Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Safi sana mh Waziri,tunataka jamii zinazojitambua
 
Ahsante Sana kwa mchango wako. Tayari tumeimarisha umoja na BASATA na COSOTA na Bodi ya FILAMU katika hili. Naamini safari yetu ya kuimarisha mifumo husika itaenda salama na kudhibiti haya mambo. Tayari ma MC na maafisa utamaduni wamepelekewa maelekezo ya kukumbushwa wajibu wao ambao uko kwenye mipango yao ila sijui kwa nn baadhi ya watu wanaishi hadi wakumbushwe. Ila tutafika.

Ngoja nitafute picha hapa ya 12 Sept 2023 tulipoanzia safari.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Pongezi zimefika, maana kesho tutakuwa nao.

Sisi hili bara letu, tutasonga mbele tu kwa kupendana na kuamini kuwa Kila mmoja anao mchango anataka kwenda pazuri na Ili afike huko, anahitaji kuanzisha mwendo na apate ushirikiano wa jamii na wataalamu mbalimbali kwenye safari yake Ili afike salama. Ubarikiwe [emoji1666]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani hili nimejibia, kuwa, mpango ni huo phase one ni hiyo Iko online, imetekelezwa imeisha juni 2022. Tathmini imefanyika na wataalamu watafiti wabobezi kuanzia huko ngazi ya jamii Hadi taifa, na Sasa umeshaandaliwa mpango mpya wenye mambo mapya na ubunifu tele tele. Utatoka Novemba 2022 tunaadhimisha hizi siku 16 za kupinga ukatili.

Hivyo kukupeleka google uone wa zamani ni Ili Hadith yetu ya engagement ianzie kwenye background hiyo. Halafu acha nijisifie mwenyewe kuwa, sidhani kama mm ni miongoni mwa watu wapenda porojo Ili nimpoteze mtu... 😅 sidhani. Ila kufikiriwa hivyo napo sawa tu....

Na ukisoma humo ndani utaona role ya wizara ya Jamii ni uratibu wa kisekta, kamati tendaji Iko hapo na Sasa kwa ubunifu tumepanua muundo Ili machinery hii ifanye kazi kitofauti hadi ngazi za mikoa na wilaya. Nisimwage mtama kwenye yaliyomo yasubiri uzinduzi.

Ila msiwe na hasira hasira jamani... hoja ngumu zahitaji utulivu utulivu [emoji847]

Ndugu zangu, nimewaongezea na kapicha la siku ile tumekusanya sekta zote kwenda kujadili tathmini ya MTAKUWWA iliyoisha 2022 na ile ijayo. Someni iliyoisha Ili mje msome na ijayo kisha mje sasa na maoni, mm nitapokea na nitakuja Twitter space kabisa huko huko tuongee mchambue mwanzo mwisho. Ahsante sana FaizaFoxy kwa kuchangia mjadala moto moto kabisa 🤝🇹🇿🔥💪

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 

Attachments

  • IMG-20231014-WA0007.jpg
    72.3 KB · Views: 2
Amina umefafanua vzr kimantiki kabisa na mifano hai

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwa aina ya mtindo wa maisha ya vijana walio wengi kwa jinsia zote hao wazee kwenye hiko kijiji na msimamo wa waziri dhidi ya ajenda yao hilo nadhani wapo sawa.

Nadhani pia kwa msaada wa serikali na wizara husiki inaweza kuwa mwanzo mzuri wa jamii kuanza wajibu wa kurudisha maadili kwenye jamii husika .

Maoni yalio wasikishwa kwenye mada hii na majibu ya waziri yanatia moyo sana haswa sisi vijana tunao ona vijana wenzetu wakiwa kwenye uvunjifu mkubwa wa maadili kwa kuiga mitindo mibovu kutoka kwa wafu wasio paswa kuigwa .

Tulipo jaribu kuwaambia vijana wenzetu juu y mitindo huo wanayo iga kwamba sio rafiki kwa hatma ya maisha yao walitubeza na kutuona washamba tusioenda na wakati .

Inapotokea hoja na mijadala kama hii na maazimio kutoka Kwa wazee wetu kama hao wanaojadiliwa hapa tunaona mwanzo mzuri wa ujenzi wa maadili mema kwa vijana wenzetu.

Kwenu wizara natumaini mna watendaji na maafisa wenu kwenye wilaya kata na hata vijiji, wanaweza kuwa mabalozi kwa jamii nyingine huko wanako hudumu kuwaeleza kwamba kijiji cha arumeru huko Arusha wamechukua uamuzi wa kurudisha maadili kwenye jamii yao kwa mfumo huu nasi kama serikali ama wizara tukawapa mwongozo huu, mnaweza pia nanyi kuutumia kwa lengo ya kufanya jamii kuwa na maadili .

Hii inaweza kuleta mabadiliko ya namna fulani baada ya miaka kadhaa, tukawa na taifa la vijana wenye maadili na wasio pelekwa na kila aina ya mitindo inayoibuka .

