Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anajidai anajua sana, yeye alikuwa mkuu wa wilaya na hatimaye mkoa, alifanya nini?

Yeye hapendi kuulizwa, akiulizwa anaona anapunguziwa madaraka. Anakuwa mkali kweli. Lakini yeye kidimo domo kujifanya yeye ndiye kiranja mkuu kwa wenzake.

Yeye afanye kazi za chama, aongelee ya chama na siyo ya serikali.

Serikali ina msemaji wake. Afanye kazi zake za chama.
 
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613
Labda kama kaandikiwa ila kama kaandika yeye basi hana uwaziri. Makonda anachokifanya siyo kuhoji bali ni kuonesha collective responsibility kichama ili tuonekane kama chama tunamtfutia kura Dkt Samia mwenyekiti wetu na hakuna jambo baya kabisa. Bashe nadhani ndoto yake ya urais inaishia hapo (maana Makonda hayupo hapo ki bahati mbaya).
 
CCM ina viasilia vya kikomunisti hasa vile vya kisovieti.

Kwa vyama vya namna hiyo, makamisaa ambao ni political agitators hawana ukomo wa madaraka na huwajibika kwa KM au M/kiti wa chama tu.

Makonda kama katibu mwenezi ndio kamisaa na mfitini mkuu wa kisiasa(political commissar and agitator) wa CCM.

Mteuliwa yoyote wa serikali inayoongozwa na chama cha namna hii lazima alikubali hili.

Ukimpenda jongoo penda na mti wake.
 
Labda kama kaandikiwa ila kama kaandika yeye basi hana uwaziri. Makonda anachokifanya siyo kuhoji bali ni kuonesha collective responsibility kichama ili tuonekane kama chama tunamtfutia kura Dkt Samia mwenyekiti wetu na hakuna jambo baya kabisa. Bashe nadhani ndoto yake ya urais inaishia hapo (maana Makonda hayupo hapo ki bahati mbaya).
Wacha weeeeee.
 
"Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndiyo wanaweza kuniita na kunihoji, hakuna mtu mwingine yoyote, watu wajue mipaka yao ya kazi," Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

View attachment 2884613
Ukiona waziri yeyote anaepewa maagizo na makonda ni drama na usanii kuhadaa umma.
Watakua washa fanya rehearsal pale jukwaani ni ku perform tu wakinufaika na ubumbuazi wa kiakili wa wengi wa watanzania.
 
Ni sawa na kusema huyo ‘Bi Tozo’ hana jeuri ya kutumbua mtu.

Mawaziri wasaidizi wake wameharibu popularity ya raisi kila kitu kinaenda mrama.

Badala ya kuwatumbua, mama watu kaamua atengeneze sinema yake ya ‘hadaa’ kwa wananchi aonekane anajali. Halafu anatokea mtu anataka kutia kitumbua mchanga na hiyo move yenyewe.

Kwani huyo Makonda ukienda kanda ya ziwa unadhani utakuta kuna hata moja limetekelezwa aliloagiza si wote wanajua sio boss wao ila wanacheza sinema ya ‘bi-tozo’ tu.

Kumvaa Makonda hadharani ni sawa na kuujaribu uvumilivu wa raisi hasa kwa mawaziri walioharibu kama Bashe.

Watch this space
Karma !
 
Anajidai anajua sana, yeye alikuwa mkuu wa wilaya na hatimaye mkoa, alifanya nini?

Yeye hapendi kuulizwa, akiulizwa anaona anapunguziwa madaraka. Anakuwa mkali kweli. Lakini yeye kidimo domo kujifanya yeye ndiye kiranja mkuu kwa wenzake.

Yeye afanye kazi za chama, aongelee ya chama na siyo ya serikali.

Serikali ina msemaji wake. Afanye kazi zake za chama.
Mnara wa Babeli tayari !
Katibu Mkuu anaagiza kingine Mwenezi analeta kingine !!
Ngoja Tusubiri !
 
