Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Pre GE2025 Waziri Bashe: Wenye mamlaka ya kuniita na kunihoji kwenye nchi hii wapo wanne tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Baadhi ya anayoyafanya ni mazuri hasa kwa wale ambao hawana sauti na kupata kutatuliwa kwa kero zao, swali ni moja tu ana mamlaka gani ya kushurtisha mamlaka nyingine zisizofungamana na chama kufanya anavyotaka yeye.

Yeye mamlaka yake hayavuki nje ya chama sasa inakuwaje anakuwa na nguvu ya kutoa hukumu kwa mamlaka nyingine na wao wakatii?

Kuendelea kumtii matamko yake kunatengeneza delusional power kwa muhusika kuhisi ana nguvu kubwa mno. Makonda ni mtu wa mihemko na mpenda sifa, wasipomdhibiti mapema atakuja kuingilia mpaka mamlaka ya aliemteua. Kwa sasa keshaanza kujihisi kuwa na yeye ni raisi.
Niliuliza hili kwenye uzi mwingine.
 
Bashe kaniangusha hahahaha inasemekana kaandika hayo uko x lakini leo hii kapigiwa Simu na Makonda kaulizwa maswali na kajibu vizuri na kuahidi kusimamia maekekezo ya chama.

Hahaha kweli za kuambiwa changanya na zako…Jamani mihemko ya uko x angalieni isije kuwapotezea vibarua vyenu
Tunasubiri Nape Nnauye naye apigiwe simu, tuone maigizo.
 
Kuna clip inatrend mitandaoni ikimuonyesha Waziri wa Kilimo, Mh Hussein Bashe akiongea kwa hasira kuhusu kutoruhusu mtu yeyote kumfanyia lobbying ili aondoe bei elekezi ya sukari iliyowekwa na wazir ihuyo ili kulinda wazalishaji wa sukari na wakulima wa ndani. Bashe amesema mtu anayeweza kumuita na kumhoji ni Rais, VP au PM. Wengine wote waliosalia ni punda tu!

Inasemekana huyo mtu aliyeandaliwa kufanya lobbying si mwingine bali ni katibu mwenezi wa CCM, ndugu Paul Makonda. Habari kutoka ndani ya chama zinapenya kwamba siku mbili zilizopita mwenezi alifanya kikao usiku wa manane jijini Dar es Salaam na wafanyabiashara wa kihindi wanaoagiza sukari kutoka nje na kuazimia Makonda amuite Bashe na kumuonya aondoe bei elekezi kwa sababu bei hiyo sio rafiki kwa wafanyabiashara hao.

Watu walio karibu na Makonda na ambao ni waaminifu kwa Rais Samia, walipozipata taarifa hizi, wakazifikisha kwa Bashe mara moja. Ndipo Bashe alipotoka hadharani na kuweka msimamo wake.

"Urafiki kati ya Makonda na hawa wafanyabiashara ulijengeka wakati Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam ambapo hao wawekezaji wamekuwa wakikichangia chama kwa hali na mali". Alisema mmoja wa wadau wsliohudhuria kikao hicho.

MAONI YANGU
Mimi binafsi naona Makonda yupo sahihi kwa upande mmoja na hayuko sahihi kwa upande mwingine. Yupo sahihi kwa kuwa biashara ya bidhaa za kilimo haiamuriwi na bei elekezi bali nguvu ya soko (demand and supply). Bidhaa zikiwa chache na uhitaji ukawa mkubwa, bei lazima ipande automatically. Na bidhaa zikiwa nyingi sokoni, bei lazima ishuke. Sasa inakuwaje Bashe aweke bei elekezi badala ya kuacha soko liamue?

Kwa namna nyingine, Makonda ana makosa. Wahindi kuchangia CCM hakiwezi kuwa kigezo cha kuingilia maamuzi ya seriakli. Kama alizoea kuchukua hela kwa wahinri wakati akiwa RC, sasa wakati wake umepita. Amuachie Albert Chalamila naye ale. Kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake na kwa wakati wake.
Ikiwa huo ndo UKWELI,

Mwenezi anamhujumu Sa100 nyuma ya pazia.
 
IMG-20240128-WA0037.jpg
IMG-20240128-WA0036.jpg
 
🤔🤣🤣🤣🤣🤣 wakigombana chukua jembe ukalime…
Mfano katika hili suala ambalo Bashe analalamikiwa kuwa mabwana shamba wamejigeuza watoza ushuru.

Je lina ukweli wowote?
Yeye Bashe analifahamu hilo?
 
Back
Top Bottom