Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makonda hana kosa, yuko sahihi kwa kile anachofanya kulingana na nafasi yake, akiwa kama mwenezi wa chama ni jukumu lake kufuatilia utendaji wa mawaziri wa chama chake wanaohusika kuitekeleza ilani yao, na kama hao mawaziri wakiyumba, Makonda lazima awaamshe.

Wengi wanaomponda Makonda wanasukumwa na his past record, na mazoea, lakini hawana hoja thabiti za kusimamia, ni chuki binafsi kwa Makonda, sijui wanataka Makonda akizunguka huko mikoani kufuatilia kero za wananchi awaulize wenyeviti wa mitaa wa CCM kuhusu ukosefu wa sukari!.

Watu lazima mkumbuke, mawaziri ndio wanaohusika kwa kiasi kikubwa kutekeleza ilani ya serikali ya chama chao, Makonda lazima ahangaike nao, hawezi kwenda kwa mwingine yoyote nje ya hao, sio Kinana, wala Nchimbi, hao mambo yao mwisho chamani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwani yeye ni mtendaji wa chama?

Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.

Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.

Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.
Exactly, kama mtu wa chama ana hoja na waziri, aipeleke kwa Samia au PM an Naibu PM ndio/ ndiye atamuita na kumtaka majibu, siyo Makonda
 
Kwani yeye ni mtendaji wa chama?

Bashe yupo sahihi. Mawaziri wote na watendaji wengine wote wa Serikali wanawajibika kwa aliyewateua, na siyo mwingine yeyote.

Chama kama kinaona kuna jambo ambalo halipo sawa, kinatakiwa kimhoji Rais ambaye ni kiongozi wa chama na ndiye msimamizi wa Serikali. Msimamizi wa Serikali, ndiye ana uwezo wa kuwahoji wateule wake na watendaji wote wa Serikali.

Makonda ni mpuuzi. Anawarukia watu ambao hawawajibiki kwake wala kwa chama bali kwa serikali na wakuu wa Serikali.
Chama ni kikubwa kuliko serikali na ndio maana kimekaa madarakani hadi leo.
 
Huyu bwana aliyepandisha Bei ya Sukari ili mabepari wampe rushwa Leo ndo amekuwa shujaa kwenu?

Hii nchi imejaa wapumbavu
Sidhani kama ni busara kutumia neno wapumbavu kwa wanaoonyesha ubovu wa nyumba inayovuja. Bashe haungwi mkono kwa sababu ya ushujaa, ubovu uko kwenye mfumo wa uongozi na utawala uliohodhiwa na CCM, huo ndio unaoleta adha zote hizi za upungufu wa sukari na kupanda kwake.
 
Ni msomi halali ukiona mtu anayumbishwa na kilaza Makonda jua huyo alifoji vyeti.
Na kujiamini ...
Watanzania wengi hatujiamini .. Na uoga sana wa kutumia Mahakama pale unapokandamizwa...Kuna kipindi kama miaka 4 ...Mnyeti akiwa RC akifanya ziara vijijini huko Manyara alimfanyia kituko mkulima mmoja ..

Akaenda kuripoti polisi ..polisi wakamtimua ..akafunga safari Dodoma kwa IGP ..basi yule bwana akapigiwa simu na RC kwenda ofisini kwake na kuyamaliza japo aliambiwa chunga sana....ni wachache wana udhubutu huo
 
..unaweza kuwa Waziri bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

..Rais ana nafasi 10 za kuteua wabunge na sio lazima wawe wanachama wa chama chochote cha siasa.

..kwa hiyo anaweza kuteua Waziri asiye na chama kwa kutangulia kumteua kuwa mbunge.
Kweli kabisa nadhani Angela kairuki, hata prof. Kabudi pia Dr.possi wamekua mawaziri wakiwa wabunge Wa kuteuliwa.
 
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613
Mleta mada unaweza kuwa una Pass kama ulipita chuo kikuu.
Bashe ni serikali wakati Makonda ni Chama.
Swali kwako, kati ya chama na serikari nani boss?
 
Huyo kwanaza ni Msomali, pili ni Muislam mwenye kufata dini yake.

Hkuna Msomali duniani na hakuna Muislam mwenye kuufata Uislam wake akaburuzwa kijinga.
 
Back
Top Bottom