Anajidai anajua sana, yeye alikuwa mkuu wa wilaya na hatimaye mkoa, alifanya nini?

Yeye hapendi kuulizwa, akiulizwa anaona anapunguziwa madaraka. Anakuwa mkali kweli. Lakini yeye kidimo domo kujifanya yeye ndiye kiranja mkuu kwa wenzake.

Yeye afanye kazi za chama, aongelee ya chama na siyo ya serikali.

Serikali ina msemaji wake. Afanye kazi zake za chama.
Chama kilichounda serikali hii,kwa hiyo chama hicho hakina mamlaka ya kuihoji seriakali yake!?. Ujinga ni mzigo mkubwa sana kichwani.
 
Kwahiyo hawa mawaziri wanataka waharibu tu na waachwe
Wote si ni CCM,acha waulizane.

Makonda kaza hadi mwisho as long as unapigania maslahi ya wanyonge.

Sukari kilo ni elfu5.
 
Kuna clip inatrend mitandaoni ikimuonyesha Waziri wa Kilimo, Mh Hussein Bashe akiongea kwa hasira kuhusu kutoruhusu mtu yeyote kumfanyia lobbying ili aondoe bei elekezi ya sukari iliyowekwa na wazir ihuyo ili kulinda wazalishaji wa sukari na wakulima wa ndani. Bashe amesema mtu anayeweza kumuita na kumhoji ni Rais, VP au PM. Wengine wote waliosalia ni punda tu!

Inasemekana huyo mtu aliyeandaliwa kufanya lobbying si mwingine bali ni katibu mwenezi wa CCM, ndugu Paul Makonda. Habari kutoka ndani ya chama zinapenya kwamba siku mbili zilizopita mwenezi alifanya kikao usiku wa manane jijini Dar es Salaam na wafanyabiashara wa kihindi wanaoagiza sukari kutoka nje na kuazimia Makonda amuite Bashe na kumuonya aondoe bei elekezi kwa sababu bei hiyo sio rafiki kwa wafanyabiashara hao.

Watu walio karibu na Makonda na ambao ni waaminifu kwa Rais Samia, walipozipata taarifa hizi, wakazifikisha kwa Bashe mara moja. Ndipo Bashe alipotoka hadharani na kuweka msimamo wake.

"Urafiki kati ya Makonda na hawa wafanyabiashara ulijengeka wakati Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam ambapo hao wawekezaji wamekuwa wakikichangia chama kwa hali na mali". Alisema mmoja wa wadau wsliohudhuria kikao hicho.

MAONI YANGU
Mimi binafsi naona Makonda yupo sahihi kwa upande mmoja na hayuko sahihi kwa upande mwingine. Yupo sahihi kwa kuwa biashara ya bidhaa za kilimo haiamuriwi na bei elekezi bali nguvu ya soko (demand and supply). Bidhaa zikiwa chache na uhitaji ukawa mkubwa, bei lazima ipande automatically. Na bidhaa zikiwa nyingi sokoni, bei lazima ishuke. Sasa inakuwaje Bashe aweke bei elekezi badala ya kuacha soko liamue?

Kwa namna nyingine, Makonda ana makosa. Wahindi kuchangia CCM hakiwezi kuwa kigezo cha kuingilia maamuzi ya seriakli. Kama alizoea kuchukua hela kwa wahinri wakati akiwa RC, sasa wakati wake umepita. Amuachie Albert Chalamila naye ale. Kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake na kwa wakati wake.
 
Bashe kaniangusha hahahaha inasemekana kaandika hayo uko x lakini leo hii kapigiwa Simu na Makonda kaulizwa maswali na kajibu vizuri na kuahidi kusimamia maekekezo ya chama.

Hahaha kweli za kuambiwa changanya na zako…Jamani mihemko ya uko x angalieni isije kuwapotezea vibarua vyenu
Angeendelea kukaza fuvu lake[emoji1787]
 
Back
Top Bottom