Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Kunyoa kiduku Ni chanzo cha kuporomoka maadili, wanyoa viduku ndio hao wavuta bangi na vibaka kutohusianisha hiyo staili na hizo tabia inakuwa ngumu, lakini Kama jamii imeliona hilo kuwa Ni chanzo wizara husika na sisi wasomi sasa ni kuunga mkono kwa hatua ya Kwanza kutoka hapo ndio ushauri na namna nyingine ifuatwe, wewe ulitaka waziri apinge? Ingekuwa ni namna ya kufisha juhudi za wananchi katika kuhakikisha jamiii inakuwa na maadili. Hivi kwa mawazo yako hivi huon Kama viduku na uvaaji wa nguo fupi pamoja na mambo mengine unachangia kuporomoka kwa maadili? Umewataja wamasai kwamba wananyoa kiduku hebu waza kwa sauti hao wamasai ushasikia ni vibaka? Wana namna yao ya kuhakikisha jamii yao ina maadili
Ndugu yangu, ahsante kwa mchango wako kwenye mada hii. Ni Katika wadau tu kuchangia hoja mbalimbali ndiyo tutajenga jamii yetu kutazama mambo Kwa sura mbalimbali kulingana na mazingira.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
UPO SAHII MH
LAKINI KIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA YA SASA ILIYOPO MADARAKANI AKIKUAMBIA NJOO TUSHIRIKIANE KUTAFUTA UFUMBUZI WA TATIZO LAZIMA UJIFIKIRIE MARA MBILI MBILI.
NB:HISTORIA NA KUMBUKUMBU NI MWALIMU MZURI SANA NA NDIO MAANA MZEE KIKWETE AKASEMA AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO
Maandishi yako makubwa yanaumiza macho ,hapa si vitani andika kwa herufi ndogo utaeleweka vizuri tu.
 
Ni lazima kulinda maadili. Kuachia Mmomonyoko ni hatari kwa jamii. Nipongeze kijiji cha Arumeru kwa ujasiri na upendo kwa vijana wao.
Vijana ni msingi wa taifa ni lazima wahifadhiwe ki maadili.
Ila kule dodoma wakifanya mmomonyoko wa maadili kama yule naibu waziri sio hatari.Lakini madogo wa Arusha wakinyoa viduku ni hatari
 
Ulienda shule kusomea ujinga ndio sababu unaelimishwa unashupaza fuvu. Unashikilia kuvaa kimini badala ya kuangalia mzizi wa sheria za watu wa arumeru.
😂😂😂 acha kupanic Mkuu, chagia mada kwa hoja mjadala uende vizuri... vimini, jinzi, mitindo ya nywele si chanzo cha kuharibika kwa maadili....mambo yametokea enzi na enzi leo ndio tunasema yanaharibu jamii? Jamii ingekuwa imepotoka kitambo sana kama hili lingekuwa kweli. Unakubali kuwa wizi kwenye kijiji hicho umetokea sababu ya mavazi na mitindo ya nywele? Embu kuwa serious bwana
 
Hamia Marekani. Acha kubishabisha kipuuzi. Mheshimiwa waziri kwenye uzi mmoja kajitahidi kufafanua ila wewe umeng'ang'ania kubisha. Pumbavu sana. Nadhani mimi utanielewa kwasababu kistaarabu huelewi.
Ndio maana ya kubishana kwa hoja na matusi wala kejeli, kutukana na kutumia lugha mbaya inaonesha tu uwezo wako mdogo kichwani... mwenye uelewa wala hajapinic na anachangia mada vizuri tu, una la kujifunza hapo. Ukiangalia upande mzuri wa kitu angalia na upande mwingine wa shilingi
 
