Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Na ni yeye Mwinyi ambae hakuwa muungwana.

Alitaka waziri afanyeje, amtunzie mirunda na mi kokoto yake mbele ya nyumba ya Waziri?

Au waziri asinunue vya kwake kwa sababu hakuna nafasi ya kuvitunza nyumbani kwake ?

Na kama mtu umemwona ni mdhulumati kwa nini umempa uwaziri, ili atuibie ?

Wana bahati sana wanaandika vitabu vya gibberish kama hizi huku Afrika ambako hakuna audience ya kuchambua pumba na michele wanayoisema
Uungwana nyie uzao wa Kaini hamuwezi kuwa nao lakini kama mtu katolewa ghafla unamuambia toka basi vitu vyake muachie usimpore

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nakumbuka ile Mihadhara ya Dini mbalimbali pale kwenye Bustani za Mnazi Mmoja ilikuwa ni Burdani ya kujifunza Imani mbalimbali

Ilifikia wakati tukawa hatuwaogopi tena Wehu kwa kuwadhani ni Maafsa Usalama wa Taifa

Alhaji Alli Hassan Mwinyi alikuwa ni Kiongozi na si Mtawala
 
Na ni yeye Mwinyi ambae hakuwa muungwana.

Alitaka waziri afanyeje, amtunzie mirunda na mi kokoto yake mbele ya nyumba ya Waziri?

Au waziri asinunue vya kwake kwa sababu hakuna nafasi ya kuvitunza nyumbani kwake ?

Na kama mtu umemwona ni mdhulumati kwa nini umempa uwaziri, ili atuibie ?

Wana bahati sana wanaandika vitabu vya gibberish kama hizi huku Afrika ambako hakuna audience ya kuchambua pumba na michele wanayoisema
Mwinyi alikuwa na bado no muungwana. Mwinyi alijiuzulu na akachaguliwa waziri mwengine mpaka wakati huo alikuwa na saruji mifuko 100 na bati 150 (si mirunda na kokoto ka.a unavyodai) hivyo alipopata pa kuviweka alirudi kuvichukua na akazuiwa, sasa hapo yeye amekosa uungwana gani ? Natepe kumganyia visa mwinyi, si kwamba aliifanyia Tanzania nzima, hakufanya mahusiano yao binafsi yaathiri manufaa jamuhuri ingepata kwa utumishi wake na hiyo ilikuwa sehemu ya kiapo chake.
 
Wanasiasa wajifunze kwa mzee Ali Hassan Mwinyi, kuwa usitumie madaraka na mamlaka vibaya hasahasa ukiwa mkubwa kimadaraka. Kumbuka utahukumiwa na historia..

Toka Maktaba :

3 Sept 2016
Alichokizungumza Rais Magufuli kuhusu Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein

Magufuli amshauri Dr. Mohamed Shein asisaini mafao ya ustaafu ya Maalim Seif Hamad

’Kama mtu anaukataa mkono wako na wewe kataa mkono wako kufanya mambo yake, ajifunze ajue mkono wako una thamani, haiwezekani mbele ya watu unatoa mkono anaukataa halafu unatoka kwenda ofisini unasema unasaini hapa hela ya huyu kwenda kutibiwa’:-JPM
 
Mwinyi alikuwa na bado no muungwana. Mwinyi alijiuzulu na akachaguliwa waziri mwengine mpaka wakati huo alikuwa na saruji mifuko 100 na bati 150 (si mirunda na kokoto ka.a unavyodai) hivyo alipopata pa kuviweka alirudi kuvichukua na akazuiwa, sasa hapo yeye amekosa uungwana gani ?
Alirudi kuvichukua baada ya muda gani ?

Hii ni hadithi ya upande mmoja, hujui Waziri alihangaika vipi kumsihi aje kuchukua mabati yake yenye kutu na tetanus hatari kwa watoto wa waziri.

Na Mwinyi mwenyewe kasema sasa hivi kapoteza kumbukumbu, ikifika mchana hajui asubuhi aliamkia wapi. Sasa unaandika leo kitabu cha miaka 40 iliyopita, unakumbukaje Waziri alivyohangaika kukutafuta?

Mwinyi hakuwa muungawana.
 