Kwako mh waziri Dkt. Gwajima D pole na hongera kwa uvumilivu wa maoni unayoyapata hapa Jf, sio leo wala kesho utaacha kukutana na maoni yanayovunja moyo, yanayokejeli , yanayoishi na kila namna isioleta furaha, kamwe hakuna jinsi utayakwepa haya maadamu upo hapa kwa utambulisho wa wazi, sio vyepesi kwa mtu wa nafasi yako kuwa kama wewe, wewe mwenyewe ni shahidi na sisi wote tu mashahidi.
Hii ni kwa sababu ya kuepuka kadhia za namna huo ndio maana wengi wa nafasi kama yako hawapo kama wewe.

Ombi langu kwako uendelee kuwepo hapa, uwepo wako hapa umekua mchango chanya mkubwa kuliko unvyo dhani, umekua mkubwa kiasi hakuna maelezo ya kutosha kusema .

Tuvumilie , tujibu kiustaarabu, nasi wengine tunakuunga mkono hatutaacha kukutetea kwenye hoja inayojenga , kukosoa panastahili, na kutoa maoni panapo hitajika.
Tunakushukuru sana .
 
Unaonaje turudi kuishi mapangoni na tukawashe vibatari vya kupekesha moto kwenye mchanga[emoji847] Ili turudie mambo yote ya kale....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mh. Hiyo haikuwa hoja yangu hata kidogo, ni vyema ufahamu kuwa viduku, rasta, vimini nk. Hakijawahi kuwa kipimo cha uvunjifu maadili, haya engine upita na upepo wake na maisha yakaenda vizuri kabisa. Miaka yenu ya ujana vimini ilikuwa ni fashion, ikapotea na kurudi na itapotea tena.
 
Nipo pamoja nanyi hadi ukamilifu wa kazi hii niliyopewa.

Moyoni mwangu nilishatanguliza kusimika misingi ya hekima ya wenye hekima, Niko Nuruni tayari hakuna jipya tena la kuniweka mbali na maoni ya jamii Kwa sura zote maana nami ndiyo hapo ninapopenyeza ajenda halisi za wizara yao na penye kujifunza najifunza ila siwaachi jamii na mm ndiyo saiti zangu, tutazoeana tu [emoji28][emoji1666]

Ahsante Sana ubarikiwe kwa muda wako na maoni yako...

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mpumbavu. Waziri kafafanua zaidi ya mara moja lakini bado unakaza fuvu kama mwendawazimu.
 
Ahsante Sana nashukuru kama hakika haikuwa hoja yako.

Sasa nadhani mm kwa maoni yangu Kila mara narudia kwamba: haya yote yaliyoanzishwa na jamii kwenye mjadala wao, kazi ya mifumo na wataalamu ni kuyajengea utaratibu wa mijadala waulizane waelewane wajue na mambo mengine kisha wahitimishe wao.

Na kwa kuwa hawatahitimisha kwa mtutu wa bunduki Bali fikra zao zitabadilika wao wenyewe kwa ridhaa yao, unaweza kukuta hata vijana wa huko wanaodhani sasa kufanya hivi au vile ni fasheni, wakaja hapa na ushuhuda kuwa, aisee tumeona haifai kabisa sijui ilikuwaje, hata kama linafaa kwingine.

Narudia tena kusema kuwa, hakuna sare sare Duniani na kilicho sare kule kinaweza tu kukataliwa kwingine bila shurti na jamii fulani ikawa na utaratibu wao usiovunja sheria wala katiba na ukapendwa tu na jamii ingine vilevile.

Mkinielewa point hii, mtavuta subira muone jamii hii iliyojadili haya mwisho itafika wapi. Je wakikubaliana hivyo kwa wema pasi na shurti atatokea mtu aende awaambie haya nyie nyoeni hivi vaeni vile?

Mm labda ndiyo sijawaelewa? , ila sisi tunachowapa ushirikiano huko ni kile nimekisema kwenye video....

Hii hapa sikiliza, wapi labda ndugu yangu mpendwa hujaelewa? Niko kwa ajili ya jamii nitakuja nijibu au nifafanue nk. Ahsante sana
Your browser is not able to display this video.


Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ubarikiwe sana Mh.
 


Mambo ya msingi kwa nchi hii ni pamoja na kulinda na kutunza maadili ya wananchi wa nchi hii.


Kila jamii inazo Mila, Desturi na Tamaduni zake na ni wajibu wa hizo jamii kuzilinda na wao wameamua kulinda Mila, Desturi na Tamaduni zao kwa style hiyo.

Kijiji kutokua kisiwa haina maana kiache kuzingatia taratibu zao za maisha kwa mujibu wa Mila na Tamaduni zao.

Tujifunze kuheshimiana na kuheshimu mipaka baina yetu.
 
Lina koneksheni gani na uhalifu au mmomonyoko wa maadili. Hadi Karne iliyopita tulikuwa tukicheza ngoma za asili huku wadada chuchu zikiwa nje.


Kwamba jamii zote za watanzania wa nchi hii walikua na Tamaduni za kucheza ngoma, tena wakiwa uchi?


Halafu ukosefu wa mavazi na uwezo wa jamii kuyapata hayo mavazi enzi hizo umezingatiwa kwa kiasi gani kwenye hoja yako hii?
 