Nimpongeze Mheshimiwa waziri kwa majibu mazuri na elimishi.
Kwa upande wangu, mporomoko wa maadili unaanzia kwenye uvaaji; akina dada nguo za kubana, vimini, mipasuo (inayoacha nje sehemu kubwa ya mapaja) na suruali(jeans) zenye chane na kwa kina kaka kuvaa mlegezo. Uvaaji huo unaweza kupelekea msisimko wa mwili hivyo kuvuta hisia na kuhamisha akili ya mtu mwingine na kumletea mawazo hasi. Mitindo ya nywele sina tatizo nayo kwani sidhani kama ina athari zozote. Hivyo basi, jamii ielimishwe katika eneo hilo la uvaaji wa mitindo
sisimuzi.
Kuhusu kukaa bila kazi nyakati za mchana, nina imani kila mtu ana kwao/ kwake eneo anapoishi. Na kuna viongozi wa mitaa, basi hao viongozi wahakikishe wanajua shughuli za kila mtu anayeishi eneo lake na sheria ndogo za kudhibiti vitendo viovu (pengine vya kuiga mitandaoni) zinatungwa na kusimamiwa ipasavyo.
Kwa sheria na adhabu nilizoziona kwenye hiyo jamii, Vijana wanaweza kutoroka taratibu na kulowea ktk miji isiyo na hizo sheria hasa miji mikubwa ambako wanaweza kuharibika zaidi.
Asante kwa mchango wako Mkuu, nina swali kidogo hapa... kuna jamii ambazo wanavaa vipisi vya nguo kama utamaduni wao na husikii mambo ya kumomonyoka kwa madili wala vitendo vya ukatili... suala la kumsababishia mtu ushawishi sababu fulani kavaa nguo fupi au iliyochanwa sio kwamba inatumika kama kisingizio cha kuhalalisha vitendo vibaya kufanyika? Unatenda kosa na kumtupia mtu lawama kwa kushindwa kutuliza tamaa zako?
 
Ni lazima kulinda maadili. Kuachia Mmomonyoko ni hatari kwa jamii. Nipongeze kijiji cha Arumeru kwa ujasiri na upendo kwa vijana wao.
Vijana ni msingi wa taifa ni lazima wahifadhiwe ki maadili.
Swali je, ni mitindo ya nywele na mavazi ndio mzizi wa mmomonyoko wa maadili?
 
Acheni kuwa mashabiki wa ujinga watu wa aina hii ndio mmekuwa vichocheo vya ushoga na mmonyoko wa maadili Kwa nyanja mbalimbali.
Leta hoja mkuu, kivipi kiduku kinaleta mmomonyoko wa maadili, tuweke hisia pembeni na kuangalia mzizi wa tatizo. Usiniambie vijana wamejiingiza kwenye wizi na matendo mengine maovu kisa mtu kanyoa kiduku au kavaa jinzi. Ili kumaliza vitendo hivyo ni muhimu kujua tatizo limeanzia wapi na sio kutupia lawama kwenye vitu ambavyo ni rahisi kuwa midomoni mwa watu na kukwepa kuwajibika
 
Naona tunachanganya kati ya kutembea uchi na mtu kuvaa nguo fupi ambayo wala haikuthiri wewe kwa lolote. Si kosa mtu kuvaa nguo fupi imani na jinsi unavyoona/kuangalia vitu ndio inakufanya utake watu wawe kwa namna fulani ambayo wewe haikupendezi. Tatizo si nguo fupi wala kiduku, ni mambo uliyohusanisha na viduku pamoja na nguo fupi. Baba, mama, dada kunyoa kiduku au kuwa na nguo fupi wala hainipi shida, imekuwa hivyo toka enzi, wala si maajabu kuwa wameleta kitu kibaya chenye kuharibu uhai na maisha ya watu...kuna mambo mabaya ya kupiga vita viduku na nguo fupi si kati yao
enzi zipi zilivaliwa
 
Dkt gwajima D. ni waziri anayefanya kazi zake kama zima moto "reactive" siyo "proactive".

Kama ni daktari wa binadam simshangai, ndivyo uzoefu wa madaktari ulivyo. kazi zaoni kuzima moto tu.


Ulishwahi kusikia Daktari yupi wa Tanzania kabuni kitu kipya kwa ubunifu wake? Labda abuni porojo na ngonjera (theories) tu.
 
Habari za mchana.

Kwanza ahsante kwa kufuatilia habari za jamii.

Halafu, mimi ningekuwa wewe nataka kutoa ushauri kwanza ningeanza hivi;

Nashukuru Mungu sasa jamii imeanza kutambua umuhimu wa kudhibiti mmomonyoko wa maadili jambo ambalo ni kilio kikubwa na walau wanakaa na kujadili hata kama mijadala yao inaweza ikawa labda ina changamoto. Hii ni hatua moja.

Halafu ningeshauri kuwa, sasa tafadhali, wataalamu wa Maendeleo na Ustawi na wengine mbalimbali waende wakae na jamii hii wawaongoze vema Ili Nia yao nzuri isiishie njiani hasa ukizingatia kwamba yako mambo mengi ya kutazama.

Hapo mm ningeona ushauri wako mzuri sana na wewe ungekuwa pengine mwanatimu hiyo, kama mwingine aliyetoa ushauri makini kwenye ukurasa wa BASATA jana sasa tunamtumia.

Hii habari ya WAKATI WOTE kuwa NEGATIVE tu na jamii na kuibua MABAYA TU mema hapana mimi binafsi nakataa na ndiyo kinachotuzamisha sisi nchi nyingi za bara letu. Lazima tujue kupokea, kushauri na kurekebisha kwa hekima na kutia moyo wengine.

