Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Mchanganyiko wa Taaluma na Siasa unapelekea vitu kama hivi ?

Hio ni Dawa inatibu au ni lishe inayoongeza kinga hence mwili kuweza kupambana vyema...,

Na swali la nyongeza nini msimamo wa Wizara kuhusu Corona ipo au haipo na kama haipo dawa ni ya nini ?
Maswali ya msingi sana haya
 
Hata dawa unazokunywa za wazungu nyingi ni mitishamba,mboga mboga na matunda na majani ya miti au hujui hilo?

Hizo dawa za mitishamba wenzetu waliotuzidi akili wanatajirika nazo sie bado tunalala kwenye matembe!!! Wazungu na Wachina kila leo wanashinda humu nchini kutafuta mitishamba kutoka kwa waganga wetu wa kienyeji; baada ya hapo wanarudi kwao na kuzitengeneza kama food supplements na kuwatibia ndugu zao na kutengeneza mabilioni ya shilling!! " MDHARAU CHAKE NI MTUMWA!"
 
madini ya kutengeneza hizo smartphone yanatoka kwetu au hujui hilo?
Labda mm ndy nikupe ufahamu kuhusu hayo madini ya coltan (columbalite tantalite)
Mwenzako nishafika mpaka north kivu congo!
Utaniambia nini mimi

Ova
 
na wote waliokunywa kikombe cha babu na wakaacha dawa za hospitali wameshaondoka!!
Hapana.
Kasoro 'Jiwe' bado anadunda!
Ni kweli kabisa
Kwa sasa siyo "kweli" tena. Ingia 'pharmacy' yoyote, kama una bahati watakuonyesha quinine pekee katika dawa zote walizonazo humo.
Dr.Gwajima atupe hata publication moja kuhusu hizi dawa,walipewa wangapi katika condition gani na matokeo yake yakawaje.
Kazi ya mkemia mkuu ni kuangalia kuwa hakuna ingredient ambazo zinaweza kuwa ni sumu lakini si kazi yake kupima efficacy wala efficiency ya dawa.
Kazi kubwa ya utafiti wa dawa yoyote ni kuhakikisha ni "salama" na kama "inafanya kazi" inatibu ugonjwa unaolengwa.

Hii si dawa, haihitaji utafiti wa namna hiyo. Usalama wake unajulikana; kwa sababu vitu vyote ni chakula na viungo vinavyotumiwa duniani kote. Kuhusu sehemu ya pili "potency", wanatumia ushahidi 'anecdotal' evidence', mazoea ya watu kuitumia kwa matumizi kama hayo. Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi amabo unapatikana kwa kufanya utafiti (clinical study) kujua kwa uhakika kwamba inafanya kazi.
 
Labda mm ndy nikupe ufahamu kuhusu hayo madini ya coltan (columbalite tantalite)
Mwenzako nishafika mpaka north kivu congo!
Utaniambia nini mimi

Ova
na sisi kabanga mines kagera tuna madini ya kutengeneza simu
 
dose

Kunywa mililita 20 sawa na vijiko vikubwa vya chakula viwili (2) kila baada ya masaa 8.

Kwa ambao tayari ni wagonjwa kunywa hadi utakapo pona

Kwa ambao sio wagonjwa unaweza kutumia kiasi hicho
mara moja au mbili kwa siku kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.
Niulize swali! Baada ya kusaga huu mchanganyiko na maji ya lita moja ya moto unaweza kuchuja na kuwa kwenye kimiminika aina na juice? Au unautumia hivyo hivyo
 
Wakati mwingne Jf nawafananisha na wachambuzi wa soka hasa wa hapa Tz. Utasikia wanaelezea matukio ya wachezaji uwanjani,na hata sometime kukosoa kuwa pale mchezaji alitakiwa kupiga kwa kufunika mguu, mpira ungempita mgongoni beki na kupita katikati ya miguu ya golikipa na kujaa wavuni. Ukitaka balaa sasa tafuta historia yake,utashangaa kuona hajawah kucheza soka hata kugusa tu chandimu utotoni.
Ndiyo,jamaa zangu wa humu jukwaan kila jambo tunabisha tu..hahahaha!!!
Mtu kama YEHODA inamhusu sana. Na si katika mjadala wa aina hii tu, karibu kila mjadala huwa hana mchango wa kuonyesha kuna analojua juu yake.
 
Jiwe anaiharibu Tanzania yetu. Sasa jiwe anahalalisha ushirikina nchini
 
Niulize swali! Baada ya kusaga huu mchanganyiko na maji ya lita moja ya moto unaweza kuchuja na kuwa kwenye kimiminika aina na juice? Au unautumia hivyo hivyo
unachuja kwa chujio kwanza
 
Mchanganyiko wa Taaluma na Siasa unapelekea vitu kama hivi ?

Hio ni Dawa inatibu au ni lishe inayoongeza kinga hence mwili kuweza kupambana vyema...,

Na swali la nyongeza nini msimamo wa Wizara kuhusu Corona ipo au haipo na kama haipo dawa ni ya nini ?

Mfano, akisema ipo; utafanya nini?

Akisema haipo, itakusaidia kitu gani?

Umeshaambiwa Corona ipo nchi jirani na inawezekana ipo Tanzania kwa hiyo chukua tahadhari, na tahadhari za kuchukua ulishapewa siku nyingi. Tena ukaambiwa haina dawa, ila kuna tiba lishe na ukapewa mwongozo namna ya kuandaa ambapo hata buku 2 haziishi ila bado mnauliza maswali ya kijinga kabisa yaani zero face and brain combined!

Aisee!
 
Upumbavu tu tuambiwe kwenye hizo product kuna nutrient na ingredients gan and how do they play a physiological role of rise a body immunity from immunologic perspective
Tufuate miongozo ya wataalam kujikinga na colona
 
Mfano, akisema ipo; utafanya nini?

Akisema haipo, itakusaidia kitu gani?....
Wizara ya Afya na Viongozi hawapo pale kama maigizo au waigizaji ni taasisi inayotoa miongozo na Taarifa zote kuhusu afya ya wananchi.

Inasikitisha sana hata hujui kazi ya taasisi eti akisema ipo nitafanya nini ( akisema ipo inabidi atoe miongozo) na kama haipo ni taadhari gani wanafanya ili iendelee kutokuwepo.

Hawapo pale kuuza sura bali wapo hapo kuhakikisha afya ya kila mwananchi na kipindi hiki ambapo kila nchi duniani inasumbuka na hili janga inabidi nao kwa kusaidiana na wenzao watafute kila mbinu ya kupambana....
 
Back
Top Bottom