Kwa aina ya mtindo wa maisha ya vijana walio wengi kwa jinsia zote hao wazee kwenye hiko kijiji na msimamo wa waziri dhidi ya ajenda yao hilo nadhani wapo sawa.
Nadhani pia kwa msaada wa serikali na wizara husiki inaweza kuwa mwanzo mzuri wa jamii kuanza wajibu wa kurudisha maadili kwenye jamii husika .
Maoni yalio wasikishwa kwenye mada hii na majibu ya waziri yanatia moyo sana haswa sisi vijana tunao ona vijana wenzetu wakiwa kwenye uvunjifu mkubwa wa maadili kwa kuiga mitindo mibovu kutoka kwa wafu wasio paswa kuigwa .
Tulipo jaribu kuwaambia vijana wenzetu juu y mitindo huo wanayo iga kwamba sio rafiki kwa hatma ya maisha yao walitubeza na kutuona washamba tusioenda na wakati .
Inapotokea hoja na mijadala kama hii na maazimio kutoka Kwa wazee wetu kama hao wanaojadiliwa hapa tunaona mwanzo mzuri wa ujenzi wa maadili mema kwa vijana wenzetu.
Kwenu wizara natumaini mna watendaji na maafisa wenu kwenye wilaya kata na hata vijiji, wanaweza kuwa mabalozi kwa jamii nyingine huko wanako hudumu kuwaeleza kwamba kijiji cha arumeru huko Arusha wamechukua uamuzi wa kurudisha maadili kwenye jamii yao kwa mfumo huu nasi kama serikali ama wizara tukawapa mwongozo huu, mnaweza pia nanyi kuutumia kwa lengo ya kufanya jamii kuwa na maadili .
Hii inaweza kuleta mabadiliko ya namna fulani baada ya miaka kadhaa, tukawa na taifa la vijana wenye maadili na wasio pelekwa na kila aina ya mitindo inayoibuka .
Kwako mh waziri
Dkt. Gwajima D pole na hongera kwa uvumilivu wa maoni unayoyapata hapa Jf, sio leo wala kesho utaacha kukutana na maoni yanayovunja moyo, yanayokejeli , yanayoishi na kila namna isioleta furaha, kamwe hakuna jinsi utayakwepa haya maadamu upo hapa kwa utambulisho wa wazi, sio vyepesi kwa mtu wa nafasi yako kuwa kama wewe, wewe mwenyewe ni shahidi na sisi wote tu mashahidi.
Hii ni kwa sababu ya kuepuka kadhia za namna huo ndio maana wengi wa nafasi kama yako hawapo kama wewe.
Ombi langu kwako uendelee kuwepo hapa, uwepo wako hapa umekua mchango chanya mkubwa kuliko unvyo dhani, umekua mkubwa kiasi hakuna maelezo ya kutosha kusema .
Tuvumilie , tujibu kiustaarabu, nasi wengine tunakuunga mkono hatutaacha kukutetea kwenye hoja inayojenga , kukosoa panastahili, na kutoa maoni panapo hitajika.
Tunakushukuru sana .