Katika kitabu cha kuelezea maisha yake mstaafu Mwinyi anasema alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani Waziri aliyechukua nafasi yake alimtaka ahamishe haraka mizigo yake ili yeye ahamie kwenye nyumba ya serikali aliyokuwa anakaa mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi alishindwa kuhamisha vifaa vyake vya ujenzi wa nyumba yake ya mikocheni kwa mwalimu, yule waziri akamdhulumu.

Pamoja na ubazazi na udhulmati wa waziri huyo lakini mzee Mwinyi alipochaguliwa kuwa Rais wa JMT alimchukua waziri huyo kwenye baraza lake la mawaziri.

Waziri huyo ni nani?

Wahenga Pascal Mayalla, Mohamed Saidi na Mrangi nikumbusheni!

Kazi Iendelee.
Leo MATAGA mnasema CCM hajaanza udhulumati leo? Ama kweli hujafa hujaumbika
 
Alirudi kuvichukua baada ya muda gani ?

Hii ni hadithi ya upande mmoja, hujui Waziri alihangaika vipi kumsihi aje kuchukua mabati yake yenye kutu na tetanus hatari kwa watoto wa waziri.

Na Mwinyi mwenyewe kasema sasa hivi kapoteza kumbukumbu, ikifika mchana hajui asubuhi aliamkia wapi. Sasa unaandika leo kitabu cha miaka 40 iliyopita, unakumbukaje Waziri alivyohangaika kukutafuta?

Mwinyi hakuwa muungawana.
Habari hii ni ngeni kwako, lakini si kwa kila mtu. Hujui lakini ilikuwa 'stori' iliyovuma wakati fulani. Hata hivyo wewe usiyejua mwinyi alielezwa kwa muda gani akachukue vitu vyake, na kuwa ni stori ya upande mmoja, unasemaje Mwinyi si muungwana kwa kusikia upande huo huo mmoja ?
 
Kutokana na yaliyo andikwa kwenye Kitabu chake Mzee Mwinhi, inaomekana katika Marais walio pata taabu sana ktk uongozi kuanzia alipo teuliwa kuwa waziri basi ni Huyu Mzee wetu Mwinyi.

Pamoja na kuwa mwadilifu na mtiifu lkn bado alichukiwa sana na alifanyiwa fitina za hali ya juu mpaka akajiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani lkn badae alirudishwa tena ulingoni lkn bado alipigwa fitina na kubabaishwa kuwa eti ni mdini anapendelea waislamu n.k, ama hakika walimyumbisha sana lkn kutokana na uadilifu wake na ucha Mungu alibakia kuwa Imara na Hatimaye Mungu alimsaidia.

Hakika kuna mafunzo mengi sana ya kujifunza ktk kipindi cha utawala wake.

tujirekebishe kwa wale wote wenye chuki binafsi na uchu wa vyeo, tuache tabia za kuiguruga nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli.

tuache kutafuta vyeo kwa uchawi au kwa kuhadaa/unafiki kwani cheo/uongozi hutoka kwa Mungu.

Tusibaguane wala kuchukiana au kufanyiana fitina kisa ni mkristo au mwislamu, sisi sote walio na dini na wasio na dini tunaunganishwa na MAMA Tanzania.

tusibaguane kwa makabila au ukanda kwani sisi sote ni watanzania, hivyo yatupasa kudumisha Amani, Upendo na Utulivu kwa masilahi ya nchi yetu.
 
hivi viongozi wenye roho mbaya ktk dunia hii bado wapo? kwa hapa kwetu Tz
 
Uungwana nyie uzao wa Kaini hamuwezi kuwa nao lakini kama mtu katolewa ghafla unamuambia toka basi vitu vyake muachie usimpore

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Hakutolewa ghafla, alijiuzuru mwenyewe na alijua anatakiwa ahame na mazaga zaga yake yote.

Mwinyi hujitanabaisha kama muungwana. Waswahili wanasema "mwenye chake muungwana."

Mtu akikufukuza kwake wewe na mali zako, ni yeye ndio muungwana, kwa sababu ana chake na ana kwake, hasumbui mtu kumtunza au kumtunzia, wewe king'ang'anizi ndio umekosa chako na huna kwako na huna uungwana! Mwinyi alikosa uungwana.
 
Back
Top Bottom