Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,160
- 9,151
..but this is petty.
..hivi kulikuwa na haja ya kuandika haya kwenye kitabu chake?
Inawezekana ndio yaliyomuumiza sana ndani ya maisha yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
..but this is petty.
..hivi kulikuwa na haja ya kuandika haya kwenye kitabu chake?
Kwani wewe hakuna kitu umejifunza hapo??
kuna mambo mengi sana Mzee mwinyi ameyaandika katika kitabu chake. ni vyema ukapata nakala yako ukajisomea kwa undani zaidi.
Lkn kwa mujibu wa muhtasari ulio somwa na Prof. Mkandala ni kwamba Mzee Riuksa ktk safari yake ya maisha ya uongozi amekumbana na changamoto nyingi sana tena panda kichwa, mfano;
1. changamoto za kibaguzi kuhusu dini yake, kuhu asili yake.
2. changamoto za kiuchumi, baada ya kupokea kijiti kutoka kwa Hayati mwalimu JK alikuta hali ya kiuchumi ni mbaya sana isiyo elezeka, alifanya jitihada za kuifungua nchi na mambo yakaanza kuwa mazuri lkn aliaanza kupigwa fitina kali kuwa amekumbatia ubeberu badala ya ujamaa , n.k,
alipata changamoto ya uchochezi wa kidini ambao ulisimamiwa na kuenezwa na Rev.Mtikila ambaye kwa maksudi na chuki alieneza chuki za kidini ambayo ilimpa taabu sana mzee Ruksa kuendesha nchi.
ilichochewa Migomo ya wanafunzi na maandamano n.k n.k
Alifanyiwa figisu na fitina mpaka aliamua kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani n.k.
alipigwa fitina na Jungu mpaka akashindwa kuwa mwenyekiti wa CCM taifa.
n.k nk.
Kama mambo haya bado yapo ni bora tuyaache mara moja kwani haya tija kwa taifa letu. lkn pia ni vyema viongozi wetu wakafahamu ni wapi walikosea mpaka hali hii ikakomaa, inaonekana kuna tatizo mahala, nalo linafaa lirekebishwe ili kunusuru umoja wa taifa letu.
Jackson Mvangila MakwetaMzee ana roho nyeupe ndio maana ameishi miaka mingi, he is 96 today.
Ni mzanzibari hivi. Jina limenitoka
Late Major General Abdalah Natepe
Hassan Nassoro Moyo
Alikuwa Lowassa. Nadhani na yeye atakuja kujibu akitoa kitabu chake mwaka mmoja kabla hjasafiri!
Au ni Ameir?
Hassan nasoro Moyo.
Ahsante sana bwashee!
Jackson M MakwetaAlikuwa Hassan Nasoro Moyo
Huyu hajakisoma kitabu, ni mambo ya kuambiwa huku alikuwa hasikilizi vizuriUmesoma kitabu chake chote? Wapi alisema alibaguliwa dini yake?
Anaitwa Abdalla Said NatepeNi mzanzibari hivi. Jina limenitoka
Kufuga mwizi?Mzee ana roho nyeupe ndio maana ameishi miaka mingi, he is 96 today.
Abdalah Said Natepe, tena Mzanzibari mwenzie!!!Katika kitabu cha kuelezea maisha yake mstaafu Mwinyi anasema alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani Waziri aliyechukua nafasi yake alimtaka ahamishe haraka mizigo yake ili yeye ahamie kwenye nyumba ya serikali aliyokuwa anakaa mzee Mwinyi.
Mzee Mwinyi alishindwa kuhamisha vifaa vyake vya ujenzi wa nyumba yake ya mikocheni kwa mwalimu, yule waziri akamdhulumu.
Pamoja na ubazazi na udhulmati wa waziri huyo lakini mzee Mwinyi alipochaguliwa kuwa Rais wa JMT alimchukua waziri huyo kwenye baraza lake la mawaziri.
Waziri huyo ni nani?
Wahenga Pascal Mayalla, Mohamed Saidi na Mrangi nikumbusheni!
Kazi Iendelee.
