#COVID19 Waziri Dorothy Gwajima: "Mume wangu ametest mitambo, kakuta Niko fiti"

#COVID19 Waziri Dorothy Gwajima: "Mume wangu ametest mitambo, kakuta Niko fiti"

Hadi leo nashindwaga kuelewa aina hii ya waziri alipewaje, yawezekana ana tu za darasani za kukariri ama kufanya hesabu lakini kiukweli huyu mama ana matatizo ya kiakili
tatizo lake liko wapi?...ufinyu wenu wa kuelewa na kupambanua mambo ndio unawafanya mhitimishe hivyo
 
Hakuna kitu kama hicho,japo mimi bado ila nitachanja kabla wiki haijaisha,nawasihi chanjeni kipindi hiki ambacho kuchanja ni bure kuna kipindi utajuta kama hukuchanja, halafu una jambo haliwezi kwenda mpk uwe na kadi ya kuchanja uviko19...Dunia ndo ishabadilika mkuu huna ujanja wa kwenda tofauti na wakulungwa.

Hisia zako tu
Chanjo itabaki kuwa hiyali
Na sioni sababu ya kuipigia promo chanjo.

Unajohofia nenda uchanje
Umaaona chanjo ni upuuzi acha kuchanja.
 
Wanaume wengine mnasemaje? Mbona hamleti mrejesho? Maana yasemekana mitambo huwa inaharibika baada ya chanjo.

IMG-20210818-WA0002.jpg
 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amesema baada ya kuchanja chanjo ya COVID-19, mume wake ametesti 'mitambo' kwake na kukuta yupo 'fiti'.

Ametoa kauli hivyo leo Agosti 18, 2021 jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou Toure.

Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndiyo maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanja chanjo hiyo.
 
Back
Top Bottom