Kwahiyo unashauri watoto wa kike watembee uchi,wanyoe viduku,na vijana wa kiume wavalie suruali mpaka kwenye magoti ?

Binafsi nimezipenda Sheria zilizo letwa na nampongeza waziri

lakini pia natamani zienee inchi nzima Kama ikiwezekana

Hivi inakuaje mtu una mguu size 5 afu unaenda kununua kiatu size 45 si bange hizo?

Af wanajisifu ndiyo mkoa wenye watu wa janja tz nzima😂😂😂
 

Kwamba kwa sababu kuna viongozi na vijana wa hovyo kila sehemu basi juhudi za kurekebisha zifutiliwe mbali na kusahaulika kabisa?

Ukitambua kwamba hao Viongozi unaowalaumu ni zao halisi la jamii zetu utaelewa ni kwanini hiyo jamii ya hicho kijiji imechukua hatua hizo katika jitihada za kulinda maadili na Tamaduni zao.

Watanzania hawawezi kuwalaumu hao viongozi kwa maana wao na hao ni zao kutoka shamba moja japo mbegu tofauti.

Hatua ya hiyo jamii kusimamia Mila, Tamaduni na Maadili yao ni Nzuri mno na yenye kufaa kuigwa na kila mwenye upeo unaojitegemea na mwenye kutambua umuhimu wa kesho yetu iliyosafi na utaifa wetu kwa Umoja wetu mbali ya tofauti zetu za kikabila na kiImani.




Tujifunze kushirikiana katika kheri tunapopata japo kiongozi mmoja mwenye nia thabiti ya kushirikiana na sisi kuyafikia malengo yetu na ya jamii zetu.







PS; Tafadhali acha kumfokea Doctor Gwajima na hizo CAPS zako, kuwa na Adabu.
 
Kila jamii ikiset rurels zake kulingana na invyotafsiri 'maadili' nini kinatengenzwa hapo?


Itatengenezwa heshima na ustaarabu miongoni na kati ya hizo jamii.

Hizo jamii zitatambua mipaka kati yake na kuilinda.

Jamii zitasimama imara kujilinda na kulinda mazingira yao na hatimaye utaifa utasimama tena ndani yetu na nchi kuimalika katika malengo na safari yake.

Jamii yoyote isiyotambua wala kuheshimu mizizi yake ni jamii mfu kwa maana inapotezwa na upepo tu uvumao kuelekea popote bila dira maalum.

Mizizi yetu ndio misingi yetu ndani ya family zetu, jamii zetu na taifa letu kwa ujumla.





Kumbuka; kila jamii hapa duniani ina identity (utambulisho) wake, haijalishi ni mdogo kiasi gani, lakini leo hii ukiulizwa utambulisho wa Mtanzania/ Mtanganyika ni upi, unaweza kuusema ama kuuonyesha?
 


Ukuaji wote huu wa technology bado tunashindwa kutafuta usahihi wa yale tuliyofundishwa na kukaririshwa hapo kabla?

Kwa mazingira ya kuishi nyikani (Tanganyika) kwa pamoja na wanyama wa porini, huyu binaadam anapata wapi duka la mavazi ili aache kuvaa vipisi vya nguo?

Huyo binaadam alikua karibu kiasi gani na kiwanda cha kutengeneza mavazi ya kujisitiri mwili wake?

Ni ipi tafsiri yako/ sahihi ya neno Tamaduni? Neno Mila? Neno Desturi?

Unayo taarifa yoyote ya maisha ya mtanganyika miaka kati ya 1500 na 1800?






Maasai anavaa shuka tupu, Mang’ati pia, lakini ni wapi umewaona waki modify mavazi yao na muonekano wao kuufanya uwe wa kisasa (sexualiteit) zaidi?

Haya mavazi ya bafuni wanayovaa wakina dada barabarani na sokoni sasa hivi ndio unafananisha na hivyo vipande vya magome ya miti na ngozi za wanyama?
 
Swali je, ni mitindo ya nywele na mavazi ndio mzizi wa mmomonyoko wa maadili?


Chimbuko la huo mtindo wa kunyoa wa kiduku ni wapi? Ni jamii ipi ina utaratibu huo?

Kwanini vijana wa Tanzania waige taratibu na mitindo kutoka jamii zingine? Hawana taratibu na mitindo yao ya nywele wakasimama nayo?



Kijana wa kiume wa Maasai hajawahi kunyolewa wala kulazimishwa kunyoa nywele zake ndefu. Hujiulizi ni kwanini?
 


Kwamba wewe ndio mjuzi sana kuliko Waziri na team yake ya wasaidizi na wataalamu?

Kwamba haya uliyoweka hapo juu ni wewe pekee uyajuayo na kuyatumia katika kutimiza wajibu wako?

Ni rahisi sana kukand’ya juhudi za wengine na wakati huo huo tukitumia nafasi hiyo kudisplay Ego zetu na kujivua nguo hadharani.

Maandishi yako yanakutafsiri Kama mwanamke hasiyekua na stara katika kinywa chake na mwenye kutenda ili kufurahisha watu fulani. (If a parasite was a human….)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…