2021 alikuwa mwanachama wa TANU na mwanasiasa maarufu wa jamii ya Ismailia.
Aliteuliwa kama katibu mkuu wa kwanza wa Wizara ya Elimu na Habari mwaka 1961 baada tu ya kupata uhuru.
Waziri wa wizara hiyo alikuwa Oscar Kambona. Alishika nyadhifa mbalimbali Serikali na alikuwa anazungumza kiswahili.
Fuatilia usilete tu habari za kuzusha.
 
bashe boss wa polisi toka lini??

anaitwa na anahojiwa vyema kabisa,tofauti yake na mtu mwingine yeye ana dhamana kubwa,hawezi fatwa kibabe abebwe msobe msobe,anaitwa na anaeleza ni wakati gani atafika kuitikia wito.
Anahojiwa kwa utaratibu upi?Wa Magufuri kutokutii sheria za nchi au wa Sheria za nchi yetu?
 
Ali Noor Kassim aliyezaliwa mwaka 1924 na kufa 2021 alikuwa mwanachama wa TANU na mwanasiasa maarufu wa jamii ya Ismailia.
Aliteuliwa kama katibu mkuu wa kwanza wa Wizara ya Elimu na Habari mwaka 1961 baada tu ya kupata uhuru.
Waziri wa wizara hiyo alikuwa Oscar Kambona. Alishika nyadhifa mbalimbali Serikali na alikuwa anazungumza kiswahili.
Fuatilia usilete tu habari za kuzusha.

..hakuwa Tanu.

..na alikuwa hajui kuzungumza kiswahili.
 
..hakuwa Tanu.

..na alikuwa hajui kuzungumza kiswahili.
Utakuwa humjui Al Noor Kassim kwa jina la utani Nick.Umehadithiwa fanya utafiti wacha kubishana tu bila ushahidi.Kama huamini ninachokueleza inga google tafuta ukweli.
 
Kwani yeye ni mtendaji wa chama?

Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.

Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.

Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.
Tanzania ni nchi ya mabwege. Makonda anaogopwa mikoani huko utadhani yuko juu ya Mungu. Kila mtu anamwita ''mheshimiwa''.
 
Back
Top Bottom