Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Na ni yeye Mwinyi ambae hakuwa muungwana.

Alitaka waziri afanyeje, amtunzie mirunda na mi kokoto yake mbele ya nyumba ya Waziri?

Au waziri asinunue vya kwake kwa sababu hakuna nafasi ya kuvitunza nyumbani kwake ?

Na kama mtu umemwona ni mdhulumati kwa nini umempa uwaziri, ili atuibie ?

Wana bahati sana wanaandika vitabu vya gibberish kama hizi huku Afrika ambako hakuna audience ya kuchambua pumba na michele wanayoisema

..nahisi ni mifuko ya sementi iliganda mzee akadhani amefanyiwa fitina.🤣
 
Kwa hisani kubwa kabisa ya Jamiiforums tarehe 23 Julai 2019
: Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi

Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa mzee Abdallah Said Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Meja Jenerali Abdallah Said Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Meja Jenerali Natepe.

Ikampasa mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serikali.

Mzee Abdallah Said Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee Ali Hassan Mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Mzee Abdallah Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee Ali Hassan Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hapa sasa Mzee Meja jenerali Abdallah Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee Ali Hassan Mwinyi.

Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Abdallah Said Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia mzee Abdallah Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu Mh. Ali Hassan Mwinyi rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe, mzee Ali Hassan Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

N.B
Habari za ziada kwa hisani ya intaneti

Sunday, September 26, 2010​

MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR ABDALLA SAID NATEPE AMEFARIKI DUNIA​


Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.

Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”
Angekuwa mwendazake sasa, sijui angefanywa nini
 
..lakini kuna jedwali linaonyesha aliyempokea Mzee Mwinyi wizara ya mambo ya ndani ni Hassan Nasoro Moyo.

..Je, huko kwenye kitabu Mzee Mwinyi amemtaja kwa jina mhusika au ametuachia kitendawili tutegue wenyewe?
Soma bandiko Number 24.
 
..lakini kuna jedwali linaonyesha aliyempokea Mzee Mwinyi wizara ya mambo ya ndani ni Hassan Nasoro Moyo.

..Je, huko kwenye kitabu Mzee Mwinyi amemtaja kwa jina mhusika au ametuachia kitendawili tutegue wenyewe?
Mzee Moyo wakati Mzee Mwinyi anajiuzulu alikuwa ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais maana yake alikuwa ana nyumba tayari ya serikali.

Iko hivi ukiwa waziri ukahamishiwa wizara nyingine huhami nyumba unahama ofisi tu.
Kwa hiyo hakukuwa na sababu Mzee Moyo kuhama nyumba aliyokuwa akiishi wakati akiwa waziri wa Nchi na kuhamia alipokuwa anakaa Mzee Mwinyi eti kisa amemrithi wizarani.

Kilichofanyika ni kuwa Mzee Moyo alihama kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kwenda ofisi ya Mambo ya Ndani na sio kuhama nyumba.

Mzee Natepe(Major Geneal Mstaafu) aliteuliwa kuwa katika baraza la mawaziri na kulazimika kupewa nyumba na serikali na ndipo alipopewa ya anayetoka Mzee Mwinyi.
 
Anazungumziwa aliyerithi wizara baada ya Mwinyi kujiuzulu, au waziri kwenye serikali ya Mwinyi!
Kitabu kinasema "Baada ya Mzee Mwinyi kuchaguliwa Rais alimteua huyo bwana aliyemdhulumu vifaa vyake vya ujenzi na kumtoa kwenye nyumba.."

Msingi wa hoja yangu upo hapa
 
Huyu ni Mzanzibar tena ni muhasisi wa mapinduzi matukufu.
Kuasisi mapinduzi sio kuwa Mzanzibar, mzee Natepe kwao ni kusini. Kwani John Okelo aliyeongoza mapinduzi alikuwa Mzanzibar?
Kuna mzee Natepe na Kisasi, je unamfahamu mzee Kisasi?
 
Hiyo siyo sifa. Alilea mwizi, shame on him.
Kumsamehe na kumuonesha upendo mwizi au mtu aliekufanyia ubaya ni sifa nzuri ktk maisha... Hata Yesu aliwasamehe na kuwaombea msamaha kwa Mungu wale wote walimtesa mpk kufa pale msalabani, je kwa mtazamo wako unafikiri Yesu alikuwa mjinga?
 
Back
Top Bottom