Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Hivi akili yako ipo sawa?? Huja soma kwamba ali pata msukumumo wa kutakiwa kuondoka ili yeye aingie kwenye hiyo nyumba , Na arudi kwao ZnZ .
Na huja soma baadae muhusika alimpelekea mabati na cement alivyokuwa "white house"
Alipata, sio "ali pata."
Hujasoma, sio "huja soma."

Kuandika kwenyewe hujui halafu unaniuliza mimi kama akili zangu ziko sawa.

Pia Tanzania hakuna "white house," kuna State House.

Huwezi hata kuandika maneno ya Kiswahili, umesoma shule wapi wewe ?

Mwinyi hakupewa msukumo wa kuondoka, alijiuzulu mwenyewe kwa siku aliyopanga mwenyewe. Huwezi kuacha kazi halafu ukabaki kwenye nyumba.

Alijua anaondoka, akaacha eneo limezagaa building material utadhani construction site, alikosa uungwana. Mwenye chake muungwana.
 
Kitabu kinasema "Baada ya Mzee Mwinyi kuchaguliwa Rais alimteua huyo bwana aliyemdhulumu vifaa vyake vya ujenzi na kumtoa kwenye nyumba.."

Msingi wa hoja yangu upo hapa
siyo rahisi kukubali uteuzi ki ivo wewe!!. Huyo waziri hana ubongo au!!!

Nasema. hakujua kabisa kosa lake huyo hata usipomsamehe mbinguni anaenda. Angejua ile dhambi ingemtesa sana tu!! lazima.km angejua amezulumu.

Aliona labda ni matofali ya sirikali sababu Mwinyi hakumlalamikia wala kuyadai.ayafanyeje sasa.

Au alimwekea mtego kisiri kuwa amemnyanyapaa?? Hiyo sasa ni mwinyi. hata ka Mungu haikubaliki.

Laiti angefanya maksudi asingekubali uteuzi piga ua.

Atakuamini vipi? Atadhani unataka kulipiza ki aina.

Mtu akikufanyia ubaya maksudi na akajua kuwa umejua lkn umempotezea tu kirahisi Na unauwezo wa kumfanya chochote anaweza kufa ghafla kwa kihoro......narudia.....

Bora mtu umseme!! urushe ngumi kidogo!!matusi. atajua haya...yameisha...lkn ukipiga kimya weeee!!thubutuuuuuu
 
It is not petty. Anataka wanasiasa vijana wajifunze kujishusha na kutolipiza visasi.

Kumbuka kuwa alipokuwa rais alikuwa anamuapisha huyo huyo aliyemfanyia unyama akiwa amesimama mbele yake akiahidi utii kwa rais.

Ni lazima huyo aliyefanya ubaya alikuwa na unyonge mwingi wakati wa kiapo na wakati wa kupokea maagizo.

Wanasiasa wengi wa afrika hawana uwezo wa kujishusha, wanajawa na kile kiburi cha elimu kinachochanganyika na ushauri mbovu wa wapambe wanaoshauri ubaya ufanyike ili waendelee kuutunza ukaribu wao na bosi wa nchi.

..unadhani Mzee Mwinyi angekuwa kapuku angekuwa anazungumza lugha ya kusamehe, au angekuwa analilia mabati, misumari, na mifuko yake ya saruji iliyoharibika wakati anahamishwa?

..hili suala la kusamehe nadhani linaendana na nafasi ya mtu aliyofikia. kwa mfano, siamini kama Mzee Mandela angewasamehe makaburu kama asingekuwa Raisi. Naamini kitendo cha kuwa Raisi kilimpunguzia machungu Mzee Mandela, na kumtemesha nyongo ya kisasi aliyokuwa nayo gerezani.
 
Alikufa akiwa maskini kabisa na yeye alizulumiwa na wajanja wa njombe huko na uchagani
Mzee makwetta alikuwa na roho mbaya sana. Huwezi amini alipokuwa waziri wa elimu aliwanyima scholarship watu wa kwao, akiwaza kuwa wakienda kusoma nje wakirudi watampindua ubunge. Watu wa kwao hawataki hata kumsikia
 
Umekuwa mwepesi sana kutoa hukumu kwa vile labda ulikuwa hujazaliwa kipindi hicho. Mzee Mwinyi alipokea nchi hii ikiwa hoiiii bin taaban! Yaani aliachiwa fremu tu ya nchi. Hata ukitaka sabuni ya mawingu ya kufulia ilikuwa lazima upange foleni, kwa waliokuwa vijijini ile mifuko ya kitambaa (kikiitwa Marekani) iliyokuwa ikija na mchele na unga ndiyo mavazi, redio ya mkulima ndiyo ilikuwa ya maana, eti kuwa na televisheni au friji ulikuwa mlanguzi, heeeee!