Hakuna jambo gumu kama kuifanya jamii Ione wajibu wao, hivyo wanapouona ni HATUA MOJA na wanapohitaji technical support ni HATUA INGINE.

Kwa taarifa yako, sisi kupitia uzoefu huu sasa tunapeleka maelekezo kote wakae wafanye mipango chini ya wataalamu kupitia hatua hii ya kuwa, jamii IMEONA KIU ya kufanya mabadiliko.

Hata hivyo, AHSANTE SANA kwa mchango wako. Pongezi kwao SITATENGUA ila tunaenda na wataalamu huko ili twende nao kisayansi zaidi maana hii ni safari ya mabadiliko ya fikra za jamii.

Ubarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Asante kwa kuongeza ufafanuzi huu, maelezo ya kwanza hayakuridhisha, kwa kupeleka wataalamu walau hapo unatoa matumaini kuwa kutakuwa na muongozo na maboresho kwa kile walichokianzisha👏👏
 
Dkt gwajima D. ni waziri anayefanya kazi zake kama zima moto "reactive" siyo "proactive".

Kama ni daktari wa binadam simshangai, ndivyo uzoefu wa madaktari ulivyo. kazi zaoni kuzima moto tu.


Ulishwahi kusikia Daktari yupi wa Tanzania kabuni kitu kipya kwa ubunifu wake? Labda abuni porojo na ngonjera (theories) tu.
Ahsante Sana kwa evaluation yako. Sasa zimamoto ipi tena iwapo mpango Mkakati kutokomeza ukatili upo rasmi na tunaelimisha utekelezwe na jamii ila jamii inajivuta ukiwemo wewe hapo. Tena wewe ni mtoa mada humu miaka mingi ambaye nilidhani na wewe ungekuwa proactive kuelimisha jamii kuhusu huu mpango tangu uzinduliwe uwe Balozi, kumbe na ww unasubiri tu ku react kwenye taarifa za hapa na pale.

Halafu wanajamii wengine wakitekeleza mpango tukasema tukawape moyo mnasema tuko reactive. Kumbe hiyo proactive inakuwa yangu peke yangu nyie jamii hamtakiwi kuwa? Kumbe itakuwaje Sasa wakati mpango ni wa wizara na jamii.

Hata hivyo, ahsante Sana kwa mchango wako ila sasa amka upite google usome MTAKUWWA kisha urudi uangalie ww hapo kwenye eneo lako jukumu lako lipi Ili likitokea tatizo usiwe reactive wewe na jamii yako Bali muwe proactive. Hbr za asubuhi lakini.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa kuongeza ufafanuzi huu, maelezo ya kwanza hayakuridhisha, kwa kupeleka wataalamu walau hapo unatoa matumaini kuwa kutakuwa na muongozo na maboresho kwa kile walichokianzisha[emoji122][emoji122]
Maelezo yalikuwa sawa tangu mwanzo ila tu ama watu husoma na kuibuka na kipande kidogo kwa faida zao au tu basi tu tabia yetu kizazi cha sasa kutafuta angle ya kushusha kitu au kumshusha mtu. Ila tu kwa kuwa kweli ni dawa ya uhuru, huwa haisumbui Sana baadae wale au yule aliyelipindisha huja kukiri tu.

Siku hizi nimekuwa bibi mwelimisha jamii[emoji1]. Jumamosi njema na baraka kwako.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
MH UNA SIASA NZURI ZA KIDPLOMASIA ILA NATUMAINI UMENIELEWA KAMA MSOMI
NB:MUNGU HAPENDI UNAFIKI NA YOYOTE ANAYEWALAUMU VIJANA WA KITANZANIA KUA HAWANA MAADILI,LAZIMA AKEMEE PIA NA VIONGOZI WA SERIKALI KWA KUKOSA MAADILI PIA.
SISI VIJANA TUNAWATAZAMA VIONGOZI KAMA VIOO NA TUNAIGA CHOCHOTE WANACHOFANYA KWENYE MAISHA YAO YA KILA SIKU.
MMOMONYOKO WA MAADILI UMEANZIA JUU KWA VIONGOZI ILA WATANZANIA WANAOGOPA KUSEMA KWA KUHOFIA MKONO NA NGUVU YA DOLA.
SABABU TANZANIA NI KUFURU KUMKOSOA KIONGOZI HASA KWENYE NGAZI ZA KITAIFA.
Andika vizur basi huo uandishi umefunzwa wapi KAZI ukaidi Tu hata Sheria za uandishi huna kisha kuja shindana na Dkt
 
Back
Top Bottom