Mbona hayo yalishawahi kuandikwa humu kitambo! Pia kama unasema yalipata kutu kwanini baada ya mwinyi kuwa raisi alimpelekea vile vitu? Kumbuka jamaa alimnyima mwinyi akimwambia ni mali ya serikaliAlirudi kuvichukua baada ya muda gani ?
Hii ni hadithi ya upande mmoja, hujui Waziri alihangaika vipi kumsihi aje kuchukua mabati yake yenye kutu na tetanus hatari kwa watoto wa waziri.
Na Mwinyi mwenyewe kasema sasa hivi kapoteza kumbukumbu, ikifika mchana hajui asubuhi aliamkia wapi. Sasa unaandika leo kitabu cha miaka 40 iliyopita, unakumbukaje Waziri alivyohangaika kukutafuta?
Mwinyi hakuwa muungawana.
Kuna mdau kaandika mahali mambo fulani nimeyakopi kama yalivyo hapo chini.Hakutolewa ghafla, alijiuzuru mwenyewe na alijua anatakiwa ahame na mazaga zaga yake yote.
Mwinyi hujitanabaisha kama muungwana. Waswahili wanasema "mwenye chake muungwana."
Mtu akikufukuza kwake wewe na mali zako, ni yeye ndio muungwana, kwa sababu ana chake na ana kwake, hasumbui mtu kumtunza au kumtunzia, wewe king'ang'anizi ndio umekosa chako na huna kwako na huna uungwana! Mwinyi alikosa uungwana.
Alimnyima vitu vyake kivipiii ??Mbona hayo yalishawahi kuandikwa humu kitambo! Pia kama unasema yalipata kutu kwanini baada ya mwinyi kuwa raisi alimpelekea vile vitu? Kumbuka jamaa alimnyima mwinyi akimwambia ni mali ya serikali
Haya mambo yanajulikana zaidi ya miongo miwili iliyopita, hivyo kumbukumbu unayotaka kusema haipo sasa ilikuwepo.Alirudi kuvichukua baada ya muda gani ?
Hii ni hadithi ya upande mmoja, hujui Waziri alihangaika vipi kumsihi aje kuchukua mabati yake yenye kutu na tetanus hatari kwa watoto wa waziri.
Na Mwinyi mwenyewe kasema sasa hivi kapoteza kumbukumbu, ikifika mchana hajui asubuhi aliamkia wapi. Sasa unaandika leo kitabu cha miaka 40 iliyopita, unakumbukaje Waziri alivyohangaika kukutafuta?
Mwinyi hakuwa muungawana.
Jackson kama ulivyoeleza ni kweli alileta maendeleo huko kwenu na unaweza kusema alikuwa kiongozi mzuri pure technocrat na sio mwana siasa , lakini hili suala la yeye kutaka nyumba kwa haraka na kuchukua hivyo vifaa linafahamika zaidi ya miaka 20 iliyopitaKuna mdau kaandika mahali mambo fulani nimeyakopi kama yalivyo hapo chini.
Mmmh!
Ukikosa ku-peruse ukurasa wako wa mtandao kwa saa 12 tu,unakuwa umeachwa nyuma masafa.
Sikuwapo hewani kwa saa 36 hv,usiku huu napitia group hili,nayaokoteza mengi.
Hili la Mhe.J.M.Makwetta,limenigusa.
Asante kwa analysis hii ndg yetu.
Nami niseme tu,nilimfahamu Jackson (Mungu airehemu roho yake) enzi anasoma sekondari A level-1960s,nikiwa nasoma Lupembe Primary School.
Aliwahi kuwa anakuja kutufundisha darasani kwa wakubwa wetu madarasa ya V,VI&VII,anapokuwa likizo.
Lakini kwangu na kwetu wa familia za Aron B.Swalle,Mzee Francis M.Hongoli Lupembe,Mzee Godfrey M.Hongoli Lupembe - Jackson alikuwaga mgeni wetu mara nyingi.
Alikuwa akija kuonana na wazee wale mara kadhaa,hasa akiwa masomoni Chuo kikuu na alipoanza kufundisha IDM Mzumbe.
Ikumbukwe,Jackson alikuwa shemeji yake Mzee Francis kwa Shangazi Munyawvolofu,hivyo automatically kuwa ndg wa akina Hongoli na uzao wao.