Umewahi kuisikia 'redio kiroboto' iliyokuwa ikieleza kwa kificho jinsi nchi ilivyokuwa ikipata shida kwa kukosa mahitaji muhimu? Mbali ya kutukanwa na kushambuliwa na Nyerere na wengine hadharani Mzee Mwinyi alikuwa mvumilivu na hakuwahi kumjibu hata siku moja.

Umewahi kusikia vijana waliowahi kuteka nyara ndege ili angalau kujikwamua katika hali ngumu iliyokuwepo? Wale walikuwa desperate yaani (siyo kwamba naona ni vyema). Ilikuwa safari nje ya nchi lazima upate kibali cha Ikulu na Income tax ndiyo upatiwe tiketi.

Mzee Mwinyi hii nchi aliitoa mbali sana ambao nyinyi kwa sasa munaona ni vitu vya kawaida. Yeye kama binaadamu hakuwa mkamilifu na alifanya makosa kadhaa lakini kwa kweli aliyofanya mema ni mengi kuliko hayo mapungufu.

Lakini sisi binaadamu hatuna shukurani hata tukifanyiwa wema vipi bado baya moja litakuwa na nguvu zaidi kuliko yale mengine.
Ukiona mtu anajenga hoja kwa kuegemea umri wake ama kujisifia taaluma yake ujue ni mtupu katika hoja.
Ninyi vibinti vya themanini mshajiona wazee. Kwa wazoefu tuliobahatika kwa neema za Mungu kuziishi awamu zote za Urais nchini hatuna mawaaa tunapowapima viongozi wetu.

Narudia tena pasi kumvunjia heshima Mzee wangu Mzee Ruksa, alikuwa Rais dhaifu na bila shaka yeyote aliyedharaulika kuliko rais yeyote katika historia ya nchi yetu.

Hakuwa mjenga hoja pale alipobanwa hata na vijana wa chuo kikuu hapa Mlimani (Kina Mbatia et al) na wala haku execute any notable actions against maadui zake wala wa nchi yetu.

Udhaifu wake ulionekana si kwa waliokuwa chini yake tu, bali hata wastaafu na hata vijana wa nje ya Chama na wa vyuo vikuu.

Kuwa dhaifu si dhambi, ni sawa na kuwa mfupi ama mrefu. Kamata nakala yako ya MZEE RUKSA ujipe elimu walau juu ya mapungufu ya Mzee wangu Mwinyi na si kupuyanga kujibu hoja kwa hisia na si kwa kutumia ubongo!
 
Miaka ile ya mwisho mwa uongozi wa Nyerere kuelekea ile ya Mwinyi hapa bongo kulikuwa na umaskini mkubwa sana. Mzee Mwinyi ikabidi akubaliane na masharti ya IMF kama yalivyoletwa.

Ni katika kipindi hicho cha miaka ya 1980 katikati ndio vijana wengi wenye uwezo na elimu waliposafiri kwenda Uingereza, Canada na Marekani. VIjana wenye elimu wakiwa ni watoto wa wazazi wenye nafasi serikalini ndio wakafanya mikakati ya kufanya mitihani ya TOEFL ili wapate nafasi za kujiunga na vyuo vikuu vya huko nje.

Hawa wanaoitwa diaspora wengi wao waliondoka nchini kipindi hicho, hali ya uchumi ilikuwa mbaya tukiwa tumetoka kupigana vita ya Kagera, na hazina ya nchi ikiwa tupu.

Hivyo Mzee Mwinyi ni shujaa mwenye kila aina ya haki ya kuenziwa. Wapo wanaojaribu kumdhihaki lakini alichokifanya kwa kutazama mazingira ya wakati ule ni chema kwa ajili ya Tanzania.
Mkuu kwa heshima zote Mzee Mwinyi hadhihakiwi. Ila wanaomsema wanamsema kwa uelewa wao kama ambavyo wewe umemuelezea kwa uelewa wako.

Kama marais wengine waliomfata na kustaafu na aliyemtangulia kwa cheo chake tu anapaswa na ndivyo ilivyo anaenziwa.

Kuenziwa kwake hakutunyima haki ya kumpima uimara wake kama kiongozi mkuu wa nchi katika nyakati zake kwa kulinganishwa na aliyemtangulia na waliomfata.
 
Mtwara ni asili yake, bali alishiriki serikali ya zanzibar na bado familia yake inaishi zanzibar hata sasa.
Sikatai juu ya hili, je asili yake ni wapi? Ndio kinachomata.
Na sio yeye pekee, bali wapo hadi wenye asili ya Tanga walioshiriki kwenye mapinduzi.
 
Alipata, sio "ali pata."
Hujasoma, sio "huja soma."

