Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

msipuuze hiyo michanganyiko nimetoka hospital juzi na imenisaidia sana

Shuhuda kama hizi zipo nyingi hata mtaani. Ila kuna watu wana gubu hawataki. Sijui wanataka nini 😀
 
Kazi ya mchanganyiko wa vyakula hivi ni ku boost kinga ya mwili ili uweze kupambana na maradhi
Unao ushahidi gani kuhusu madai haya! Kuna utafiti wowote unaoonyesha ushadi huo? Ninaposema 'utafiti' usiniwekee mambo ya vijiweni au 'hearsay!.
 
Tiba asili inasaidia mengi sio Corona tu!
1. Uzazi
2. Nguvu za kiume
3. Surua na tetekuwanga
4. Kansa
6. Mafua
7. Pumu
8. Mafua
9. Mifupa nk
Tuthamini dawa za asili maadamu hakuna kupiga RAMLI chonganishi!
10. Kumrejesha mke au mume aliyekukimbia.
11. Mke au mume kukupenda, a.k.a. limbwata.
12. Kuona wachawi.
13. Misukule
14. n.k.
 
Unaonaje tukifuta wizara ya afya halafu kila mtu akapewa kitabu cha turejee edeni, kutakua na haja ya kua na wizara ya afya tena ama kutakua na haya ya kua na hospitali? Zote itabidi zifungwe, sio?
ni kama vile umejipanga kubishana, ngoja nikuache
 
Hapana.
Kasoro 'Jiwe' bado anadunda!

Kwa sasa siyo "kweli" tena. Ingia 'pharmacy' yoyote, kama una bahati watakuonyesha quinine pekee katika dawa zote walizonazo humo.

Kazi kubwa ya utafiti wa dawa yoyote ni kuhakikisha ni "salama" na kama "inafanya kazi" inatibu ugonjwa unaolengwa.

Hii si dawa, haihitaji utafiti wa namna hiyo. Usalama wake unajulikana; kwa sababu vitu vyote ni chakula na viungo vinavyotumiwa duniani kote. Kuhusu sehemu ya pili "potency", wanatumia ushahidi 'anecdotal' evidence', mazoea ya watu kuitumia kwa matumizi kama hayo. Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi amabo unapatikana kwa kufanya utafiti (clinical study) kujua kwa uhakika kwamba inafanya kazi.
Asante sana,:hii si dawa",umemamliza kila kitu.Ni "tiba lishe"
 
Nchi imegeuka kua ya kishirikina, inchi ya wapiga ramli.

Toka lini kachumbari/chachandu ikawa tiba ya magonjwa?

Tufute wizara ya afya maana haina uhumimu, tutumie waganga wa kienyeji na wapiga ramli.
Dawa nyingi unazozifahamu ni za kienyeji hata hizo zinazotoka nje zinatokana na mimea.
Hii dawa yao kama inatibu basi inshaalah
 
Kwanini asilimpelekee Magufuli maana yupo chato toka ugonjwa umeingia kwa kasi tena. Huu ni global disease ujinga wake amueleze mume na Magufuli.
Jamal's udaktari wake pembeni,Anaburuzwa na Kuwe,Eeh mungu ibarika Tanzania
 
Asante sana,:hii si dawa",umemamliza kila kitu.Ni "tiba lishe"
Lakini, hata hilo neno "Tiba Lishe" sijui hasa linalenga nini. Linaweza kuwa na utata.

Kuna vigezo vyovyote vinavyofuatwa kuonyesha kuwa chakula/kiungo kina sifa ya kuwa "Tiba Lishe"?

Ni vigezo gani hivyo, na vinahakikiwa vipi?

N.B. Nimekumbuka: "Tiba Lishe" ndio "Food supplement"?
 
Waziri wa Afya Dk Gwajima azindua dawa ya Asili ya Corona waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

MCHANGANIKO WA DAWA LISHE NA MITI DAWA KWA AJILI YA TIBA YA KORONA

Namna ya kuandaa DAWA LISHE

Mahitaji:
1 Tangawizi ya urefu wa
kidolegumba chako vipande 5
2 Kitunguu swaumu punje 10
3 Pilipili kichaa 4
4 Kitunguu maji chekundu kikubwa1
5 Limao 2
6 Maji ya moto Lita 1

Uandaaji:
1. Osha dawa lishe zote,
2. katakata vipande vidogo vidogo,
3. Ondoa mbegu za limao,
4. Saga mchanganyiko wote kwenye Brenda. (kama huna Brenda au twanga kabla ya kuweka maji moto)
5.Chuja na chujio
6.Hifadhi katika chombo safi kama chupa safi

Kunywa mililita 20 sawa na vijiko vikubwa vya chakula viwili (2) kila baada ya masaa 8.

Kwa ambao tayari ni wagonjwa kunywa hadi utakapo pona

Kwa ambao sio wagonjwa unaweza kutumia kiasi hicho
mara moja au mbili kwa siku kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

=====

WAGANGA WAKUU IMARISHENI MIFUMO YA UDHIBITI NA KINGA YA MAGONJWA: Dkt. GWAJIMA

*Wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya,Wafawidhi na Maafisa Afya Mazingira nchini wametakiwa kuendelea kuimarisha mifumo yote ya udhibiti na kinga ya magonjwa kwa kushirikiana na wananchi ili kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema viongozi hao wanatakiwa kuwakumbusha wananchi kwenye elimu ambayo Wizara imekuwa ikiitoa ikiwemo kuimarisha usafi, kujifukiza, kufanya mazoezi, kula lishe bora, kunywa maji mengi bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo taifa hili limejaaliwa.

“Serikali itaendelea kuchukua tahadhari zote za ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa yote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote na kuendelea kuelimisha wananchi juu ya hatua za kuchukua”. Alisisitiza Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema Wizara yake haina mpango wa kupokea Chanjo ya COVID-19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye mataifa mengine kwani Serikali kupitia wizara ya afya inazo taratibu zake za kufuata pale inapotokea kupokea bidhaa yeyote ya afya na hufanyika baada ya Serikali kujiridhisha na sio vinginevyo.

Kwa upande wa Tiba Asili Dkt. Gwajima amesema Wizara kwa kushirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali , Baraza la Tiba Asili na wananchi wajuzi wa tiba asili tayari wameshafanya usajili wa bidhaa (dawa) za tiba asili, alizitaja miongoni mwa dawa hizo ni COVIDAL,NIMECAF,PLANET++,BINGWA na COVOTANXA.

Aliongeza bidhaa za mafuta tete ambayo imehakikiwa na Mkemia Mkuu kuwa ni salama na zinatumiwa na watu mbalimbali ni Uzima Herbal Drops, BUPIJI, EUCALYPTUS OIL, LEMONGRASS ESSENTIAL OIL na bidhaa zingine zitaendelea kutajwa na Baraza la Tiba Asili

“Uko ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu watu wengi ambao wamepata nafuu na kupona magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ambukiza yaliyokuwa yanawasumbua mara baada ya kutumia dawa za tiba asili hata kama walikuwa kwenye matibabu mengine ya dawa za hospitali”.Alisema Dkt. Gwajima.

Hata hivyo Waziri huyo alilielekeza Baraza la Tiba Asili/Mbadala kutoa orodha ya dawa zote ambazo zimepita kwenye utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kimaabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuonekana kuwa matokeo ya awali ya uchunguzi ni salama kwa matumizi na kuwa dawa hizo zimekuwa zikitumiwa na watu wengi kwa muda mrefu na kuwaponya ama kupata nafuu.

Dkt. Gwajima amewataka wataalamu wote na wajuzi wa tiba asili wasisite kujitokeza na kufuata taratibu za kuwasilisha dawa na bidhaa zao kwa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ili zifanyiwe uchunguzi wa kimaabara kabla ya kukabidhi taarifa ya matokeo ya uchunguzi Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Waziri amesisitiza kwenye kujikinga na hivyo Serikali imeboresha kwenye viwanja vya ndege,mipaka pamoja na sehemu za kupimia magonjwa mbalimbali ili yasiingie nchini kwa watu wanavyoingia na kutoka.

“Tiba asili sio jambo la leo,tumezaliwa tumeona akina mama zetu wanatumia baadhi ya majani kwa kutibu mafua au homa na kujifukiza na baada ya hapo wanatoka salama na kuendelea na kazi,hivyo tiba asili haijatokana na ugonjwa wa Corona bali ni kutoka enzi na enzi”.

Dkt. Mollel amesema hatua za usafi zinatakiwa kuongezwa nguvu na kuwataka wataalamu wa afya kuacha kufikiria mgonjwa anavyoenda kwenye kituo cha afya anaumwa kifua ana Corona bali kuhakikisha wanampima vipimo vingine ili wasije kuuwa watu na mambo mengine ambayo hayana uhusiano na Corona.
View attachment 1691879View attachment 1691881View attachment 1691882View attachment 1691883
Akionesha mfano wa kujifukiza kwa Waandishi wa Habari
View attachment 1691886View attachment 1691887View attachment 1691888
View attachment 1691889
Zilipendwa.Hata ile ya Madagascar mlikunywa wenyewe hamkutupa.Na hii kunyweni wenyewe kwanza hakuna Corona Tanzania. Mchanganyiko huu tulishakunywaga siku nyingi.Labda mtupe mpya.
 
Upumbavu mtupu.
Dawa ya nini huku mnasema hakuna COVID 19?.
Kila mvumbuzi bongo anaavumbua dawa ya COVID 19 ikiwa na contents zilezile
 
Wanasanyansi wa kitanzania wa National Institute for Medical Research (NIMR) ndio wamefanya huo utafiti .Huwaamini wanasayansi wetu? Ulitaka wawe wakoloni wazungu waliojaa kichwani kwako ndio wafanye uwaamini?
Wanasayansi hawaruhusiwi kusema chochote hata kama ni wao wamegundua.Wanaotakiwa kusema mafanikio ya utafiti wao ni wanasiasa.Over
 
Mwarobaini watu tumekunywa miaka na miaka maini hayajafa wewe unasema hapa. Hao walioua uliwaona wapi. Mnaua kwa konyagi mnasingizia mwarobaini. Hiyo ni dawa nzuri sana ya malaria kama hujui
Weka data za tafiti au andiko hapa.Ahsante.
 
Back
Top Bottom