Lkn pia,Jackson alikuwa rafiki,wa kiwango tofauti cha ukaribu na wasomi wa mwanzo wa Kanikelele akina:August P.Mpolo,Metusala S.Sasami,John A.B.Swalle (Nyalusi).
The man was humble ambaye alikuja kuwa model wangu.
Jamani,niliwahi kudokeza huko nyuma kuwa,
KWA CHOCHOTE KITAKACHOSEMWA JUU YA HISTORIA YA LUPEMBE aka KWAVISU,JOHN AaRON MHAVILE aka MUNYILEMBULA aka Baba Joyce,na
JACKSON M.MAKWETTA aka Munyamtwango, ni wabunge wa kupigiwa mfano.
One can write volumes kuwahusu wanasiasa hao.
Time will tell.Tuombe Mungu.
Mhavile alijenga uchumi na misingi ya elimu kwa kujenga misingi ya ushirika (akiwa ameazimwa na wazee akina Mbanga,purposely kwa kazi hiyo,maana alikuwa msomi wa Std.X)
Lupembe Farmers' Cooperative Union,kika-boost kilimo cha Pareto,Kahawa na Chai.
I can humbly argue here kwamba TURNING POINT YA MAENDELEO YA KWAVISU,NI PARETO,KAHAWA,NA CHAI.
Baadae Chai,ilileta HYBRID 614,i.e.In stand to be corrected,zao lililotutoa kutoka kutegemea wvuledzi,mayao na sweda kwa chakula,kuwa A FOOD SECURED LUPEMBE.
Jackson alikuja kuanzia alipokuwa ameishia Mhavile.
Akipokea kijiti toka kwa Mwl.Sapali,Jackson alianza na ELIMU.
Aliiga approach ya wenzetu wa Kilimanjaro kwa kuunganisha nguvu za wananchi na kwa kutumia NDDT,tukaanza kujenga sekondari kwenye kila tarafa.
Ikumbukwe kuwa,ni Makwetta,aliyemwambukiza J.J.Mungai,wazo la sekondari za jamii nae akajiongeza kwa kujenga shule za kata kwa kupitia MET kule Mufindi.
Mchokozi hapa,nitofautiane na hoja na:4.
Pamoja kwamba Jackson Makwetta alimfundisha Anne Semamba Makinda kule IDM,
Njia ya Anne kiutumishi hasa ktk siasa,haikumtemea Jackson.
Jackson hakuwa mwanasiasa in the real meaning of it.
Jackson was purely academic,professional and pragmatic technocratic.
Aliingia ktk ulingo wa siasa,just by virtue kwamba mfumo wetu wa utawala unatulazimisha tutumie ulingo wa siasa kufikia malengo ya kuingia kwenye timu za kuongoza wengine.
Ikumbukwe,Anne aliingia ktk siasa,akiwa kiongozi wa kitaifa wa TYL,tangu akiwa chuoni IDM Mzumbe.
Na waliingia bungeni pamoja na Jackson mwaka 1975,Anne akiwa anatokea TYL.
i.e.kwa msiofahamu TYL ni TANU YOUTH LEAGUE,sawa kwa mbaali na UV-CcM.
Wkt Jackson hakuwa kuwa kwenye top-clique ya Chama,Anne ameogelea humo tangu akiwa kinda mwali.
Anne ni mjumbe wa NEC-CcM, hata kabla ya Mzee Mkapa (RiP) na Dr.Kikwete.
Hata Mzee Rukhsa nadhani.
Nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu wa chama 1982 tukiwa pale Diamond Jubilee,BwM aliangukia pua kuingia NEC,Anne na JK walipeta kupitia UVCcM.
Halikadhalika kwenye MM wa kihistoria wa CcM kule Kizota 1987,Mzee Mkapa aliambulia patupu ktk kinyang'anyiro kuwa m-NEC,Anne aliibuka kidedea.
JK (akigombea kwa mara ya kwanza kupitia Kapu Kuu) aliibuka mshindi wa tatu,nyuma ya Kingunge na Nnauye Moses - vinara wa propaganda hao.
Miaka yote ya utumishi wake Jackson M.Makwetta,hakuwahi kutafuta durectly nafasi ya uongozi ktk chama.