Kuandika kwenyewe hujui halafu unaniuliza mimi kama akili zangu ziko sawa.

Pia Tanzania hakuna "white house," kuna State House.

Huwezi hata kuandika maneno ya Kiswahili, umesoma shule wapi wewe ?

Mwinyi hakupewa msukumo wa kuondoka, alijiuzulu mwenyewe kwa siku aliyopanga mwenyewe. Huwezi kuacha kazi halafu ukabaki kwenye nyumba.

Alijua anaondoka, akaacha eneo limezagaa building material utadhani construction site, alikosa uungwana. Mwenye chake muungwana.
Sasa alivirudisha vya nini
 
Kuna yule aliyempiga kofi!!!
Halafu mzee akasamehe kwa status ya mwinyi , angeozea jela
Na bado hakuwa na kinyongo kwa wale "mashemeji" zake yaani wanafunzi wa shule ya sekondari Forodhani waliokuwa wakipiga kelele za "shemeji, shemeji" kila msafara wake ulipokuwa ukipita maeneo yale kwa vile alijichukulia kibinti kidogo kilichokuwa bado kinasoma shule hiyo miaka hiyo. Huyo binti alikuwa mtoto wa KK aliyekuwa meya wa jiji la Dsm kipindi hicho.
 
Linapokuja swala la mahusiano kila mtu ana udhaifu wake,
Bahati mbaya unapokuwa na status kubwa haya mambo yanakuwa hayafichiki tena ,
Nina hakika hata wewe una matukio yako ya kimahusiano ambayo unasema hili likijulikana nimekwisha!
 
siyo rahisi kukubali uteuzi ki ivo wewe!!. Huyo waziri hana ubongo au!!!

Nasema. hakujua kabisa kosa lake huyo hata usipomsamehe mbinguni anaenda. Angejua ile dhambi ingemtesa sana tu!! lazima.km angejua amezulumu.

Aliona labda ni matofali ya sirikali sababu Mwinyi hakumlalamikia wala kuyadai.ayafanyeje sasa.

Au alimwekea mtego kisiri kuwa amemnyanyapaa?? Hiyo sasa ni mwinyi. hata ka Mungu haikubaliki.

Laiti angefanya maksudi asingekubali uteuzi piga ua.

Atakuamini vipi? Atadhani unataka kulipiza ki aina.

Mtu akikufanyia ubaya maksudi na akajua kuwa umejua lkn umempotezea tu kirahisi Na unauwezo wa kumfanya chochote anaweza kufa ghafla kwa kihoro......narudia.....

Bora mtu umseme!! urushe ngumi kidogo!!matusi. atajua haya...yameisha...lkn ukipiga kimya weeee!!thubutuuuuuu
Kama hakujua alichomtendea Mzee Mwinyi, ni kipi kilimjulisha makosa yake hapo baadae hadi akamrudishia mabati yake?
 
Sasa alivirudisha vya nini
Alimrudishia kwa sababu alishampa somo la kuhadithia milele na hatarudia tena kusumbua watu majumbani kwao wamtunzie mabati kwenye front yard ya Waziri.

Nitarudia mpaka uelewe: Mwenye chake muungwana.

Mtu akikunyanyasa na mali yake, na nyumba yake, hata akufukuze kama mbwa ni yeye ndio muungwana kwa sababu ana kwake, hasumbui mtu. Wewe unaesumbua watu wakutunze au wakuhifadhie mabati majumbani mwao, wewe ndio sio muungwana.

Mwinyi alijua ni yeye amekosa uungwana ndo maana pamoja na yote hayo bado akamwita awe Waziri kwenye serikali yake.
 
Ni member wa Mapinduzi Marehemu Major General Said Abdallah Natepe.

Na sio Mzee Hassan Nassoro Moyo kwa kuwa Mzee Moyo hakuwahi kuwa Waziri kwenye serikali ya Mzee Mwinyi awamu zote mbili 1985-1990 na 1990-19995
Mzee Moyo hakuwahi kuwa Waziri kwenye serikali ya Mzee Mwinyi.
Umetoa conclusion kwa kumwangalia Mzee Mwinyi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku ukisahau pia amepata kuwa Rais wa Zanzibar!

Rekodi mbalimbali zinaonesha Abdallah Said Natepe aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwaka 1980, na aka-resign mwaka 1983 baada ya wafungwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya uhaini (au labda walishakuwa convicted), yaani Pius Lugangira na Hatty MacGhee kutoroka gerezani!

That being said, sina shaka yoyote anayezungumziwa hapa ni Hassan Nassoro Moyo ambae alikuwa waziri wa kilimo Zanzibar from 1980 to 1985, na pia ndie alichukua nafasi ya Mwinyi pale mambo ya ndani!
 
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom