Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Ndugu yangu, ahsante kwa mchango wako kwenye mada hii. Ni Katika wadau tu kuchangia hoja mbalimbali ndiyo tutajenga jamii yetu kutazama mambo Kwa sura mbalimbali kulingana na mazingira.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Maandishi yako makubwa yanaumiza macho ,hapa si vitani andika kwa herufi ndogo utaeleweka vizuri tu.
 
Ni lazima kulinda maadili. Kuachia Mmomonyoko ni hatari kwa jamii. Nipongeze kijiji cha Arumeru kwa ujasiri na upendo kwa vijana wao.
Vijana ni msingi wa taifa ni lazima wahifadhiwe ki maadili.
Ila kule dodoma wakifanya mmomonyoko wa maadili kama yule naibu waziri sio hatari.Lakini madogo wa Arusha wakinyoa viduku ni hatari
 
Ulienda shule kusomea ujinga ndio sababu unaelimishwa unashupaza fuvu. Unashikilia kuvaa kimini badala ya kuangalia mzizi wa sheria za watu wa arumeru.
😂😂😂 acha kupanic Mkuu, chagia mada kwa hoja mjadala uende vizuri... vimini, jinzi, mitindo ya nywele si chanzo cha kuharibika kwa maadili....mambo yametokea enzi na enzi leo ndio tunasema yanaharibu jamii? Jamii ingekuwa imepotoka kitambo sana kama hili lingekuwa kweli. Unakubali kuwa wizi kwenye kijiji hicho umetokea sababu ya mavazi na mitindo ya nywele? Embu kuwa serious bwana
 
Hamia Marekani. Acha kubishabisha kipuuzi. Mheshimiwa waziri kwenye uzi mmoja kajitahidi kufafanua ila wewe umeng'ang'ania kubisha. Pumbavu sana. Nadhani mimi utanielewa kwasababu kistaarabu huelewi.
Ndio maana ya kubishana kwa hoja na matusi wala kejeli, kutukana na kutumia lugha mbaya inaonesha tu uwezo wako mdogo kichwani... mwenye uelewa wala hajapinic na anachangia mada vizuri tu, una la kujifunza hapo. Ukiangalia upande mzuri wa kitu angalia na upande mwingine wa shilingi
 
Asante kwa mchango wako Mkuu, nina swali kidogo hapa... kuna jamii ambazo wanavaa vipisi vya nguo kama utamaduni wao na husikii mambo ya kumomonyoka kwa madili wala vitendo vya ukatili... suala la kumsababishia mtu ushawishi sababu fulani kavaa nguo fupi au iliyochanwa sio kwamba inatumika kama kisingizio cha kuhalalisha vitendo vibaya kufanyika? Unatenda kosa na kumtupia mtu lawama kwa kushindwa kutuliza tamaa zako?
 
Ni lazima kulinda maadili. Kuachia Mmomonyoko ni hatari kwa jamii. Nipongeze kijiji cha Arumeru kwa ujasiri na upendo kwa vijana wao.
Vijana ni msingi wa taifa ni lazima wahifadhiwe ki maadili.
Swali je, ni mitindo ya nywele na mavazi ndio mzizi wa mmomonyoko wa maadili?
 
Acheni kuwa mashabiki wa ujinga watu wa aina hii ndio mmekuwa vichocheo vya ushoga na mmonyoko wa maadili Kwa nyanja mbalimbali.
Leta hoja mkuu, kivipi kiduku kinaleta mmomonyoko wa maadili, tuweke hisia pembeni na kuangalia mzizi wa tatizo. Usiniambie vijana wamejiingiza kwenye wizi na matendo mengine maovu kisa mtu kanyoa kiduku au kavaa jinzi. Ili kumaliza vitendo hivyo ni muhimu kujua tatizo limeanzia wapi na sio kutupia lawama kwenye vitu ambavyo ni rahisi kuwa midomoni mwa watu na kukwepa kuwajibika
 
enzi zipi zilivaliwa
 
Dkt gwajima D. ni waziri anayefanya kazi zake kama zima moto "reactive" siyo "proactive".

Kama ni daktari wa binadam simshangai, ndivyo uzoefu wa madaktari ulivyo. kazi zaoni kuzima moto tu.


Ulishwahi kusikia Daktari yupi wa Tanzania kabuni kitu kipya kwa ubunifu wake? Labda abuni porojo na ngonjera (theories) tu.
 
Asante kwa kuongeza ufafanuzi huu, maelezo ya kwanza hayakuridhisha, kwa kupeleka wataalamu walau hapo unatoa matumaini kuwa kutakuwa na muongozo na maboresho kwa kile walichokianzisha👏👏
 
Ahsante Sana kwa evaluation yako. Sasa zimamoto ipi tena iwapo mpango Mkakati kutokomeza ukatili upo rasmi na tunaelimisha utekelezwe na jamii ila jamii inajivuta ukiwemo wewe hapo. Tena wewe ni mtoa mada humu miaka mingi ambaye nilidhani na wewe ungekuwa proactive kuelimisha jamii kuhusu huu mpango tangu uzinduliwe uwe Balozi, kumbe na ww unasubiri tu ku react kwenye taarifa za hapa na pale.

Halafu wanajamii wengine wakitekeleza mpango tukasema tukawape moyo mnasema tuko reactive. Kumbe hiyo proactive inakuwa yangu peke yangu nyie jamii hamtakiwi kuwa? Kumbe itakuwaje Sasa wakati mpango ni wa wizara na jamii.

Hata hivyo, ahsante Sana kwa mchango wako ila sasa amka upite google usome MTAKUWWA kisha urudi uangalie ww hapo kwenye eneo lako jukumu lako lipi Ili likitokea tatizo usiwe reactive wewe na jamii yako Bali muwe proactive. Hbr za asubuhi lakini.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa kuongeza ufafanuzi huu, maelezo ya kwanza hayakuridhisha, kwa kupeleka wataalamu walau hapo unatoa matumaini kuwa kutakuwa na muongozo na maboresho kwa kile walichokianzisha[emoji122][emoji122]
Maelezo yalikuwa sawa tangu mwanzo ila tu ama watu husoma na kuibuka na kipande kidogo kwa faida zao au tu basi tu tabia yetu kizazi cha sasa kutafuta angle ya kushusha kitu au kumshusha mtu. Ila tu kwa kuwa kweli ni dawa ya uhuru, huwa haisumbui Sana baadae wale au yule aliyelipindisha huja kukiri tu.

Siku hizi nimekuwa bibi mwelimisha jamii[emoji1]. Jumamosi njema na baraka kwako.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Andika vizur basi huo uandishi umefunzwa wapi KAZI ukaidi Tu hata Sheria za uandishi huna kisha kuja shindana na Dkt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…