Ninakaribia kuhitisha kuisoma Biography ya Mzee Rukhsa.
Waliomshauri aingize hiyo sintofahamu yake kwa Jackson,wamebughi.
Sawa,ameandika hilo ili kuonesha kuwa yeye si mtu wa visasi.
Ila wewe binafsi jiulize na kujijibu ktk moyo na roho yako,
NAFSI YAKO HAINA ELEMENT ZA KISASI KABISAAAAAA?
Kama ni HAPANA,hizo elements chache ulizo nazo,(i.e.jambo ambalo si dhambi maana umelipokea kwa uumbaji) HUWA UNAZITUMIAJE NA KWA NANI?
Ni bahati mbaya,Jackson hawezi kuinuka amjibu Mzee Rukhsa,naamini hata angeweza,the best he could have done Jackson niliyemfahamu,angemnyamazia.
Zaidi zaidi hata Mzee Rukhsa na waliomsaidia kuiandaa bio yake wasingeliingiza kumbukumbu hiyo kabisa.
In short,Mzee Rukhsa alilipiza kisasi kwa Jackson.
Again,TIME WILL TELL.
Ndugu zangu,kwa tuliomfahamu Marehemu Jackson M.Makwetta,hicho tunasoma kwenye bio ya Mzee Rukhsa kumhusu,HAKITUSHANGAZI.
Jackson was PURELY HUMBLE,FIRM N A FACTUAL TRUTH-TELLER.
Jackson alikuwa muwazi na asiyepindisha wala kukawiza jambo.Ndio kisa akawa kipenzi cha mabosi wake kuanzia:Sokoine 1977,Msuya,Salimu,Warioba,Malecela na Msuya tena.
Unapaswa uwe ulimfahamu ama kwa kufanya naye kazi au hata kwa kusimuliwa tu na waliokuwa naye karibu,ndio unielewe nisemacho.
Historia ya Mzee Mwinyi kuingia ikulu,ilijaa makandokando,hata kama hayalingani,kama tuliyoshuhudia kwa safari za wengine pia.
Asituaminishe kuwa alipita njia nyoofu na nyororo.
Yapo mengi under-cover ya kutosha volumes zingine hata tano usawa wa bio hii.
Surfice by saying,HISTORIA NI ZANA MUHIMU KWA KILA MWENYE NIA NA MALENGO THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU YAKE NA YA JAMII YAKE.
To me JACKSON M.MAKWETTA STANDS TO BE ONE AMONGST MY BEST MODELS.
MUNGU AIREHEMU ROHO YA MPENDWA JMM.
Ahsanteni sana.
Credit kwa Gideon Swale (Kiwopambuli
Okay, aliyasema 20 years ago. With fresh memory and faculties.Haya mambo yanajulikana zaidi ya miongo miwili iliyopita, hivyo kumbukumbu unayotaka kusema haipo sasa ilikuwepo.
Kwa hisani kubwa kabisa ya Jamiiforums tarehe 23 Julai 2019
: Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83? kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa mzee Abdallah Said Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Meja Jenerali Abdallah Said Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.
Ilikuwa shida kidogo maana waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Meja Jenerali Natepe.
Ikampasa mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serikali.
Mzee Abdallah Said Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee Ali Hassan Mwinyi akaviacha akaondoka.
Baada ya miezi kadhaa tu mzee Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Mzee Abdallah Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee Ali Hassan Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapa sasa Mzee Meja jenerali Abdallah Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee Ali Hassan Mwinyi.
Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Abdallah Said Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.
Siku ya kumuapisha akamwambia mzee Abdallah Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.
Siku moja mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu Mh. Ali Hassan Mwinyi rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??
Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe, mzee Ali Hassan Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
N.B
Habari za ziada kwa hisani ya intaneti
Sunday, September 26, 2010
MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR ABDALLA SAID NATEPE AMEFARIKI DUNIA
Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.
Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.
“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.
Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.
Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.
“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.
“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”
MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR SAID ABDALLA NATEPE AMEFARIKI DUNIA
Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajes...zenjfm.blogspot.com
It is not petty. Anataka wanasiasa vijana wajifunze kujishusha na kutolipiza visasi...but this is petty.
..hivi kulikuwa na haja ya kuandika haya kwenye kitabu chake?