Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Mwarobaini watu tumekunywa miaka na miaka maini hayajafa wewe unasema hapa. Hao walioua uliwaona wapi. Mnaua kwa konyagi mnasingizia mwarobaini. Hiyo ni dawa nzuri sana ya malaria kama hujui
Pole sana.kama unaweza kusoma vizuri angalau ungeweza kuhisi vizuri usingeandika ulichoandika
 
.... Aiseeee!! Ile ya madagascar aliyokwenda kuichukua kabudi ipo wapi?
Hahaha umenikumbusha mbali. Taifa linaloongozwa kwa hurela alfa hurela Ila wananchi wake baadhi wanajielewa na hawana nguvu yakuleta mabadiriko
 
Nimr nayo ina wanasayansi ama waganga wa kienyeji?😂. Unajua maana ya sayansi?

Kitu chochote ili kiwe cha kisayansi lazima kiwe na universality, replicability, sasa ulisikia watu gani wengine Duniani wamesema chumvi, pilipili, kitunguu maji, kitunguu saumu, majani ya mlimao yanatibu corona?
Kwa hili NIMR wameingia chakaaa!!! Nawasahuri NIMR wasiseme dawa bali warudie kale ka msemo "TIBA LISHE"
 
Utajuaje unaumwa COVID kama hakuna vipimo?
Ukisikia kupumua kwa shida unasubiri kipimo? dudumia dawa chap chap .Kipimo ukisubiri ukikata pumzi tusilaumiane hapa siji hata kukuzika umeyataka
 
Ukisikia kupumua kwa shida unasubiri kipimo? dudumia dawa chap chap .Kipimo ukisubiri ukikata pumzi tusilaumiane hapa siji hata kukuzika umeyataka
Tutapataje takwimu za watu waliopumua kwa shida na ufanisi wa hii dawa?
 
Kwa hili NIMR wameingia chakaaa!!! Nawasahuri NIMR wasiseme dawa bali warudie kale ka msemo "TIBA LISHE"
Dawa nyingi ni za kula na kunywa ni lishe sababu asilimia kubwa zinapitia mdomoni

Lishe ni chochote kinachopitia mdomoni kisicho cha lishe ni kama sindano za kuchomwa mwilini kwenye makalio nk
 
Ilikuwa za kwetu bado kugundua ulitaka watu wafe hadi tutakapogundua?
Sasa mbona hamkuzigawa kwa watu na mkaacha kuwapima?

Mkadai kuwa Korona imeisha kwa maombi ya siku ya 3, hapo hapo mkakataza kutangazwa kwa visa vya Korona, mkaacha watu wakaendelea kufa.

Yaani mkasababisha hasara kote kote( watu kufa na hasara ya gharama kuleta mzigo wa Madagascar )
 
Waziri wa Afya Dk Gwajima azindua dawa ya Asili ya Corona waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Uwe na CHOMBO cha kuweka huu mchanganyiko

Moja Chukua limao mbili zikate kate na maganda yake toa mbegu tu tupa huko .Vipande ulivyokatakata weka Kwenye chombo

Pili chukua kitunguu maji chekundu kimoja kikate kate kiweke kwenye chombo ulimoweka limao ulizokatakata

Tatu Chukua Tangawizi tano za saizi ya kidole gumba Zikatekate weka kwenye chombo

Nne chukua Kitunguu saumu chukua punje kumi za kitunguu saumu weka kwenye chombo

Tano chukua pilipili kichaa nne Katakata weka kwenye chombo

Chukua maji lita moja changanya kwenye hicho chombo

Weka kwenye blenda au kwenye kinu saga huo mchanganyiko

Huo mchanganyiko ukishasaga hiyo juice yake ndio uinywe

Pilipili kichaa 4![emoji23]
 
Mwandishi unapotosha unaposema dawa ya Corona. Corona haina dawa mpaka sasa. Nyungu inasaidi kwa siku tatu kabla Corona haijaingia kwenye mapafu. Vidudu vinakufa vikiwa bado puani kama temp ikifika 51 na ndiyo maana wanahimiza kufukiza. Kinga nzuri mpaka sasa ni kuvaa barakoa, kunawa na sabauni na kuweka mika moja na mtu mwingine
 
Wakati mwingne Jf nawafananisha na wachambuzi wa soka hasa wa hapa Tz. Utasikia wanaelezea matukio ya wachezaji uwanjani,na hata sometime kukosoa kuwa pale mchezaji alitakiwa kupiga kwa kufunika mguu, mpira ungempita mgongoni beki na kupita katikati ya miguu ya golikipa na kujaa wavuni. Ukitaka balaa sasa tafuta historia yake,utashangaa kuona hajawah kucheza soka hata kugusa tu chandimu utotoni.
Ndiyo,jamaa zangu wa humu jukwaan kila jambo tunabisha tu..hahahaha!!!
 
Kwanini asilimpelekee Magufuli maana yupo chato toka ugonjwa umeingia kwa kasi tena. Huu ni global disease ujinga wake amueleze mume na Magufuli.
Mchanganyiko wa Taaluma na Siasa unapelekea vitu kama hivi ?

Hio ni Dawa inatibu au ni lishe inayoongeza kinga hence mwili kuweza kupambana vyema...,

Na swali la nyongeza nini msimamo wa Wizara kuhusu Corona ipo au haipo na kama haipo dawa ni ya nini ?
Unauliza wakati jibu unalo mwenyewe, hiyo pia ni dawa kwa sababu Ina boost immunity yako (tiba lishe).
 
Back
Top Bottom